
| Kinana akemea wanaofanya kampeni za urais | Send to a friend |
| Sunday, 05 February 2012 10:14 |
|
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulahaman Kinana jana amesema makada wa chama hicho walioanza harakati za Urais 2015 wote hawana sifa za kushika nafasi. Mjumbe huyo ambaye ni Mlezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam alisema hayo jana katika Ukumbi wa Kitonga Inn Upanga jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam. Kinana alisema chama kina changamoto kubwa kuhakikisha kinaimarika kutokana na kuporomoka kwa maadili. Alisema hatua ya baadhi ya makada kuonyesha nia hata kuanza kampeni za chini chinikuwania urais wa mwaka 2015 hata muda wa kuanza haujafika ni kuporomoka maadili miongoni mwa wanachama. Alisema baada ya kusikiliza vilio vya wanafunzi wa vyo vikuu ametambua kwamba chama kimejikwaa hasa katika mbio za urais na kuhawahakikishia wanafunzi hao kuwa hakuna wenye sifa za kuwa rais katika hao wanaosikika kuanza kampeni. “Naomba kuwaeleza nimesikia kilio chenu, na nitakwenda kuwakilisha kwenye kamati kuu kwa hasira kama mlivyoeleza, lakini nataka kuwaambia kwamba hakuna wenye sifa ya kuwa rais kwa sasa kwa sababu mchakato wa kupata rais bado hajajulikana,” alisema Kinana huku akishangiliwa na wanafunzi waliofurika Ukumbi huo. Kinana alisema kuna viongozi wengi ndani ya CCM wanatamani urais bila ya kuacha serikali itekeleze ilani ya chama kitendo kinachosababisha kuongeza makundi. “ Nataka kuwahakikishia kama mlivyosema wote wanaotafuata urais mwaka 2015 hawafai na hawana sifa maana wameshindwa kuhakikisha wanamsaidia Rais Jakaya Kikwete kukamilisha ahadi wanaanza kukimbilia uras,” alisema. Kinana alisema kutokana na mambo kuwa mazito na kuhitaji majibu ya busara atahakikisha anarejesha majibu ya maswali yao kwa kuwandalia mkutano mwingine kama huo. Aliwatahadharisha makada wa chama hicho kukataa rushwa kutokana na watu kutaka kupanga viongozi wabovu kutokana na pesa zao bila ya kuangalia hatima ya chama kwanza. Awali wanafunzi hao walisema walitaka kujua hatua ambazo zimechukuliwa na CCM kumaliza migogoro ambayo imebuka miongoni mwa wanachama wake. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














