MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Johari Urembo:Vaa pete za kisasa uongeze urembo wako
BOOKMARK THIS PAGE
Urembo:Vaa pete za kisasa uongeze urembo wako  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 20:25



Urembo ni mada pana ambayo yaweza kuchambuliwa katika nyanja mbalimbali.
 
Na ili mwanamke uwe wa kisasa, basi huna budi kufanya hili na lile ili kutia nakshi ule uzuri ambao Mungu amekupa. Lakini leo tutaangazia pete za  kisasa kwa wanawake. Miongoni mwa mambo yanayotia chumvi urembo wako, pete ni mojawapo.

Pete ni pambo linalopambwa katika vidole vya mwanamke. Ni moja ya vikolombwezo ambavyo vyaweza kuweka tofauti muonekano wako.

Kuna aina nyingi za pete na kila moja ina maana yake katika vidole. Zipo pete za uchumba, ndoa, za misiba na nyingine kwa ajili ya kujipamba katika vidole vyako kwa ajili ya urembo tu.

Katika imani za dini, pia kuna aina mbalimbali za pete kwa mfano katika dini za kikristo mara nyingi pete huvaliwa baada ya wanandoa kufunga pingu  za maisha, hivyo pete kwao ni muhimu kama kiwakilishi cha kiapo cha ndoa.

Pete hutengenezwa kwa namna tofauti, zipo dhahabu, shaba, kareti shanga, plastiki, almasi na zile ambazo zimetengenezwa kiasili kama aina ya magome.

Pete hizi huuzwa kwa bei tofauti kwa kutegemea na thamani yake kwani almasi inajulikana iko juu zaidi.

Katika safu yetu ya urembo leo, tutazungumiza pete za kisasa za rangi kwa ajili ya kumechisha na vazi lako. Katika pete hizi za urembo ni wajibu wa mwanamke mwenyewe kuchagua ni pete ya aina gani inamfaa kulingana na vazi lake.

Wengine hupendelea pete zao ziwe na viua, herufi za majina, aina ya mnyama, au aina fulani ya kito ambacho yeye mwenyewe anaona akiweka katika pete yake, atapendeza.

Pete za rangi zitakufanya uwe wa kisasa zaidi na wa kipekee. Lakini pia, utajisikia mwenye kujiamini uwapo mbele za watu kutokana na pete uliyoivaa.

Chagua pete ya rangi kulingana na rangi ya mwili wako. Watu weusi hupendeza rangi zilizotulia wakati weupe hupendeza zaidi rangi za kung’aa.

Makala hii imeandaliwa na Ellen Manyangu
This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner