Taifa Stars ya 3 kuwasili AFCON

Baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Misri jana kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki, timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajiwa kuwasili Ivory Coast muda huu tayari kwa ushiriki wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Januari 13 hadi Februari 11.

Kwa kuwasili muda huo, Taifa Stars inakuwa timu ya tatu kati ya 23 tofauti na wenyeji Ivory Coast kuwasili katika nchi hiyo baada ya Morocco na Guinea Bissau zilizotangulia jana.

Baada ya msafara wa Stars kutua jijini Abdijan ambako utapokelewa na waziri wa usafirishaji wa Ivory Coast, Amadou Kone utaunganisha moja kwa moja kwenda San Pedro ambako timu hiyo itacheza mechi zake tatu za hatua ya makundi.

Baada ya Stars kuwasili kesho, idadi kubwa ya timu zitaanza kuwasili kuanzia kesho Jumanne ambapo Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abidjan unatarajiwa kuwa na pilika nyingi za mapokezi.

Mabingwa watetezi, Senegal watawasili kesho Jumanne wakiwa sambamba na Misri na Msumbiji.

Msafara huo wa Taifa Stars uliofua leo Ivory Coast unajumuisha wachezaji 27 waliosajiliwa kushiriki fainali hizo pamoja na wengine watatu ambao majina yao yalishindwa kuingia katika kikosi cha mwisho ambao kikosi cha mwisho ambao ni Abdul Sopu, Metacha Mnata na Khleffine Hamdoun.

Taifa Stars katika fainali za AFCON mwaka huu imepangwa katika kundi F na timu za Morocco, Zambia na DR Congo.

Itaanza fainali za mwaka huu kwa kuikabili Morocco, Januari 17 na Januari 21 itakabiliana na Zambia huku mechi yake ya mwisho ya Makundi ikiwa ni Januari 24 dhidi ya DR Congo.