Serikali yatoa fedha matengenezo barabara ya Songea-Njombe

Muktasari:

Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuanza matengenezo ya barabara ya lami Songea-Njombe ambapo kwa kuanzia kipande cha Songea-Lutukira kinatarajiwa kufumuliwa na kujengwa upya kwa awamu hadi Njombe.

Madaba. Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuanza matengenezo ya barabara ya lami Songea-Njombe ambapo kwa kuanzia kipande cha Songea-Lutukira kinatarajiwa kufumuliwa na kujengwa upya kwa awamu hadi Njombe.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Madaba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia Hassan kwa kupata tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundo mbinu Babacar Ndiaye ya mwaka 2022 pamoja na kuzindua mkakati wa kuwajengea uwezo na kuwainua kiuchumi Vijana wa jimbo la Madaba ikiwa ni pamja na kuhamasisha kushiriki sensa mwezi wa nane 23 mwaka huu.

 Alisema wananchi wa mkoa wa Ruvuma wanakila sababu ya kumpongeza Rais  Samia kwani ameta maendeleo makubwa hapa nchini na ameonyesha dhamira ya dhati ya kuboresha miundo mbinu ya Barabara, Madarasa , ambapo  tayari kipande cha  Barabara ya Luanda hadi Bandari ya Ndumbi kimetengewa fedha, pia kipande Cha Likuyufusi-Mkenda  kinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha Lami na tayari wamepata pesa.

Aidha, Sh600 milioni zimetengwa na na tayari Sh400 milioni zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya sekondari Madaba hivyo ameweza kufungua miundo mbinu ya barabara.

Kwa upande wake Mbunge Jimbo la Madaba Dk Joseph Mhagama alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye miundo mbinu bado wanachangamoto ya wananchi ambao nyumba zao zimejengwa kando kndo ya barabara ya Songea-Njombe ambazo zimewekewa X hawajalipwa fidia zao hivyo ameiomba serikali kuwalipa ili waweze kutafuta maeneo mengine na waende kufanya maendeleo .

Alisema Serikali ya awamu ya sita imedhamilia kuifungua barabara ya Mkiu-Liganga-Madaba wamedhamilia kuifungua barabara hiyo, Barabara ya wino, Magingo-Mtyangimbole zimepigwa x hivyo wananchi wameshindwa kuziendeleza ,wanamadaba wanakila sababu ya kumpongeza Rais.Samia Hassan kwa kuweza kupata pesa ya kujenga Barabara ya Songea -Makambako kwa kiwango Cha lami.

Dk Mhagama aliongeza kuwa , Hospitali ya Wilaya inajengwa  Madaba ,pia  kituo cha afya madaba kimejengwa kwa gharama ya zaidi ya milioni 500 na kinaendelea kuboreshwa na kimesaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma za upasuaji kwa wajawazito  ambao walikuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kupata matibabu Songea.kata Matetereka jumla ya sh 500milioni zimepelekwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha Afya.

"Madaba tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Samia Hassan kwa kupata tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu Babacar Ndiaye ya mwaka 2022 tunamuomba atusaidie kujenga Barabara kwa kwa kiwango Cha lami ya Mkiu-Liganga-Madaba na kuboresha Barabara ya Makambaku Songea."alisema Dk Joseph Mhagama

Aidha, kulipa fidia za nyumba zilizopo pembezoni mwa Barabara hizo ili kuharakisha ukuaji wa uchumi wa Wananchi wa Madaba na Watanzania.

Akiwazungumzia Mkakati wa kuwawezesha kiuchumi vijana wa jimo lake alisema, Vijana  wa Madaba wamejaliwa Wana Afya njema,wamesoma vizuri hivyo yeye kama Mbunge amedhamilia kuwasaidia vijana kutoka kwenye utegemezi na Katika kulijenga Taifa letu.

Amesema vijana wa Madaba wanahitaji kuwezeshwa tu hivyo amewagawa kwenye Makundi matatu eneo la kwanza ni kuwaendeleza kiuchumi, NMB wameeleza fursa ambazo watawapa vijana ili kuwainua,TFS pia wameeleza fursa mbalimbali za kiuchumi ili vijana waweze kunufaika nazo.

Ofisa maendeleo amekabidhiwa jukumu la kuwaunganisha vijana ili waone nini kifanyike ili kukuza uchumi wao.

Upande wa michezo,Fred Mbuna capten wa timu ya Taifa ambapo atakuwa anafatilia ligi inayotarajiwa kuanza hivi Karibuni na kuangalia wenye vipaji na kuwatambua.

Alisema, kipaji ni mtaji watumie vipaji vyao wapo ambao wamejaliwa vipaji vya Biashara watumie fursa kujifunza ili vikawanufaishe

"Mimi pamoja na mgeni rasmi tumejipanga kuhakikisha tunaendelea vipaji vyenu ili kesho mje mtulee ,"

Akitoa taarifa ya vikundi vya vijana vinavyojishugulisha na miradi mbalimbali ya kiuchumi ,Anita Makota Ofisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amesema, vikundi vya vijana 21 vyenye jumla ya wanachama 244 vimepata mikopo ya Sh110,906,500

Amesema, halmashauri hiyo imeendelea kujipanga kuhakikisha vikundi vyote vinawezeshwa kiuchumi vinatimuza adhima ya mikopo na kufuata mtiririkowa marejesho kulingana na Mkataba wa mikopo yao.