MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Hoja Binafsi Muundo Wizara ya Afya unakwenda na wakati?
BOOKMARK THIS PAGE
Muundo Wizara ya Afya unakwenda na wakati?  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 20:13


KWA UJUMLA pamoja na bajeti kubwa na misaada mbalimbali ambayo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii hupata, bado sekta hii siku zote imekuwa katika tatizo hili au lile.

Tatizo hili la madaktari kugoma ni tatizo lililokuwa njiani na kila mtu akawa analiona, lakini wengi wakaamua kuficha kichwa chao mchangani kama vile mbuni afanyavyo anavyoona hatari mbele yake.

Hili ni kosa kwa sababu unatoa nafasi kwa nadhara makubwa zaidi
kutokea. Isitoshe hili ni moja tu kati ya matatizo ambayo wizara hiyo
inakabiliana nayo. Yapo mengine mengi, makubwa kwa madogo ambayo kama petroli yanahitaji mtu kupita tu na kijinga cha moto na moto ukalipuka.

Hivyo, kutafuta mchawi wa matatizo ya sekta ya afya
kunakoishia kumtaja mtu mmoja au wawili sio kitu cha busara wala
hekima na hakimsaidiii yeyote ndani au nje ya wizara husika.

Aidha, wabunge kupuuza na kuona suala hili sio muhimu kumezidi kuwatia hasira wananchi kiasi cha kujiuliza hivi huko bungeni anayewakilishwa ni serikali au ni mpiga kura jimboni. Jibu pengine wanalo wakubwa wenyewe na staili na stahili zao katika biashara za nyakati zetu ambazo ni wengi wasioziona!

Binafsi ninaamini kuna matatizo yafuatayo katika wizara husika:
Utawala, uaminifu na uwezo wa mameneja wa mahospitali;
madaktari kufunguka macho zaidi juu ya haki zao zisizotekelezwa;
manesi na wafanyakazi wasaidizi katika mahospitali mbalimbali kugeuzwa wafanyakazi maskini na ombaomba; wagonjwa kukosa mahitaji, ulinzi na maangalizi ya msingi.


Aidha ni makosa kwa upande wangu kwa wizara hiyo kubebeshwa idara kama ile ya Ustawi wa jamii na makundi yake ambayo kwa maono yangu ni mzigo ambao nao unahitaji ubebaji wa aina yake ili kutendea haki sawa pande
zote mbili, yaani Idara ya Afya na ile Idara ya Ustawi wa Jamii.

Vilevile, huu ni wakati wa kuangalia upya kama woga wetu wa kuiachia
mikoa na wilaya kuwa huru zaidi katika mipango, mikakati,
oganaizesheni na utekelezaji wa majukumu ya sekta ya afya nchini ni
kitu kinachosaidia kupungua au kuongeza matatizo katika sekta hiyo.

Matatizo mengine ninayoyaona kwa upande wangu ni lile la ujira,
maslahi na posho za watumishi wa ngazi za kati na chini katika wizara
hiyo; kukosa utawala na menejimenti bora ya rasilimali watu katika
sekta muhimu kama hii;  muundo wa wizara uliopitwa na wakati;
kukosa aina yoyote ya ushindani kati ya wafanyakazi na kati ya
mahospitali nchini; kukosa mifuko maalum kwa mahospitali na watumishi inayoweza kuchangia kuleta ahueni kwa njia moja au nyingine; udhibiti dhaifu wa rasilimali na hususan fedha wizarani na kukosekana na ubunifu na uvumbuzi katika sekta nzima ya afya nchini.


Ninaamini sina akili wala uwezo wa kutoa majawabu kwa changamoto
zinazokabili wizara hii, kwani kitakwimu na kitaalamu sijajaliwa uwezo
wa kufundwa na kuelewa kila jambo lipasalo. Nitajaribu tu kutoa mawazo ya kijuu juu ambayo kwayo waelewa zaidi wanaweza kujenga juu yake na hatimaye ufumbuzi wa matatizo ya kudumu au ya muda mrefu kwa wizara na changamoto zake yakapatikana.

Sekta hii ni nyeti. Inahitaji mameneja na watawala ambao wanaoana na kuiva vizuri na watumishi wa ngazi za juu na chini. Ukiwaweka watu
wanaojiona ni wakubwa, bora na muhimu zaidi kuliko wengine basi
misingi yote ya kuwa na wizara yenye mafanikio unakuwa umebomolewa fumba na kufumbua. Siingilii kwa undani zaidi juu ya hili, lakini kwa wote wanaoelewa ukweli huu tutakuwa kwa uhakika katika ‘frikwensi’ moja hapa.

Ikiwezekana majopo ya wataalamu husika yatastahili kuwashauri wakubwa wa nchi nani anafaa kwa nafasi ya uwaziri, unaibu waziri na nafasi za juu katika wizara na mahospitali kwa namna wazi na bora zaidi kuliko iliyopo hivi sasa. Kubwa la kuzingatiwa ni kuwa na watu wenye uwezo wa juu kiutendaji katika masuala ya utawala, uaminifu na uwezo wa kiumeneja katika  mahospitali  na sekta ya afya na tiba kwa ujumla.

Madaktari kutokana na yale yanayotokea kwingineko hivi duniani wameona mengi ambayo yamewasaidia kufunguka macho juu ya mambo mengi. Ni vizuri viongozi wa wizara wakajua kuwa wanayoyajua kuhusu sekta hiyo na mahospitali katika nchi zenye maisha bora ingawa maskini na madaktari wetu nao wamefunguka macho zaidi juu ya haki zao zisizotekelezwa.

Aidha, manesi na wafanyakazi wasaidizi katika mahospitali mbalimbali
wamechoka kugeuzwa wafanyakazi maskini na ombaomba katika nchi yao na kukosa uwezo wa kuwalisha na kuwasomesha vizuri watoto wao ila kwa kungojea bakshishi kutoka kwa wakubwa ambao ndio chanzo cha wadhifa wao kimshahara, kimaslahi na kihali ya maisha.

Katika nchi ambayo kuna tatizo kubwa la ajira na vifaa vinavyotakiwa
na mahospitali vinaweza kutengenezwa na magenge ya seremala au
mawelda (wachomaji na waundaji vitu vya bati na chuma) toka Mwenge, Keko, Kawe na kwingineko nchini na wagonjwa kukosa mahitaji, samani, vifaa, ulinzi na maangalizi ya msingi, basi wanaosimamia wizara husika ni kama vile wapo wapo tu, na ni ile aina ya uongozi ambayo huachia matatizo kuendelea kuwa matatizo katika sehemu husika, hata ukiwaachia miaka hamsini kufanya kazi mahala hapo.

Aidha ni makosa kwa upande wangu kwa wizara hiyo kubebeshwa idara kama ile ya Ustawi wa jamii na makundi yake ambayo kwa maono yangu ni mzigo ambao nao unahitaji ubebaji wa aina yake ili kutendea haki sawa pande zote mbili, yaani Idara ya Afya na ile Idara ya Ustawi wa Jamii.

Kwa maneno mengine ni makosa kuwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kama wizara moja badala ya kuwa ni wizara mbili. Ndio maana hivi  leoutunzaji na usaidizi kwa  wazee, watoto watundu wanaoishinda jamii na familia zao, mayatima, walemavu, albino, wajane, ombaomba na watu kama hao ni mambo yanayofanyika kiubabaishaubabaishaji tu na kuruhusu

wajanja kujinufaisha kutokana na ombwe lililopo.

Vilevile, huu ni wakati wa kuangalia upya kama uoga wetu wa kuiachia
mikoa na wilaya kuwa huru zaidi katika mipanga, mikakati,
oganaizesheni na utekelezaji wa majukumu ya sekta ya afya nchini ni
kitu kinachosaidia kupungua au kuongeza matatizo katika sekta hiyo.

Muundo mpya, majukumu mapya

Ninavyoamini ni kuwa Wizara ya Afya ingeliachiwa tu kushughulikia
majukumu ya upatikanaji dawa, uendeshaji mahospitali na uratibu wa
shughuli za kinga, afya na tiba nchini na si zaidi ya hapo.

Shughuli na majukumu yote yanayosalia, kwa maoni yangu, yangestahili kupewa Taasisi huru ambazo utendaji wake sio utakuwa na ufanisi na ufanifu zaidi bali pia unaweza ukawa ungiza fedha zaidi kuliko ya zinavyotumia.

Pamoja na wizara kugawanywa katika sehemu zaidi ya mbili
ningelipendekeza pia kwamba hata wizara ya afya asilia yenyewe igawanywe katika: Taasisi ya Hospitali za Ngazi ya Rufaa nchini; Taasisi ya Hospitali za Ngazi ya Mkoa nchini; Taasisi ya Hospitali za Ngazi ya Wilaya nchini; Taasisi za Hospitali Binafsi na Zahananti; Taasisi za Hospitali za Kijamii na Hospitali za Kiimani nchini; Taasisi ya Utafiti kwa Tiba Mbadala na Tiba za Kisunna na Taasisi Maalum ya Kuoanisha na
Kuunganisha nguvu na uwezo wa taasisi za sekta za afya  kwa ufanisi na ufanifu zaidi nchini.

Dhamira kuu ya uanzishwaji wa taasisi kama hizo hapo juu zinatokana
na ule ukweli kwamba wizara na hospitali zetu kwa hali ilivyo
haziwwezi kujitosheleza katika mahitaji yao yote bila kuwa watundu,
wabunifu, wavumbuzi na wanaoweza kupanua wigo wa wagonjwa wanaotibiwa hadi nje ya mipaka yetu. Hiki ni kitu kinachowezakana, kinataka tu serikali iliyo angavu na inayotoa fursa kwa wenye mawazo mapya kuonekana, kufanyiwa kazi, kutunzwa na kuenziwa.

Matatizo mengine ninayoyaona kwa upande wangu ni lile la ujira,
maslahi na posho za watumishi wa ngazi za kati na chini katika wizara
hiyo. Katika nchi kama Norway hivi leo kuna watu wachache wanaotaka
uanasiasa au uwaziri kwa sababu kazi wanazozifanya zinawalipa vizuri
zaidi kuliko uwaziri au ubunge.

Kwa kugeuza miguu juu na kichwa chini sera hii muhimu ya kipato cha
mtu, leo tunaishiwa kuwa na watu wa ajabu wanaopewa nafasi za ubunge, baadhi yao wakifanya pati na kualika wasichana wenye sketi fupi tu kuliko wote kuhudhuria pati hizo !!! Hawa ndio wabunge wetu, na hii ni nchi yetu, na yote haya tumeyataka sisi wenyewe!

Wizara husika na mahospitali ni maeneo yanayohitaji idara nzito ya
rasilimali watu. Ukikosa utawala na menejimenti bora ya rasilimali
watu katika sekta muhimu kama hii; na kuwa na muundo wa wizara
uliopitwa na wakati.

(Unaweza kusoma mengineyo zaidi mtandaoni!)
Pepe: This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner