
| Daktari:Tabia za watu kulingana na tarehe za kuzaliwa | Send to a friend |
| Saturday, 04 February 2012 20:31 |
|
Na Abied Sakara FEBRUARI 4 21 JANUARI – 18 FEBRUARI WATU waliozaliwa katika kipindi hiki huwa na juhudi sana. Wana upendo sana kwa watu na huweza kutoa kila kitu walichonacho ili kuwasaidia watu wengine kutatua matatizo yao. Wakiamua huweza kumpigania rafiki hadi dakika ya mwisho, lakini wakiudhiwa huwa na tabia kinyume kabisa na hii. Wana uwezo mkubwa wa kutafakari masuala mbalimbali na ni hodari katika majadiliano na malumbano na huwa ni wepesi kuguswa hisia zao. Jambo dogo tu huweza kuwafanya wakaona uchungu au kuwaathiri kimawazo. Ni wepesi kusoma nyoyo za watu wengine na kutambua tabia zao. Wana kipaji katika biashara na shughuli zinazohusiana na fedha. Hata hivyo, huweza kutumia akili zao kwa makini na kusaidia watu wengine au jamii kupata fedha badala ya wao wenyewe. Huwa wanapendelea zaidi kuwa katika jamii kama vile mikusanyiko ya watu kwa ajili ya mikutano, sherehe na tafrija. Hufurahia sana shughuli za burudani, maigizo na tamthilia. Tatizo kubwa la watu hawa ni kuwa wakati mwingine huweza kuchanganywa na changamoto za maisha wakakata tamaa na kupoteza mwelekeo. Lakini akitokea mtu akamtanabahisha, huwa mwepesi kujitambua na kuendelea vyema tena na maisha yake. Vilevile pamoja na maelezo yote haya, iwapo watu wanaozaliwa katika kipindi hiki watakuwa katika hali ya maisha ya chini katika jamii, hupoteza kabisa haiba na hadhi yao. AFYA Watu waliozaliwa katika kipindi hiki kwa kawaida husumbuliwa na maradhi ya viungo vya ndani ya mwili. Huweza kupata matatizo ya mmeng’enyuo wa chakula mwilini na maradhi ya neva yanayotokea kwa nadra sana na ambayo hayatibiki kwa urahisi kwa kutumia dawa za kawaida. Pia husumbuliwa na maumivu katika mikono, miguu, magoti na sehemu za katikati ya uti wa mgongo. Vilevile husumbuliwa na matatizo ya mtiririko wa damu na maradhi ya homa ya manjano. MARAFIKI Watu waliozaliwa katika kipindi hiki hupata marafiki bora zaidi miongoni mwa watu waliozaliwa kati ya 21 Machi – 20 Mei na 21 Septemba – 20 Novemba. VITO Watu waliozaliwa katika kipindi hiki huwa na bahati wakivaa vito vilivyopambwa kwa ametisti (kito cha thamani chenye rangi ya zambarau), yakuti ya rangi ya waridi na munistoni (kito cha rangi ya bluu yenye kijani kibichi). RANGI Rangi za bahati kwa watu waliozaliwa katika kipindi hiki ni samawati na kijivu. Tutakuwa tukikuletea mfululizo wa elimu hii ya kisaikolojia kila mwezi, ili upate fununu na ukweli kuhusu uhusiano kati ya majina, tarehe za kuzaliwa, aina ya rangi za bahati, pete na vito, marafiki wanaolandana kitabia, pamoja na wapenzi. Sayansi hii ipo na si kuwa watu hubahatisha, bali elimu maridhawa inayokuwezesha kuishi na kuyamudu vyema mazingira yako. Itaendelea |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














