Maganga wa CWT, wenzake wadakwa na Polisi

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga.

Dodoma. Jeshi la Polisi limewakamata  wanachama 10 wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Japhet Maganga kwa tuhuma za kusababisha fujo kwenye mkutano wa chama hicho.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Februari 17, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema kuwa wanachama hao walikamatwa katika mkutano wa chama hicho jana.

“Tulipata taarifa kuwa kuna watu wanafanya fujo tukaenda kudhibiti kabla hayajatokea madhara kwenye mkutano huo, sisi hatujui ilikuwaje zikatokea fujo waulizwe CWT wenyewe,”amesema Kamanda Otieno.

Mwananchi Digital ilipomtafuta Rais wa CWT, Leah Ulaya alijibu yupo kwenye kikao na kwamba angezungumzia jambo hilo baada ya kumaliza kikao.


Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea kurasa zetu.