Pingamizi la Mwakinyo latupiliwa mbali

Muktasari:

  • Pingamizi hilo lililosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Amiri Msumi lilitupiliwa mbali baada ya kuona mahakama hiyo haikuona haja ya kuendelea kulishikilia kutokana na kukosa mashiko kwa mujibu wa sheria.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana Alhamisi imefanya uamuzi mdogo wa kutupilia mbali pingamizi lililoweka na bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo katika kesi ya madai inayomkabili dhidi ya Kampuni ya Promosheni ya Ngumi za Kulipwa, Paf Promotion.

Pingamizi hilo lililosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Amiri Msumi lilitupiliwa mbali baada ya kuona mahakama hiyo haikuona haja ya kuendelea kulishikilia kutokana na kukosa mashiko kwa mujibu wa sheria.

Hakimu Msumi aliiambia mahakama hiyo baada ya mahakama kupitia nyaraka zilikuwepo mahakamani na kuona kilichokuwa kinapingwa mdaiwa (Mwakinyo) ni tarehe ya uthibitisho wa madai ya Paf ambayo mahakama iliona imejazwa kwa usahihi kuwa ni 11.10.2023.

Hivyo mahakama hiyo imesema kuwa pingamizi halina mashiko kwa kuwa nyaraka inayoaminiwa ya kwanza ni iliopo mahakamani na imejazwa vizuri kwa mujibu wa sheria, hivyo mahakama imeona haina haja ya kushikilia pingamizi hilo na kulitupilia mbali.

Baada ya kulitupia mbali, mahakama imetoa amri kwa  kwa kesi iendelee kwa kwa kongamano la awali (first pre trial conference' ambayo imepangwa kusikilizwa Aprili 23, mwaka huu saa sita mchana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Amri Msumi.

Katika  kesi hiyo, Paf Promotion inawakilishwa na wakili msomi, Herry Kauki wakati Hassan Mwakinyo kwa upande wa mdaiwa akiwakilishwa wakili msomi, Azad Athumani.

Ikumbukwe, Novemba mwaka jana, Paf Promotion ilimfungulia  kesi ya madai  bondia huyo katika mahakama hiyo ikiwa madai nane ya msingi likiwemo la Paf kuomba mahakama  itamke kwamba bondia huyo amevunja mkataba wa kupigana wakati madai yake ya pili kampuni hiyo imeiomba maomba mahakama hiyo kumtaka Mwakinyo aombe radhi kwa kuichafua kutokana na kutoa taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari alivyotumia kuichafua kampuni na wakurugenzi wake.

Madai ya tatu ambayo yamewasilishwa kwenye kesi hiyo ni pamoja kuomba mahakama, walipwe fidia ya shilingi 142,500,000 kutokana na hasara kukosa mapato waliotegemea kutoka kwa wadhamini lakini madai ya nne, waiomba mahakama kwa kumtaka bondia huyo arudishe dola 3000 kama pesa alizopokea huku madai yao ya sita kuomba malipo ya shilingi milioni nane ikiwa ni gharama za kulipia ukumbi.

Katika madai namba sita, kampuni hiyo imeiomba kuridishiwa jumla ya 1,287,500 ikiwa ni gharama za malazi ya mpinzani wa bondia huyo huku kiomba katika madai namba saba  imeiomba pia kurudushiwa na bondia huyo malipo ya shilingi milioni 3,832,000 ambayo ni gharama za tiketi za ndege za mpinzani wake pamoja na wasaidizi wake.

Mbali ya madai hayo, PAF kupitia wakili wake, imeomba mahakama kulipwa jumla ya shilingi 150 milioni  ikiwa madhara ya jumla waliopata baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni tofauti na mkataba wake.