
| Ufanye nini: Tumia matunda machachu kuondoa mafuta katika ngozi | Send to a friend |
| Saturday, 04 February 2012 20:27 |
|
KAMA kawaida tunaendelea na udunduzi wetu wa masuala mbalimbali yanayohusu urembo na kuboresha muonekano hasa wa ngozi yako. Mlundikano wa mafuta yaliyoganda katika ngozi, mara nyingi husababisha matatizo mbalimbali. Miongoni mwake ni pamoja na kuzalishwa kwa chunusi hususani katika ngozi ya uso, kunakochangia kwa kiasi kikubwa kuharibu muonekano wa ngozi. Kwa kuelewa hilo, wataalamu wa masuala ya urembo wa asili walikuja na nia rahisi za kupambana na tatizo hilo. Matumizi ya matunda yenye uchachu ni miongoni mwa njia hizo. Matunda machachu au ‘citrus fruit’ kama Waingereza wanavyoyaita, ni yale yenye aside, kiafya ni mazuri kutokana na kuwa na vitamin ‘C’ kwa wingi. Matunda haya yanauwezo wa kuonyesha maajabu hasa katika ngozi iliyo na mafuta kwa kukausha mafuta hayo na kukuacha ukiwa na ngozi yenye kuvutia. Mahitaji Tunda chachu 1. Maji ya kuoga ya uvuguvugu lita 10 hadi 20 Namna ya kufanya Njia ya kwanza. Kamulia matone machache katika maji yako ya kuoga na asidi katika matunda hayo husaidia kuua bakteria katika ngozi yako, pia hukausha mafuta yaliyozidi katika ngozi yako. Pamoja na hayo, matunda haya husaidia kuondoa madoa meusi katika ngozi yako na kung’arisha ngozi. Njia ya pili Sugua eneo lililo athirika kama vile usoni kwa kutumia kipande cha chungwa au limao au tunda lolote lenye uchachu . Kaa na juisi hiyo kwa muda wa dakika tano hadi kumi, kisha osha sehemu husika na paka losheni unayotumia. Kwa matokeo mazuri, unashauriwa kufanya zoezi hili mara kwa mara. Na ikiwa utazingatia maelezo hayo niliyokupa hapo juu, utafanikiwa kuwa na ngozi iliyobora na isiyo na mafuta ya kukera. Onyo Unashauriwa kutotumia matunda haya endapo unaumwa mafua kwa sababu yanaweza kukusababishia matatizo zaidi. Vilevile kwa watu ambao wana matatizo na matunda haya, labda kutokana na ongezeko la asidi walilonalo, wanashauriwa kutoyatumia kabisa na si kwa kupaka tu bali hata kwa kula. Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya Email: This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it .u |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














