Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mkewe

Mshtakiwa Ally Balanda Idofulo (kushoto) akizungumza na wakili wake, Roman Lamwai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kuhukumiwa kifungo cha kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kwa kukusudia mke wake aitwaye Selan Kondo. Picha na Hadija Jumanne.

Muktasari:

  • Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salalam, iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, All Balanda Idofulo, kunyongwa hadi kufa, baada kupatikana na hatia ya kumuua mkewe, aitwaye Selan Kondo kwa kumchoma kisu begani.


Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salalam, iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, All Balanda Idofulo, kunyongwa hadi kufa, baada kupatikana na hatia ya kumuua mkewe, aitwaye Selan Kondo kwa kumchoma kisu begani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Septemba 26, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, aliyepewa mamlaka ya nyongeza kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.

"Kwa namna yoyote ile, nimejiridhisha kuwa mshtakiwa ulimuua Kondo kwa kumchoma  kisu begeni baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wanane akiwemo mtoto wa marehemu mwenye umri wa miaka minane, ambaye aliieleza mahakama kuwa alishuhudia ukimchoma kisu mama yake begani baada ya kutokea msuguano baina yako na marehemu," amesema hakimu Kiswaga na kuongeza

"Kwenye kosa hili la mauaji ya kuua kwa kukusudia, hakuna nafuu iliyotolewa na sheria zaidi ya adhabu ya kunyongwa, hivyo mahakama hii inakuhukumu kifungo cha kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii na haki ya kukata rufaa ipo wazi iwapo hujaridhika na adhabu hii," amesema Hakimu Kiswaga.

Idofulo anadaiwa kumuua Selan Kondo, Mei 6, 2019 eneo la Tabata Liwiti, Wilaya ya Ilala.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alimuita Kondo waonane ili wajadiliane namna ya kurudiana baada ya kutengana kwa muda.

Endelea kufuatilia mitandao yetu.