Miaka mitatu ya Dkt Samia na maendeleo katika sekta ya bima

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.

Hadija Maulid, Meneja Uhusiano na Mawasiliano- TIRA

Ndugu msomaji wa ukurasa huu wa Kamishna wa Bima kari¬bu kwa mara nyingine ambapo leo tunaangazia maendeleo katika sekta ya bima kwa kipin¬di cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Has¬san ambaye ameongoza Tan¬zania kwa miaka mitatu iliyo¬pita, ambapo moja ya maeneo ambayo yameonesha ukuaji mkubwa ni sekta ya bima.

Tuungane na Dkt Baghayo Saqware, Kamishna wa Bima Tanzania akielezea zaidi

Kupitia sera zilizolenga kukuza uchumi na kuimari¬sha sekta za kifedha, Serikali, chini ya uongozi wake ime¬chukua hatua kadhaa ambazo zimewezesha kuongezeka kwa shughuli za bima nchini.

Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt Baghayo Saqware (kushoto) na Naibu wa Kamishna wa Bima, Bi Khadija Saidi (kulia) wakimkabi­dhi zawadi ya uhamasishaji kuhusu bima Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhandisi Zena Said ambaye pia ni Balozi wa Bima.

Rais Samia ameboresha mazingira ya biashara nchini, ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vinavyoweza kuzuia ukuaji wa sekta ya bima. Hatua hii imewavutia wawekezaji na kusaidia kuongeza ushindani katika soko la bima.

Katika kipindi hicho, Seri¬kali imefanya kazi na taasisi za kifedha kuboresha miundom¬binu inayohitajika kwa shu¬ghuli za bima. Hii ni pamoja na kusaidia kuanzisha mifumo ya kielektroniki ambayo inaruhu¬su utoaji wa huduma za bima kwa ufanisi zaidi.

Haya yote yamewezekana kutokana na juhudi kubwa za Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanza¬nia (TIRA) ambayo ni nguzo muhimu katika ukuaji wa sekta hii.

TIRA ambayo ilianzishwa kwa sheria ya Bima Sura Na. 394 inatekeleza majukumu ya; kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima, kuan¬daa na kutoa kanuni na mion¬gozo mbalimbali ya kusimamia soko la bima na kurekebisha sheria, kutoa elimu ya bima kwa umma, kulinda haki za mteja wa bima na kushauri Serikali kuhusu masuala yanayohusu bima.

Kamishna wa Bima, Dkt Baghayo Saqware anasema TIRA ni taasisi ya Muungano chini ya Wizara ya Fedha na inaongozwa na Kamishna wa Bima akisaidiwa na Naibu Kamishna wa Bima na inasi-mamiwa na Bodi ya Taifa ya Bima inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi.

Dk Saqware anasema ili kuongeza tija na ufanisi kati¬ka utekelezaji wa majukumu yake na kusogeza huduma kwa wananchi, TIRA hadi kufikia sasa ina ofisi zifuatazo; Makao Makuu Dodoma, ofisi ya Zan-zibar, Dar es Salaam, Kanda ya Magharibi (Tabora, Katavi na Kigoma)na Kanda ya Mashari¬ki (Dar es Salaam, Pwani na Morogoro);

Kamishna wa Bima Tanzania, Dk Baghayo Saqware.

Nyingine ni Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Njombe, Rukwa, Iringa na Songwe), Kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Geita), Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro na Tan¬ga), Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Manyara) na Kanda ya Kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma).

Mafanikio ya TIRA kwa kipin¬di cha Miaka Mitatu ya awamu ya sita chini ya Dk Samia

Dk Saqware anasema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan TIRA imepata mafanikio katika utekelezaji wa majuku yake makuu kama ifuatavyo;

Kuandaa na kutoa kanuni na miongozo ya kusimamia soko la bima na kurekebisha sheria

Soko la bima linaongozwa kwa sheria, kanuni, miongozo na taratibu mbalimbali. Kati ya mwaka 2022 na 2023, TIRA kwa kushirikiana na wadau wa bima wamefanikiwa kuandaa miongozo mbalimbali kwa ajili ya kusimamia na kuendeleza soko la bima. Miongozo hiyo ni pamoja na;

Miongozo ya usimam¬izi wa ubakizaji wa bima na bima mtawanyo, miongozo ya bima ya afya na usajili wa watoa huduma za afya, mion¬gozo ya utoaji wa ithibati kwa warekebishaji na watengene¬zaji wa vyombo vya moto kati¬ka sekta ya bima, miongozo ya uendeshaji huduma za takaful na miongozo ya utoaji huduma za bima kidijitali.

Mingine ni; miongozo ya maafisa wauza bima, miongozo ya utekelezaji wa viwango vya kimataifa vya taarifa ya kifedha kuhusu mikataba ya bima (IFRS 17), miongozo ya uwekezaji na usimamizi wa ukwasi, miongo¬zo ya kushughulikia madai ya bima, miongozo ya uendeshaji wa biasharaya benkiwakala na miongozo ya viwango elekezi vya fidia ya bima kwa madai ya majeraha ya mwili na vifo kwa mtu wa tatu kutokana na ajali za magari.

Kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima

Mamlaka imefanikiwa kusa¬jili watoa huduma za bima kama ifuatavyo;

Kampuni nne za bima mtawanyo, kampuni 36 za bima, wataalamu Nane wa ushauri wa bima mtawanyo na wataalamu nane wa ushauri wa bima mtawanyo waliopewa Ithibati, Kampuni Sita za Bima Mtawanyo zilizopewa Ithibati, wataalamu 116 wa ushauri wa bima, mawakala 1096 wa bima, benki wakala 30, wauza bima kidigitali 14, wakadiriaji hasara 56, kampuni Sita za takwimu za bima, wachunguzi binafsi Sita pamoja na maafisa wauza bima 100, waendesha bima za Taka¬ful Wawili, Washauri wa bima za Takaful Mmoja na Watoa huduma za Afya Wanane.

Utoaji wa elimu kwa umma

Mamlaka inaendelea na mkakati wake wa utoaji wa elimu kwa umma kwa kushirik¬isha wadau wote kwenye sekta. Lengo ni kufikia asilimia 80 ya Watanzania wote wenye umri wa miaka zaidi ya 18 ifikapo mwaka 2030.

Aidha, mamlaka inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa utoaji elimu na uhamasishaji kwa wizara na taasisi za umma kutekeleza sheria ya bima na sheria ya manunuzi, Na.7 ya mwaka 2011.

Hadi Julai 2023, Mamlaka imezitembelea Wizara za Kili¬mo, Nishati, Uchukuzi, Ujenzi na TAMISEMI. Mkakati huu ni endelevu na utazifikia wizara, idara na taasisi mbalimbali za umma.

Kulinda haki za mteja wa bima

Mamlaka imeendelea kuzi¬simamia kampuni za bima kuhakikisha zinalipa madai na fidia stahiki kwa wakati na kwa haki. Hadi sasa ulipaji wa madai na fidia umefikia asil¬imia 95 hivyo kupungua kwa malalamiko. Hata hivyo asil¬imia 5 ya madai na fidia yana changamoto ambazo TIRA ina¬fuatilia na kutoa suluhisho.

Kwa mfano, ulipaji wa madai ya bima za kawaida uliongeze¬ka kwa asilimia 10.1 kutoka Sh 301.9 bilioni mwaka 2021 hadi Sh 332.09 bilioni mwaka 2022.

Malipo ya madai na mafao ya bima za maisha yaliongezeka kwa asilimia 29.3 kutoka Sh 95.7 bilioni mwaka 2021 hadi Sh 123.71 bilioni mwaka 2022 .

Jumla ya kiasi cha madai kilicholipwa mwaka 2022 ni Sh 455.80 bilioni hivyo, kupungu¬za umaskini kwa wanufaika na kufanya biashara kuwa ende¬levu.

Aidha, TIRA inaendelea na uendeshaji wa mikutano ya kupokea maoni na kusikiliza malalamiko ya bima kwa wananchi ambapo hivi karibu¬ni imefanikiwa kuandaa miku¬tano mitano katika kanda zake zote.

Kuishauri Serikali kuhusu bima

Mamlaka imeendelea kuishauri Serikali katika mam¬bo mbalimbali ikiwa ni pamoja na eneo la ukatiaji wa bima za lazima, ukatiaji wa bima kwa mali za Serikali na Bima ya Afya kwa wote.

Hivi karibuni TIRA imefanya mkutano na Makatibu Wakuu pamoja na Naibu Katibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo ilifanya wasilisho kuhusu tathmini iliyofanywa na TIRA juu ya ukatiwaji bima wa mali za Seri¬kali na pia kutoa ushauri juu ya maswala mbalimbali ya bima.

Kuhusu ukuaji wa sekta ya bima Dk Saqware anasema sekta hiyo imekua kwa asilimia 26.7 ambapo mauzo ghafi ya bima yameongezeka kutoka Sh 911 bilioni mwaka 2021 hadi kufikia Sh 1,158 bilioni mwaka 2022.

Mchango wa sekta ya bima kwenye pato la Taifa unazidi kuongezeka kutoka asilimia 1.68 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 1.99 mwaka 2022.

Mamlaka imeendelea kuon¬geza gawio serikalini ambapo kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 Mamlaka imelipa gawio kwa Serikali la jumla ya Sh 2.9 bilioni. Aidha, sekta ya bima imechangia kwenye ajira kwa vijana ambapo hadi Sep¬temba 2022 imetoa ajira za kudumu kwa watanzania 4, 173.

Mafanikio mengine yaliyopati¬kana

Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Mamlaka imepata mafanikio kadhaa iki¬wa ni pamoja na:

Uanzishaji wa Konsotia ya Bima ya Kilimo

Ili kutekeleza skimu ya bima ya kilimo Tanzania kwa ufanisi, Julai 10, 2023, kulizinduliwa Konsotia ya Bima ya kilimo (Agriculture Insurance Con¬sortium).

Konsotia hiyo imeanzish¬wa ili kuweka ufanisi katika utekelezaji wa Skimu ya Taifa ya Bima ya Kilimo (TAIS) na kuongeza uwezo wa kimtaji wa soko la bima nchini kwa ajili ya kukinga majanga kwenye sekta ya kilimo.

Konsotia hiyo imeundwa na kampuni za bima zinazotoa bima ya kilimo zipatazo 15 ikiwa ni pamoja na kampuni tatu za bima mtawanyo zilizosajiliwa nchini na za kikanda ambazo ni; Tanzania Reinsurance Com¬pany (TAN-RE), Africa Reinsur¬ance Corporation (Africa Re), na PTA Reinsurance Company (ZEP-RE). Mtaji wa kukinga majanga wenye thamani ya Sh 300 bilioni umetengwa kwa aji¬li ya kukinga majanga kwenye sekta ya kilimo.

Pamoja na mambo mengine Konsotia hiyo itasaidia kuon¬gezeka kwa upatikanaji wa mtaji unaohitajika na kutumika katika ulipaji wa fidia na madai ya bima kwenye sekta ya kili¬mo, kuongeza kasi ya utekelez¬aji wa mipango na mikakati ya kitaifa ya kilimo, kurahisisha ulipaji wa madai ya mkulima mara janga linapotokea, kuon¬gezeka kwa imani kwa mku¬lima kuhusiana na umuhimu na matumizi ya bima, kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo na sekta ya bima, kuvutia uwekez¬aji kwenye sekta ya kilimo na sekta ya bima na kuongeza ajira kwa Watanzania.

Uanzishaji wa Konsotia ya Bima ya Mafuta na Gesi

Konsotia ya Bima ya Mafuta na Gesi ilizinduliwa Novemba 16, 2022 jijini Dar es Salaam

Mantiki ya kuanzisha kon¬sotia hii ni; kuhakikisha miradi yote ya gesi na mafuta inabakiza sio chini ya asilimia 45 ya ada zitokanazo na gesi na mafuta, kufuatia kutokuwa na uwezo wa soko la ndani, vihatarishi vya nishati, viliele¬kezwa nje ya nchi kwa asilimia 100 jambo lisilo na tija kwenye uchumi wa nchi.

Aidha, kuanzishwa kwa mira¬di mikubwa ya nishati kama vile bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ni fursa kwenye sekta ya bima kujipanga kwa ajili ya kuongeza tija, uchumi na ajira nchini.

Malengo ya kuanzisha kon¬sotia ni; kutoa fursa kwa kam¬puni za bima za ndani kushiriki na kuandikisha vihatarishi vya nishati ya Gesi na Mafuta nda¬ni ya nchi na kushiriki katika bima ya mradi wa LNG, una¬okadiriwa kuwa na gharama ya uwekezaji wa Dola za marekani bilioni 40 hivyo kuongezeka kwa ada za bima za kila mwaka na faida zitokanazo na kamish¬eni.

Mikakati ijayo ya TIRA hadi mwaka 2025/26

TIRA kwa kushirikiana na wadau wa bima inaendelea na utekelezaji wa mipango na mikakati ya Taifa pamoja na maelekezo ya viongozi wa juu wa kitaifa akiwemo Rais Dkt Samia na Rais Dkt Mwinyi wali-yoyatoa kwa nyakati tofauti.

Miongoni mwa mikakati ya TIRA kwa mwaka 2025/26 ni; kuanzisha na kutekeleza Mpango wa kitaifa wa Bima ya Kilimo, uanzishwaji wa bodi ya wataalamu wa Bima, Hifadhi ya Jamii na Takwimu Bima.

Kuunganisha mifumo ya kidigitali na taasisi mbalimbali za umma ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi, LATRA, NIDA, TASAC, TRA, PTA, ZRA. Len¬go ni kuongeza usimamizi na maendeleo ya soko la bima, kuendelea na utoaji wa elimu ya bima kwa umma na wadau mbalimbali.

Kufungua ofisi za Bima Mtawanyo za Kikanda ambazo Serikali inamiliki hisa za moja kwa moja au kupitia taasisi zake ili kampuni hizo ziweze kufungua ofisi nchini kwa uta¬ratibu wa mikataba ya uenyeji na kuendelea kukusanya mao¬ni ya wananchi kwa lengo la kuhuisha Sheria ya Bima Sura 394.

“Naomba kumpongeza na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uongozi bora na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ikiwa ni pamoja na kwenye sekta ya bima na Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi kwa melekezo yake na kwa ushirikiano wake,” anasema Dkt Saqware.

TIRA kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Bima itaende¬lea kuweka mazingira wezeshi kwenye sekta ya bima kwa ajili ya kuendeleza na kusimamia soko la Bima kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.