Ibada ya kumuaga Waziri Mkuu mstaafu inafanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri KKKT usharika wa Azania Front jijini Dar es Salaam leo. Saa 4:52 gari lililobeba jeneza la Lowassa limewasili kanisani hapo tayari kuanza kwa ibada hiyo. Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Februari 14 anaingia katika siku yake ya pili kuagwa kati ya siku tano zilizopangwa kwa ajili hiyo. Picha na Sunday George na Loveness Bernard