MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Habari Dk Kigwangallah: Nipo tayari kuhojiwa CCM
BOOKMARK THIS PAGE
Dk Kigwangallah: Nipo tayari kuhojiwa CCM  Send to a friend
Sunday, 05 February 2012 10:09

Fidelis Butahe  
SIKU chache baada ya Wabunge wa CCM kutaka Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangallah ahojiwe na Kamati ya maadili ya chama hicho kwa kuunga mkono mgomo wa madaktari, mbunge huyo ameibuka na kusema kuwa yupo tayari kwa lolote.  

Wabunge hao walitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma chini ya uenyekiti Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambapo walihoji, iweje mbunge huyo atetee posho za wabunge, lakini awe kinara wa kuhamasisha mgogoro wa madaktari.  

Lakini jana akizungumza na Mwananchi Jumapili, Dk Kigwangallah alihoji ujasiri walioupata wabunge hao wanaotaka yeye ahojiwe, huku akisisitiza kuwa kwa kitendo hicho ni wazi kuwa watakuwa wanamnyima uhuru wake wa kuzungumza na kutoa maoni.  Alisisitiza kuwa kauli alizozitoa katika mikutano mbalimbali na madaktari hao hazikuwa kauli za kupindua nchi bali kuwatetea.  “Niko tayari kukiri kila kitu nilichozungumza.

Niko tayari kuhojiwa na kamati ya maadili ya CCM na ninarudia tena Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni hafai, anaweza kuipoteza taswira ya CCM machoni mwa Watanzania,” alisema Dk Kigwangallah.  Alisema kuwa wabunge hao wanaotaka ahojiwe na vikao vya juu vya chama wanatakiwa kutambua kuwa hakuingia CCM ukubwani na kwamba alikuwa katika chama hicho tangu akiwa na umri mdogo.  

“Nimekipigania sana CCM, lakini leo hii wanaibuka watu na kunisema vibaya kuwa nawaunga mkono madaktari…, hawa madaktari ni Watanzania na wanachokidai ni kitu cha msingi kabisa wanapaswa kusikilizwa,” alisema Dk Kigwangallah.  Alisema kila Mtanzania ana uhuru wa kuzungumza na kutoa maoni yale na kwamba atakuwa amefanya kosa kama maoni hayo yatakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  “Mawazo yangu yachukuliwe kama changamoto na ule utamaduni wa kumkosoa mtu anayesema ukweli uondoke,” alisema Dk Kigwangallah.  

Aliongeza, “CCM haina mwenyewe…, hiki chama kimejengwa kwa misingi ya uhuru na haki ya kuheshimu mawazo ya watu wengine”.

 Alisema kuwa yeye kama daktari ana haki ya kukutana na madaktari wenzake na kwamba hilo sio kosa.  Alisema akiwa katika vikao na madaktari hao alitoa maoni yake kuhusu madai yao na jinsi serikali inavyoshindwa kuyashughulikia huku akisisitiza kuwa atakayemhukumu kwa maoni hayo hatamtendea haki, “Hatanitendea haki kwa kuwa nilichokizungumza ndio ukweli wenyewe”.  

Amshukia Blandina Nyoni  Alisema kuwa kauli yake kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni hawezi kuifuta hata kidogo kwa madai kuwa katibu huyo ana lengo la kuifanya CCM ipoteze mwelekeo.  

Dk Kigwangallah alienda mbali zaidi na kusema kuwa, “Hivi mtu ukiwa na kipele harafu ukajiangalia katika kioo na kukiona kipele hicho na badala ya kukitoa ukaamua kuvunja kioo, utakuwa umejenga au umebomoa”.  Alisema kuwa Nyoni ni tatizo ndani ya Wizara hiyo na anatakiwa kung’oka na kusisitiza kuwa yuko tayari kutoa ushahidi za kutofaa kwa katibu huyo.         

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner