Pingamizi Mwakinyo latupiliwa mbali

Muktasari:

  • Pingamizi hilo lililosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Amiri Msumi lilitupiliwa  mbali baada ya kuona mahakama hiyo haikuona haja ya kuendelea kulishikilia kutokana na kukosa mashiko kwa mujibu wa sheria.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana Alhamisi imefanya uamuzi mdogo wa kutupilia mbali pingamizi lililoweka na bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo katika kesi ya madai inayomkabili dhidi ya Kampuni ya Promosheni ya Ngumi za Kulipwa, Paf Promotion.

Pingamizi hilo lililosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Amiri Msumi lilitupiliwa  mbali baada ya kuona mahakama hiyo haikuona haja ya kuendelea kulishikilia kutokana na kukosa mashiko kwa mujibu wa sheria.

Hakimu Msumi aliiambia Mahakama hiyo baada ya mahakama kupitia nyaraka zilikuwepo mahakamani na kuona kilichokuwa kinapingwa mdaiwa (Mwakinyo) ni tarehe ya uthibitisho wa madai ya Paf ambayo mahakama iliona imejazwa kwa usahihi kuwa ni 11.10.2023.

Hivyo Mahakama hiyo imesema kuwa pingamizi halina mashiko kwa kuwa nyaraka inayoaminiwa ya kwanza ni iliopo mahakamani na imejazwa vizuri kwa mujibu wa sheria, hivyo Mahakama imeona haina haja ya kushikilia pingamizi hilo na kulitupilia mbali.

Baada ya kulitupia mbali, Mahakama imetoa amri kwa  kwa kesi iendelee kwa kwa kongamano la awali  ambayo imepangwa kusikilizwa Aprili 23.

Katika  kesi hiyo, Paf Promotion inawakilishwa na wakili  Herry Kauki wakati Hassan Mwakinyo kwa upande wa mdaiwa akiwakilishwa wakili msomi, Azad Athumani.  Paf Promotion ilimfungulia  kesi ya madai  bondia huyo ikiwa madai nane ya msingi na kutoa taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari, madai ya tatu ambayo yamewasilishwa kwenye kesi hiyo ni pamoja kuomba mahakama, walipwe fidia ya shilingi 142,500,000 kutokana na hasara kukosa mapato waliotegemea kutoka kwa wadhamini lakini madai ya nne, waiomba mahakama kwa kumtaka bondia huyo arudishe dola 3000 kama pesa alizopokea huku madai yao ya sita kuomba malipo ya Sh. Milioni 8.