Singu: Ushirikiano, weledi, kuzingatia ubora ndiyo siri ya mafanikio ya Premier Agencies

Mkurugenzi Mkuu wa Premier Agencies, Robert Singu akizungumza wakati wa mkutano wa wasambazaji wa bidhaa za mafuta na gesi uliofanyika katika jiji la Rio de Janeiro, Brazil.


Kiongozi bora katika kam­puni ni nguzo muhimu ya mafanikio. Wanatoa mwon­gozo, msukumo na mwelekeo kwa wafanyakazi. Kupitia uongozi wao, kampuni hufan­ikiwa kufikia malengo yake na kuendeleza utamaduni wa kazi uliojengwa juu ya uamin­ifu, uwazi, na uvumilivu.

Kiongozi bora anajua kuweka malengo na kuvuta timu yake kuelekea kwenye maono ya kampuni. Anajen­ga mwelekeo wa pamoja na kuhamasisha wafanyakazi kufuata lengo hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Premier Agencies, Robert Singu akiwa ameshika tuzo ya kampuni bora 100 za kati wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo hizo mwaka 2019.

Pia, husisitiza mawasilia­no ya wazi kati ya wafanya­kazi. Wanajua umuhimu wa kusikiliza maoni ya wafanya­kazi na kushirikisha habari muhimu kwa njia inayoelewe­ka.

Sifa hizi haziji hivihivi bali ni kutokana na misingi bora iliyojengwa katika safari ya kiongozi huyo. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Premier Agencies, Robert Singu ni kielelezo sahihi cha sifa hizi.

Singu ambaye kitaaluma ni mhandisi mitambo (mechan­ical engineer) alianza safari yake mara baada ya kumaliza chuo kikuu ambapo aliajiriwa kiwandani akiwa mhandisi miradi wa moja ya kiwanda cha kuzalisha sabuni na dawa za meno kilichopo Dar es Salaam.

Anasema alifanya kazi kiwandani hapo kwa muda wa miaka minne kisha akaamua kuingia katika tasnia ya mafu­ta alipoajiriwa na moja ya kampuni kubwa za mafuta nchini na kufanikiwa kufan­ya kazi miaka mitatu kabla ya kuhamia katika kampuni nyingine ambapo ndipo ndoto ya kuanzisha kampuni yake ilipoanzia.

“Nilipoingia katika tasnia ya mafuta nilikuwa katika upande wa mitambo ambao jukumu langu kubwa lilikuwa ufungaji wa mitambo mbalim­bali pamoja na kuifanyia matengenezo. Jukumu hili lilinifanya kukutana na wazal­ishaji mbalimbali wa mitam­bo hiyo,” anasema Singu.

Anasema wakati anaende­lea kufanya kazi hiyo alikua anasoma kozi ya masoko ambyo anaeleza kuwu ili­kuwa na nguzo nne ambazo alifundishwa. Nguzo hizo ni; bidhaa (products), bei (price), matangazo (promotion) na eneo (place).

“Baada ya kufanya kazi katika kampuni ya mafuta kwa miaka kadhaa niliona fursa katika sekta ya usam­bazaji, ufungaji na ukaraba­ti wa mitambo katika tasnia ya mafuta na gesi,” anasema Singu.

Anasema kutokana na fursa hiyo, mwaka 2002 alianzisha kampuni ya Premier Agencies kwa lengo la kushughulikia changamoto iliyokuwa inaik­abili sekta ya mafuta husu­sani katika upatikanaji wa mitambo bora, huduma bora za ufungaji na matengenezo.

Anasema kampuni za mafu­ta zilikuwa zinaagiza vifaa, kufunga na kufanya maten­genezo zenyewe. Baadaye ziliamua kupeleka kazi hizo katika kampuni nyingine ili zenyewe ziendeleze biashara ya mafuta hapo ndipo alipoo­na fursa hiyo

“Premier Agencies ilianza rasmi mwaka 2002 kwa mad­humuni ya kutoa huduma katika sekta ya mafuta kwa kuuza na kusambaza mitam­bo, kufunga na kutoa huduma za matengenezo,” anasema Singu.

Anasema katika kozi yake ya masoko alibobea kati­ka masuala ya biashara za kimataifa hivyo akaingia makubaliano ya kibiashara na baadhi ya wasambazaji wa mitambo wa kimataifa ambao aliwafahamu wakati ameaji­riwa.

Anasema kutokana na makubaliano hayo, Premier Agencies ni wakala wa mauzo aliyeidhinishwa wa kampumi mbalimbali kubwa za kimatai­fa (zilipo Marekani na Ulaya) zinozotengeneza vifaa/mash­ine mbalimbali mfano Dover fuelling solutions, pampu za vituo vya mafuta, Technip FMC, mita za mafuta na gesi, GRACO BVBA watengezaji mitambo ya kusukuma vilain­ishi vya mitambo (lubrication equipment)

“Premier Agencies haiuzi bidhaa pekee bali pia inatoa huduma za ufungaji, maten­genezo na huduma kwa mteja baada ya mauzo hivyo kuifa­nya kuwa ya kipekee katika soko,” anasema Singu.

Anasema bidhaa zao zina ubora wa aina moja kwa saba­bu zinazalishwa na kampuni ambazo viwango vya bidhaa zake viko sawa bila kujali inauzwa wapi. Kitu kingine ni weledi ambao wanao katika kutoa huduma.

“Ubora wa bidhaa zetu ni wa hali ya juu kwa sababu zimethibitishwa na mamla­ka zote za ndani pamoja na mashirika ya kimataifa kwa sababu kampuni ambazo tunafanya nazo kazi ni za hadhi ya kimataifa na ndi­yo maana jina la kampuni ni Premier Agencies ikiwa na tafsiri ya kuwa wakala wa bidhaa ambazo ni “Premier,” anasema Singu.

Bidhaa ambayo wanauza ukienda Marekani ama Uin­gereza utazikuta tena kati­ka ubora uleule kwa sababu viwango vya ubora vya kam­puni wanazofanya nazo kazi viko sawa dunia nzima.

Kuhusu aina ya uongozi wake katika kampuni, Singu anasema yeye ni kiongozi ambaye anapenda kujifunza na kushirikisha wafanyakazi katika kila jambo.

Mkurugenzi Mkuu wa Premier Agencies, Robert Singu (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo za kampuni bora 100 za kati mwaka 2019.

“Naamini zaidi katika kujifunza na ushirikishwaji. Katika uzoefu wangu wangu wa zaidi ya miaka 20 bado kuna vitu sivifahamu hivyo naendelea kujifunza kupitia kwa wafanyakazi pamoja na wadau mbalimbali ninaofan­ya nao kazi,” anasema Mkuru­genzi huyo.

Singu anasema mabadiliko ya teknolojia pamoja na ugun­duzi wa gesi kunafanya vitu mbalimbali kubadilika katika soko hivyo lazima awe anajif­unza kila siku ili kwenda sam­bamba na mabadiliko hayo.

Kuendeleza rasilimali watu ni moja ya mambo muhimu katika maendeleo ya kampuni, Singu anasema wamekuwa na mkakati wa kuwaendele­za wafanyakazi wao kupitia kampuni za kimataifa wana­zofanya nazo kazi.

“Ukiwa wakala aliyeidhin­ishwa wa kampuni hizi kubwa unapata nafasi ya wafanyaka­zi wako kupewa mafunzo ya kujengewa uwezo wa nam­na ya kutambua vifaa halisi na visivyo halisi, ufungaji, matengenezo nk. Hivyo hili limetufanya kuwa moja ya kampuni inayotoa huduma za kipekee na kuaminiwa zaidi,” anasema Singu.

Anasema kampuni hiyo pia imeanzisha mkakati wa kupi­ta vyuoni na kuchukua wana­funzi kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ya vitendo ambapo panapotokea hitaji la wafa­nyakazi, huwatumia walewale waliowapa mafunzo.

Kuhusu mikakati Singu anasema kwa sasa wanaanda mazingira ya kuingia katika sekta ya gesi ili kuunga mkono juhudi za Serikali na mipango ya kitaifa ya matumizi ya gesi hususani kipindi hiki amba­cho nchi ina rasilimali gesi.

Anasema kuendelea kuboresha mifumo ya ndani hususani ile ya kidijitali ili kuhakikisha inaendelea kuwa bora jambo litakalorahisi­sha utekelezaji wa masuala mbalimbali. Kingine ni kuen­delea kuboresha utoaji wa huduma na bidhaa kwa wate­ja.