Mradi wa ‘Kijani Zaidi’ wasaidia mkakati wa taifa wa upandaji miti

Ikiwa imetekelezwa kwa ushirikiano wa karibu na serikali, mafanikio ya miradii hii inaonyesha umuhimu wa kuhamasisha na kuunga mkono jitihada za kuongeza hamasa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, athari zake, na kuzizungumzia

Muktasari:

  • Miradi yote miwili inaonyesha maendeleo chanya na imefikia malengo iliyojiwekea, kama vile kurudisha ustawi wa misitu ya Pwani kupitia uhifadhi wa Vikindu na Pugu-Kazimzumbwi, mipango endelevu wa utalii, na kuunga mkono usimamizi wa jitihada za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.  

Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na WWF-Tanzania imetekeleza miradi ya Kijanisha Dodoma na Kijani Zaidi katika wilaya za Mkuranga na Kisarawe ikiwa ni sehemu ya mipango ya kampuni kupitia shughuli za uwajibikaji kwa jamii za Kitanzania. 

Mradi wa ‘Kijanisha Dodoma ulizinduliwa 2019 kwa lengo la kuunga mkono mkakati wa taifa wa serikali wa upandaji miti kwa kupanda miti takribani 100,000 jijini Dodoma na kuhamasisha usimamizi endelevu wa taka mkoani humo. Mradi wa ‘Kijani Zaidi’ ulianza 2020 ikiwa ni jitihada za kurudisha ustawi wa misitu ya Pwani ya Vikindu na Pugu-Kazimzumbwi kupitia uhifadhi na mpango endelevu wa utalii.

Miradi hii imeonyesha mafanikio makubwa kwa kufanikisha malengo yake, kama ilivyoonyeshwa kwenye ripoti ya tathmini yam waka 2021/2022.

 ‘Kijanisha Dodoma’ imefanikiwa kwa asilimia 85 ambapo miti 71,782 ilipandwa, kati ya miti 100,000 iliyotarajiwa. Kwa kuongezea, mpango umetoa fursa za vibarua 412, wakiwemo vijana 245 na wanawake 167.

Pia, mradi umesaidia mapipa ya taka 10 yenye uwezo wa lita 1,100 kila moja kusaidia shughuli za usimamizi wa taka ngumu na kufanikisha kujenga uzio wa waya zilizoshikiliwa na nguzo za zege za kilometa 1,129 kuzunguka Msitu wa Medeli Mjini Halmashauri ya Jiji la Dodoma.   

Mradi pia umetoa mafunzo kwa wajasiriamali na wanawake na vijana kuhusu ujuzi wa shughuli za kiuchumi endelevu kwa mazingira zikiwemo ubunifu na uzalishaji wa mabegi ya plastiki Rafiki kwa mazingira, maarifa ya usimamizi wa biashara, huduma kwa wateja, na mikakati ya masoko.

 Matokeo yake vijana na wanawake 40,000 kutoka jamii husika zikiwemo taasisi za elimu Dodoma zilihusishwa moja kwa moja wakati zaidi 350,000 zikinufaika kwa namna nyingine.

‘Kijani Zaidi’ imechangia jitihada za kurudisha ustawi wa misitu ya Vikindu na Pugu-Kazimzumbwi kupitia uhifadhi na mpango endelevu wa utalii.

Vikundi vya vijana na wanawake vilipatiwa mafunzo ya kuzalisha mkaa mbadala kutoka msituni na mabaki ya shambani ikiwa ni jitihada za kukuza matumizi ya nishati safi.

Mradi uliwapatia mafunzo ya kimkakati na kujipatia teknolojia inayofaa ya uzalishaji, ambayo iliwawezesha kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo majiko, mikate, keki, na skonsi. Matokeo yake sasa wanaweza kujiingizia kipato cha shilingi 40,000 mpaka 60,000 kwa wiki, kwa mujibu wa Zuweina Farah, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania.

Mpango ulilenga kuviwezesha vikundi na kukuza shughuli endelevu za kiuchumi Pamoja na kuelezea changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Vitali viwili vya miti vimejengwa Mkuranga na Kisarawe vyenye uwezo wa kuzalisha miche mpaka 30,000.

Vodacom Tanzania imetumia rasilimali zake za kampeni za kimasoko redioni na jumbe fupi za maneno kujenga hamasa na mabadiliko ya tabia kuhusu uhifadhi wa mazingira mikoani, na pia ikihamasisha shughuli jumuishi za kijamii.

Miradi yote miwili inaonyesha maendeleo chanya na imefikia malengo iliyojiwekea, kama vile kurudisha ustawi wa misitu ya Pwani kupitia uhifadhi wa Vikindu na Pugu-Kazimzumbwi, mipango endelevu wa utalii, na kuunga mkono usimamizi wa jitihada za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.  

Ikiwa imetekelezwa kwa ushirikiano wa karibu na serikali, mafanikio ya miradii hii inaonyesha umuhimu wa kuhamasisha na kuunga mkono jitihada za kuongeza hamasa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, athari zake, na kuzizungumzia.

Pia, inasisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya serikali na taasisi binafsi kukusanya rasilimali na kupanua miradi ya aina hii nchini kote. Kwa kuchukua hatua muhimu kuelezea changamoto za mabadiliko ya tabianchi, tunaweza kufanikisha lengo la mpango endelevu wa dunia na kutengeneza mustakabali wa dunia yetu. 

Hayo yalielezwa pia na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango wakati wa uzinduzi wa mpango wa taifa wa upandaji miti mapema mwaka huu ambapo alisema, “upandaji wa miti unatakiwa kuzingatiwa ipasavyo nchini kote ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kusababisha maafa matoke mabaya.”

Vodafone, kampuni mama ya Vodacom Tanzania, ilitangazwa kuwa mshirika mkuu wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP27) yaliyoandaliwa na serikali ya Misri mwaka 2022. Hatua hii ni muhimu katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na athari zake ambapo inachangia kwenye kufanikisha lengo la maendeleo endelevu ya dunia kufika 2030.

 Pendekezo la Vodafone la kuzijumuisha huduma na teknolojia muhimu kwenye mifumo ya kidigitali, kama vile ‘mtandao jumuishi wa shughuli kwenye intaneti,’ unaweza kuzisaidia jamii kutunza nishati, kutengeneza miji Rafiki kwa mazingira, na kuongeza ufanisi wa sekta tofauti za kiuchumi kama vile usafirishaji na kilimo.

Kwa kuzingatia mafanikio haya, ni muhimu kukuza ipasavyo na kuunga mkono miradi ambayo inaongeza hamasa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, athari zake, na suluhisho.