Kombe la Muungano larejea baada ya miaka 20

Muktasari:

  • Taarifa iliyolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wenzao wa Zanzibar (ZFF) imesema mashindano hayo yataanza mwezi huu kuanzia Aprili 23.

Hatimaye Kombe la Muungano limerejea tena nchini ikiwa imepita miaka 20 tangu kusimama kwa mashindano hayo mafupi yanayozijumuisha timu za Zanzibar na Tanzania Bara.

Taarifa iliyolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wenzao wa Zanzibar (ZFF) imesema mashindano hayo yataanza mwezi huu kuanzia Aprili 23.

Mashindano hayo yatafanyika Kisiwani Zanzibar kwenye Uwanja wa New Amaan Complex ikiwa ni kuelekea kilele cha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, mashindano hayo msimu huu yatashirikisha timu nne zilizothibitisha kushiriki zikiwemo mbili za Bara ambazo ni Simba na Azam FC wakati kutoka Zanzibar wamo mabingwa wa Kisiwani humo KMKM na KVZ.

Mapema Yanga inaelezwa iliomba kutojumuishwa kwenye mashindano hayo kwa kile ilichoeleza kubanwa na ratiba.