
| Daktari:Matibabu ya dharura kuzuia maambukizi ya Ukimwi ‘PEP’ | Send to a friend |
| Sunday, 29 January 2012 08:54 |
|
HABARI za virusi vya Ukimwi sio ngeni masikioni mwetu na kuna wengine siku hizi wakiona neno Ukimwi, huangalia pembeni kwa sababu akili zao huhoji kuna habari mpya kuhusu ugongwa huu? Ni kweli kabisa elimu kuhusu Ukimwi imeanza siku nyingi, lakini waelimishaji hawatakiwi kuacha kutoa elimu, eti kwa sababu watu wameelimishwa vya kutosha. Elimu haitakiwi kusimama hata siku moja kwani tabia za watu hazibadiliki siku moja, mwezi hata miaka. Leo nimewaletea habari kuhusu jinsi ya kuepuka maambukizi ya virusi vya Ukimwi iwapo kwa njia yoyote majimaji ya mtu mwenye virusi yameingingia sehemu zako zenye michubuko. Waathirika wa matukio ya bahati mbaya wanaweza kunusurika kwa kupewa dawa za dharura maarufu kama Post Exposure Prophilaxis (PEP). Maambukizo ya bahati mbaya ni kama vile ambayo yanaweza kuwakumba wafanyakazi wa hospitali. Kwa mfano muuguzi anapojichoma sindano iliyotumika kwa mtu mwenye maambukizi ya VVU au daktari katika upasuaji anaweza kujikata kidogo au damu ya mgonjwa ikamrukia sehemu zenye ngozi, laini kama machoni nk. Watu wengine ambao wanaweza kupata maambukizi ya bahati mbaya ni wale wanaojitolea kuokoa maisha ya watu waliopta ajali. Abiria hupata michubuko mikubwa na kutoka damu nyingi ambayo kwa bahati mbaya inaweza kufika kwenye kidonda au mchubuko wa mtu mwingine. Wengine ni watu waliobakwa na hasa kama ubakaji ulikuwa wa watu wengi na umesababisha michubuko. Hapa pia kuna hatari kubwa ya kupata maambukizi kwa sababu kati ya wabakaji wanaweza kuwepo wenye virusi vya Ukimwi Hapa sio mtu aliyebakwa anakuwa katika hatari kupata Ukimwi bali hata mbakaji mwenyewe. Hata kama ulikuwa na mtu wako ambaye huna uhakika na katika kutumia kinga ikapasuka na baada ya kupima mkijikuta mmoja wenu ana virusi, bado PEP itakusaidia kuzuia maambikizi. Edapo hatua za haraka hazitachukuliwa ni wazi kwamba mtu anaweza kujikuta akipata mambuizi ya Ukimwi. Kama una mwenzio mnayeaminiana mtaanza kulaumiana kuwa nani kaleta ugonjwa kumbe mliupata kwa bahati mbaya. Kwa watoto wanaozaliwa na mama ambaye naye alipata virusi kwa bahati mbaya, wapo kwenye hatari ya kupata Ukimwi iwapo hatua za kupima mapema na kupewa dawa zinazozuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hazifanyika. Sasa unatikiwa ufanye nini ? Unatakiwa ndani ya saa 72 au siku tatu uwe umeishatoa taarifa kwenye kituo chochote cha afya ili upimwe na kupewa dawa zitakazozuia kuendelea kwa maambukizo ya virusi vya Ukimwi katika mwili wako. Vituo vyote vinavyotoa huduma za kinga dhidi ya Ukimwi na vile vinavyotoa dawa za kupunguza makali, watakupa dawa bila shida. Cha msingi uwahi kabla muda uliowekwa haujapita. Ukienda siku ya kwanza, utakuwa kwenye usalama zaidi kuliko mtu anayeenda situ ya tatu. Hata hivyo iwapo kipimo kitaonyesha siku hiyo hiyo kuwa una virusi, ujue havina uhusiano na hiyo ajali na utapewa ushauri wa kuanza dawa za kupunguza makali ya Ukimwi iwapo utakuwa umefikia hatua hiyo. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














