Fei Toto aendelea kumfukuzia Azizi Ki

Muktasari:

  • Fei toto amejibu mapigo hayo kwa kupachika bao dhidi ya Singida Black Stars (Ihefu) ambalo limeifanya Azam kuendelea kujikita katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 54.

VITA ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, imezidi kupamba moto kwa viungo washambuliaji  kufuatia nyota wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' usiku huu kujibu mapigo kwa fundi  wa Yanga, Stephane Aziz Ki.

Fei Toto amefunga bao pekee lililoipa Azam ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu katika pambano kali la Ligi Kuu lililopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex na kuifanya  bu timu hiyo kufikidha pointi 54 baada ya mechi 24 na kuganda nafasi ya pili nyuma ya Yanga yenye 58 kwa mechi 22.

Bao hilo lililofungwa katika dakika ya 13 ya mchezo huo linakuwa la 14 kwa Fei Toto, moja pungufu aliyonayo Aziz Ki mwenye 15 akiongoza orodha ya wafungaji wa ligi hiyo.
 
Aziz Ki alifunga bao la 15 jana katika Kariakoo Dabi wakati Yanga ikiizamisha Simba kwa mabao 2-1.

Fei toto ameonekana kuwa mwiba katika mchezo  huo kutokana na uhuru aliokuwa nao, huku akitumika nyuma ya Kipre Jr aliyecheza kwa dakika 85 kama mshambuliaji wa mwisho.

Licha ya Ihefu kuwa na mchezaji mzoefu kama vile, Joash Onyango aliyekuwa akicheza sambamba na Benjamin Tanimu kutoka Nigeria katika safu ya ulinzi waliipata kutoka kwa kiungo huyo ambaye aliinogesha safu ya ushambuliaji ya Azam.

Licha ya kupoteza, lakini Ihefu itajilaumu kwa kupoteza nafasi kadhaa ilizotengeneza.

Kwa matokeo hayo Azam imepunguza pengo la pointi baina yao na Yanga kutoka saba hadi nne, licha ya kuwa na mechi mbili zaidi dhidi ya watetezi hao wa ligi.

Pia Azam imeongeza pengo la pointi baina yao na Simba iliyopo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 kutoka kuwa tano hadi nane, japo imekuwa mbele kwa  michezo mitatu tofauti na Simba yenye michezo 21.

VITA ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imezidi kupamba moto kwa viungo washambuliaji  kufuatia nyota wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei toto kujibu mapigo kwa fundi  wa Yanga, Stephane Aziz Ki.

Fei toto amejibu mapigo hayo kwa kupachika bao dhidi ya Singida Black Stars (Ihefu) ambalo limeifanya Azam kuendelea kujikita katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 54.

Bao hilo ambalo alifunga katika dakika ya 13 ni la 14 kwa Feisal ambaye jana, Jumamosi alishuhudia mshindani wake katika vita ya ufungaji Aziz Ki akipachika bao la 15 katika mchezo wa watani wa jadi ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Mkapa.

Fei toto ameonekana kuwa mwiba katika mchezo  huo  ambao umechezwa kwenye uwanja wa Chamazi kutokana na uhuru ambao alikuwa nao huku akitumika nyuma ya Kipre Jr ambaye alicheza kwa dakika 85 kama mshambuliaji wa mwisho.

Licha ya Ihefu kuwa na mchezaji mzoefu kama vile, Joash Onyango aliyekuwa akicheza sambamba na Benjamin Tanimu kutoka Nigeria katika safu yao ya ulinzi waliipata kutoka kwa kiungo huyo ambaye aliinogesha safu ya ushambuliaji ya Azam.

Kwa matokeo hayo inamaana kuwa Azam imepunguza utofauti wa pointi baina yao na vinara Yanga kutoka saba hadi nne huku wakiwa mbele kwa michezo miwili.

Lakini Azam wameongeza utofauti wa pointi baina yao na Simba ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 46  kutoka tano hadi nane huku wakiwa mbele kwa michezo mitatu.