MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Habari Waziri ahamia Chadema
BOOKMARK THIS PAGE
Waziri ahamia Chadema  Send to a friend
Saturday, 07 August 2010 21:42

VIKAO VYAENDELEA KUWANASA SELELII, MSINDAI, SHIBUDA
Waandishi Wetu
WAKATI taarifa za mipango ya wana-CCM wanaolia kuwa wamechezewa rafu kwenye kura za maoni kuhamia upinzani zikizidi kushamiri, waziri wa zamani kwenye serikali za awali ya pili na tatu, Arcado Ntagazwa amehamia Chadema.
 
Habari za vigogo wa CCM kufanya mipango ya kujiondoa zilitiwa uzito zaidi na kauli ya mbunge wa zamani wa Maswa, John Shibuda ambaye alikiri kufanya mazungumzo na Chadema pamoja na CUF na UDP, lakini akasema atatangaza maamuzi magumu wiki ijayo.
 
Kujiunga kwa Ntagazwa kunaonekana kutazidi kuipa nguvu Chadema, ambayo imefanya kazi kubwa ya kujiimarisha katika kipindi cha miaka mitano huku kutangazwa kwa katibu wake mkuu, Dk Willibrod Slaa kugombea urais kukikifanya chama hicho kuwa tishio jipya kwenye mbio za kwenda Ikulu.
 
Ntagazwa, ambaye aliangushwa mwaka 2005 na mwaka huu kwenye kura za maoni, hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo, lakini naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe aliithibitishia Mwananchi Jumapili juu ya kupokolewa kwa mwanachama huyo mpya. 
 
Kabwe aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge huyo wa zamani wa Kibondo alichukua kadi ya Chadema jana asubuhi wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
 
Ntagazwa ameitumikia serikali ya awamu ya kwanza akiwa Naibu Waziri wa Fedha (1983-85) na baadaye akashika nafasi hiyo kwenye Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi (1986-87).
 
Chini ya uongozi wa Ali Hassan Mwinyi alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Maliasili na Utalii (1990-2000) na kuanzia mwaka 2000 alikuwa Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) hadi mwaka 2005 alipoanguka kwenye ubunge.
"Tunashukuru kwa kumpata Ntagazwa ambaye ana uzoefu mkubwa katika serikali. Tunaamini atatusaidia wakati Chadema inapounda serikali yake," alisema Zitto, mmoja wa wabunge wa Chadema waliokuwa moto bungeni.
Baada ya kushindwa ubunge mwaka 2005, taarifa zilienea kuwa Ntagazwa ameihama CCM na kujiunga na Chadema lakini baadaye mwanasiasa huyo alijitokeza na kukanusha habari hizo akisema kuwa alikuwa akiwasiliana na mwanasheria wake ili amshtaki mwandishi, gazeti na mchapishaji wake kwa kumdhalilisha.
Kwa upande wa Shibuda, ambaye alitangaza kwa muda mrefu kuwa angegombea urais kupambana na Jakaya Kikwete ndani ya CCM, uamuzi kamili kuhusu hatua inayofuata kwake utakuwa mapema wiki ijayo.
Shibuda, mwanasiasa machachari, alisema kati ya jumatano au Alhamisi anatarajia kutangaza maamuzi magumu kutokana na kile alichokiita ni baadhi ya viongozi ndani ya CCM kuamua kutumikia wanyonyaji na mafisadi.
Mwanasiasa huyo mwenyee kupenda kuzungumza kwa kutumia misemo mbalimbali ya Kiswahili, alisema: "Viongozi wa CCM wa leo ni sawa na jiwe la bahari, halifikiri kiu ya mtende."  
 
Alifafanua kwamba wanachofikiria viongozi hao kwa kiasi kikubwa ni nafsi zao na wanasahau umasikini na matatizo ya Watanzania walio wengi.
 
Shibuda aliongeza kwamba enzi za CCM ya Mwalimu Julius Nyerere, mtu mwenye kusimamia misingi aliitwa rafiki, lakini akaongeza: "Siku hizi mtu anayesimamia misingi ya chama huitwa adui na mtu hatari sana."  
Aliweka bayana  kwamba kamwe hafikiri kukata rufaa kupinga matokeo ya kura ya maoni baada ya kushindwa kwa sababu hajawahi kukata rufaa na akatendewa haki.
 
"Msimamo wangu uko wazi; sitakata rufaa CCM kupinga matokeo. Kwa sababu historia iko bayana. Katika siku zote nilizokata rufaa ndani ya chama sijawahi kusikilizwa wala kutendewa haki," alifafanua Shibuda.
"Niliwahi kukata rufa kupinga mambo mbalimbali kuanzia Nec hadi uongozi wa Jumuiya ya Wazazi, lakini sijawahi kusikilizwa. Nilikata rufaa uenyekiti Jumuiya ya Wazazi, lakini mzee wangu (rais wa awamu ya tatu, Benjamin) Mkapa alinishughulikia kwa sababu nilikuwa nahoji kwenye Nec." 
Alisema kutokana na mtiririko huo wa matukio ya kutomtendea haki ndani ya CCM, ameamua kufanya maamuzi magumu na sasa anaanza kuagana na kupata ushauri wa mwisho kwa watu anaowaheshimu ndani ya chama hicho.
Shibuda alisisitiza kwamba anajiandaa kuhama na kufanya maamuzi hayo huku akiweka bayana kuwa "wanamapinduzi wengi walipotaka kujipanga kufanya maamuzi magumu ya kutetea, haki walikimbia kwao kidogo."
 
"Samora Machel alikimbilia nchini Tanzania, hata akina Augustino Neto wa MPLA Angola, akina Sam Nujoma wa Namibia wote walifanya hivyo, kisha wakarudi kukomboa watu wao," alifafanua.
Alisema CCM kama chama kina misingi mizuri isipokuwa kimejaa watu ambao hawataki ukweli, hasa unapokosoa utendaji mbovu, ndipo huonekana ni msaliti, adui na mtu hatari kabisa.
 
"Tanzania bila malaria inawezekana lakini Tanzania bila mafisadi na wanyonyaji haiwezekani. Sasa hivi CCM ni chama cha walowezi, wale ambao tuliwaita wanyonyaji sawa na makaburu ndiyo wameshika chama," alisisitiza.
Alisema msimamo wake hadi sasa ni kutumikia Watanzania katika misingi ambayo nchi ilirithi kutoka TANU. 
"Ndiyo maana nataka nikwambie kaka, ukihama msikiti hujagombana na msahafu. Kwa hiyo kama nitahama sitagombana na Watanzania kwani lengo ni kuwatumikia wao," alisisitiza.
 
Habari zaidi zinasema kuwa vigogo wengine kadhaa wa CCM wako njiani kujiunga na Chadema baada ya kushindwa kwenye kura za maoni ambazo wanaamini zilijaa rushwa, rafu na ukiukwaji wa taratibu.
Habari zimeeleza kuwa mazungumzo hayo yanawashikirikisha wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo baadhi ya waliokuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi.
 
Taarifa za kiuchunguzi zimeeleza kuwa hadi sasa Chadema kimefanya mazungumzo na wabunge wengi wa CCM.
Alipoulizwa kuhusu Chadema kuwasiliana na wanasiasa hayo, Zitto Kabwe chama hicho kinawakaribisha wote wanaotaka kujiunga.
Zitto alifafanua kwamba kwa kuwa Chadema ni chama cha upinzani chenye malengo ya kushika dola, kinahitaji watu makini kutoka CCM lakini akasema"hakuna taarifa rasmi ya makubaliano hadi sasa".  
Zitto, ambaye atatetea ubunge kwenye jimbo lake la Kigoma Kaskazini, alisema suala la kufanya mazungumzo na wana-CCM hao si tatizo.
 
Hata hivyo, habari ambazo Mwananchi imezipata zinawataja baadhi ya wabunge wa zamani walioongea na Chadema kuwa ni pamoja na Lucas Selelii wa Nzega ambaye, hata hivyo, alisema bado hajakubali kujiunga na chama hicho wala kujiondoa CCM.
 
"Ni kweli nilifanya mazungumzo na Chadema lakini nimekataa kwa sababu ukigombana na shehe siyo kugombana na Uislam. Siwezi kuhama CCM kwa sababu tu ya watu wachache mafisadi," alifafanua.
"Tutabanana humu humu, hakuna kukimbia wala siwezi kuwaachia waendelee kutamba, kukimbia itakuwa ni kosa kwangu. Siwezi kuwaachia waendelee kutamba  wao wenyewe."  
 
Selelii alisema uamuzi wa kuihama CCM haujaufikiria kwa sasa kwani bado anaamini chama hicho ni chake na hivyo hawezi kuondoka kwa sababu ya kufanyiwa mchezo mchafu na baadhi ya watu waovu.
Alisema hata wakati wa mchakato wa kura za maoni yupo mmoja wa watuhumiwa wakubwa wa ufisadi nchini, ambaye alipiga kambi siku hiyo kuhakikisha anamng'oa.
"Unafikiri ilikuwa mchezo alikwepo .....(jina tunalo) siku ya kupiga kura alihakikisha ananing'oa. Si unajua akiwepo, pesa anazomwaga hakuna mtu anayeweza kupona."
 
Selelii alifafanua kwamba katika uchagugzi huo alinyanyasika na kuzomewa, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kumfanya afikirie kujitoa CCM labda baada ya kufanya tathimini ya kina.  
Kigogo mwingine wa CCM ambaye inasemekana alifanya mazungumzo na Chadema ni mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai, ambaye pia ameshindwa kwenye kura za maoni.
Msindai na Dk Slaa kwa muda wote wamekuwa pamoja kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na ameng'olewa kwenye kiti hicho baada ya kukaa bungeni kwa muda mrefu. 
Katika hatua nyingine baadhi ya wabunge na vigogo wa CCM walioshindwa kwenye kura za maoni wameuponda utaratibu mpya wa ulioanzishwa na chama hicho wa kuwapata viongozi wa dola kupitia kura za maoni za wanachama wote kwa madai kuwa unachangia rushwa.
Aliyekuwa mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro alisema utaratibu huo ni mbovu kwa kuwa unachochea rushwa kutokana na ukweli kuwa wanachama wengi wanakuwa hawana ufahamu wa kutosha na elimu ya uraia.
Hata hivyo, Kimaro aliapa kuwa hatasita kulipua mabomu ya ufisadi nchini hata akiwa nje ya bunge kwa kuwa yapo majukwaa mengi ya kufanyia mambo hayo na kwamba safari yake ya kisiasa haijafika mwisho.
"Si unajua ukifungulia milango wanaingia hadi inzi. Sasa hata huu utaratibu umeruhusu wengine wa ajabu kuingia ndani ya chama... ni sawa na unapofungua mlango kutaka hewa iingie, lakini badala yake hadi nge wataingia," alisema.
 
Mpambanaji huyo wa ufisadi alifafanua kwamba, kuna watu walimchezea mchezo mchafu wakifikiri ndiyo kummaliza, lakini akasisitiza kwamba yapo majukwaa mbalimbali ya kuweza kufikisha ujumbe huo.
"Tutaendelea kubanana tu, wala sitakaa kimya. Ila moyo wangu uko safi kabisa na naamini nitaendelea kutoa mchango wangu kwa taifa," alifafanua Kimaro. 
Alisema utaratibu huo wa kura za maoni kama utaachiwa kama ulivyo bila usimamizi makini, basi utakuwa hauna maana na hautafaa kutumiwa na chama.
 
Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi aliupongeza utaratibu huo, lakini alikiri kwamba rushwa kwa sasa inashuka chini kutoka ngazi ya juu.
Karamagi, ambaye alijiuzulu uwaziri kutokana na kashfa ya Richmond, aliweka bayana kwamba kukosekana elimu ya uraia na vyombo vya kusimamia utekelezaji wa utaratibu huo na sheria ya gharama za uchaguzi, ni hatari kwa ustawi wa jamii.
 
"Kwa ujumla, nadharia ni nzuri sana, lakini kutokana na ukosefu wa vyombo vya usimamizi, hiyo imechangia ku-expand (kutanua) mianya ya rushwa kutoka ngazi ya juu kuja chini," alifafanua Karamagi.
"Lakini kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya uraia, watu hawakuwa wakichagua bali walijua hiki ni kipindi cha mavuno tu kujiingizia fedha basi. Hii ni hatari sana kwa nchi."
Dk Zainabu Gama ambaye aligombea jimbo la Kibaha Mjini, naye alisifia utaratibu huo lakini akakosoa kwamba hakukuwa na maandalizi mazuri katika utekelezaji. 
 
Kwa mujibu wa Dk Gama, utaratibu huo unawezesha wanachama wengi kushiriki kupata viongozi wa dola lakini tatizo ni elimu ya uraia kitu ambacho kiliwafanya wengi wasijue nani ni nani.
Alisema ukosefu wa elimu ya uraia kwa wanachama, kulifanya baadhi yao wafikiri uchaguzi umekuwa ni fursa ya kupata fedha badala ya kuchagua viongozi bora.
 
Gama alisema kwamba athari ya tatizo hilo ni kuchochea rushwa kutoka ngazi ya taifa hadi chini kitu ambacho alikiita kwamba ni cha hatari kwa mustakabali wa baadaye wa taifa na chama. 
Hata hivyo, alisema hafikirii kuhama CCM na lakini akadokeza: "Chama hakikujiandaa vizuri, watu walikuwa na kadi mpya nyingi tu na waliwezaa kuzifanyia modification (marekebisho) ya tarehe tu."  
"Kukosekana kwa umakini katika usimamizi, kumechangia kuongeza loopholes (mianya) ya rushwa katika kupata viongozi wa dola. Lakini, nashukuru mimi kazi nzuri," alifafanua. 
 
Siraju Kaboyonga, ambaye alikuwa mbunge wa Tabora Mjini, alisema tatizo kubwa ni ukosefu wa vyombo vya usimamizi kuanzia ndani ya chama, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hadi Takukuru.
Kaboyonga alisema hadi sasa Takukuru haijaweza kujitanua katika maeneo yote nchini ndiyo maana pamoja na juhudi zake, bado ilimezwa na watoa rushwa.
 
Mbunge huyo alisema hatua ya Takukuru kuzidiwa nguvu pia ilitokana na msimamizi wa sheria ya gharama za uchaguzi ambayo ni Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa dhaifu.
 
Alifafanua kwamba jukumu hilo lilipaswa kuwa chini ya ofisi ya vyama vya siasa wakati yenyewe haina ofisi katika maeneo mengi nchini, jambo ambalo liliifanya Takukuru kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja. 
Reinard Mrope wa jimbo la Masasi, alifafanua kwamba utaratibu huo ni mzuri lakini tatizo kubwa ni utekelezaji.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #39 2011-12-14 11:23
[quote name="KUNJAKUNJA KIBOKO"]YES KARIBU SANA MHESHIMIWA ARCADO NTAGAZWA TUIJENGE NCHI YETU TANZANIA UPYA, TUTA ANZA NA MIUNDO MBINU,HASA BARABARA ZA NDANI ILI KUWAFIKIA WANA NCHI WAKIPATO CHA CHINI NA MASIKINI WALIOSAHAULIKA KABISA SERIKALI YA AWAMU YA NNE,AFYA,MAJI,S HULE,NAKAZALIKA ,ILI KURUDISHA UHURU AMANI UMOJA NA DEMOCRASIA:,taz ama nijinsi gani serikali ya awamu ya nne ilivyo wadanganya wana nchi wanaoishi maeneo ya ukonga. hasa barabara inayotoka mombasa kwenda kwa mkolemba-kwadiwani.hadi kivule,je,huu ni ubepari ukabaila au ni ukoloni?: karibu sana mhesmiwa arcado ntagazwa tuifufue nchi:,kidumu chama cha democrasia na maendeleo:,
Quote
 
 
0 #38 2011-12-14 11:07
Quoting KUNJAKUNJA KIBOKO:
YES KARIBU SANA MHESHIMIWA ARCADO NTAGAZWA TUIJENGE NCHI YETU TANZANIA UPYA, TUTA ANZA NA MIUNDO MBINU,HASA BARABARA ZA NDANI ILI KUWAFIKIA WANA NCHI WAKIPATO CHA CHINI NA MASIKINI WALIOSAHAULIKA KABISA SERIKALI YA AWAMU YA NNE,AFYA,MAJI,S HULE,NAKAZALIKA ,ILI KURUDISHA UHURU AMANI UMOJA NA DEMOCRASIA:,taz ama nijinsi gani serikali ya awamu ya nne ilivyo wadanganya wana nchi wanaoishi maeneo ya ukonga. hasa barabara inayotoka mombasa kwenda kwa mkolemba-kwadiwani.hadi kivule imekufa kabisa. wananchi wanalazimika kutembea kwa miguu kinachosikitish a zaid ni huduma ya afya.mtu anapoteza uhai kwasababu ya miundo mbinu mibovu haiptiki kabisa,je,huu ni ubepari ukabaila au ni ukoloni?: karibu sana mhesmiwa arcado ntagazwa tuifufue nchi:,kidumu cha democrasia na maendeleo:, :-kua na aibu kidogo mshkaji> :- x :-x
Quote
 
 
0 #37 2011-12-14 09:06
YES KARIBU SANA MHESHIMIWA ARCADO NTAGAZWA TUIJENGE NCHI YETU TANZANIA UPYA, TUTA ANZA NA MIUNDO MBINU,HASA BARABARA ZA NDANI ILI KUWAFIKIA WANA NCHI WAKIPATO CHA CHINI NA MASIKINI WALIOSAHAULIKA KABISA SERIKALI YA AWAMU YA NNE,AFYA,MAJI,S HULE,NAKAZALIKA ,ILI KURUDISHA UHURU AMANI UMOJA NA DEMOCRASIA:,taz ama nijinsi gani serikali ya awamu ya nne ilivyo wadanganya wana nchi wanaoishi maeneo ya ukonga. hasa barabara inayotoka mombasa kwenda kwa mkolemba-kwadiwani.hadi kivule,je,huu ni ubepari ukabaila au ni ukoloni?: karibu sana mhesmiwa arcado ntagazwa tuifufue nchi:,kidumu cha democrasia na maendeleo:,
Quote
 
 
0 #36 2011-11-20 21:10
acha wahamie chadema.wasipofata masharti wataondoka wenyewe.
Quote
 
 
-1 #35 2011-08-08 00:46
OMG...SHIBUDA MWINGINE HUYO...CCM WANATUMA WAPELELEZI CHADEMA!
Quote
 
 
0 #34 2011-04-26 00:07
nionavyosasa katika msafara wa mamba hata kenge wamo haya nyie chadema endeleeni kuwapokea watu ambao wameshindwa kwenye kura za maoni ambao kwa hasira zao wanajifanya wanahama chama ni yaleyale ya shibuda naona yanaendelea shibudfa hampatani nae naona mnaendelea kuwachukua na tena hamchelewi kuwapa uongozo nami nasema kwa hayo mfanyayo sijui ni lini mtapata hiyo dla msemayo.huo ni mtazamo wangu tu msilete chuki!!!
Quote
 
 
0 #33 2011-04-07 17:10
MIMI NAONA KWA HALI ILIVYO SASA WANANCHI HATUJIVUNII KUWA WATANZANIA, BALI TUNAVUMILIA KUWA WATANZANIA,

MFANO NI KWA YALE YANAYOTOKEA DODOMA LEO HII.
Quote
 
 
+1 #32 2011-02-28 18:04
Kidumu chama cha maendeleo na demokrasia! Chama tawala na watendaji wake wote wanaliangamiza taifa la Tanzania. Ni usanii usio nakifani kuona serikali inataka kuendeleza makazi karibu na kambi za jeshi huku ikiwa haina uwezo wa kukagua wala kudhibiti mabomu yanayoisha muda wa uhai na usalama wake. Je, tanzania imekosa eneo la kuhamishia kambi au makazi ya watu waishio karibu na kambi za majeshi? ni aibu ilioje? Waziri mwenye dhamana, ulikuwa huna haja ya kubabaisha kwenye mjadala na BBC kwani wewe hujapima vile viwanja. Ila pia inasikitisha unaposema kuwa haviko halali na wakati viwanja hivyohivyo (sijui tuseme visivyo rasmi)vinalipa kodi ndani ya serikali. je hio kodi inalipwa kwa kiwanja namba ngapi kama havitambuliki na serikali au mamlaka husika?Poleni ndugu tuliofiwa, poleni Watanzania na ole wenu WATAZAMIA mnaojiita viongozi watanzania. ipo siku Molla atawauliza roho za watu wanaoteketea.
Quote
 
 
0 #31 2011-02-01 19:06
TUNATAKA KULETA MAENDELEO. NANI ATATUSAIDIA? KILA TUNAYE MPENDEKEZA ATUSAIDIE ANATUGEUKA, JE HATA WEWE UNAYE DHANI UTATUSAIDIA, TUTA PATAJE KUWA NA HAKIKA. KUNAHAJA YA KUIANGALIA UPYA KATIBA YETU ILI IWEZE KULETA HATA MBINU DHIDI YA WAAMINIFU KABLA YA UCHAGUZI BALI MAFISADI MARA TU BAADA YA KUUKWAA UONGOZI. NDELE VA PA SWENGU- INIHO.
Quote
 
 
+1 #30 2010-11-01 14:15
niliona swala zima la mapinduzi muda mrefu!! kama miaka miwili baada ya kuona fisadi anaachwa hafanywi kitu!!!... nina furaha ingaawa sipo nchini lakini watu wameamka na kugundua UOZO wa serikali yetu unaoletwa na CCM!! it's time to make changes...and note keeping old unproductive policies!!!!
Quote
 
 
+3 #29 2010-08-16 16:05
Anayekuja Chadema na aje. Hatumkatai mtu yeyote, ilimradi ana nia ya kuleta mapinduzi ya kweli ya kuwaondoa mafisadi madarakani. Mimi naamini kwamba, bado Watanzania hatujapata uhuru wa kweli tangu wazungu watutawale.
Kama hali ya maisha inazidi kuwa mbaya kila kukicha, huo uhuru uko wapi?
Ni muda wa kubadilisha mfumo wa uongozi.
TUNAHITAJI KUFANYA FORMATTING KATIKA NCHI YETU, HADI YULE HOHEHAHE AWE NA UHAKIKA WA KUISHI.
Inawezekana kwa kusema NO! UISADI, NO MASHATI YA KIJANI.
Quote
 
 
+2 #28 2010-08-15 20:23
It does not matter where yuo come from or who yuo are what matters is the potentiality to lead. I think it is the time to embrace changes and move on. Prove Slaa wrong instead of makingexcusses oh because he failed in 'kura za maoni' that doesnot justify he isnt a gd candidate. Jenga hoja ya msingi wewe uliyesema 'Hata Dr. Slaa alihamia CHADEMA baada ya kushindwa CCM' so what?
Quote
 
 
+2 #27 2010-08-15 11:32
CV ya Dr Slaa

EDUCATION
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993

TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985

St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981

St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]

Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973

Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969

Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960

EMPLOYMENT HISTORY
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992-1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985-1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982-1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982-1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977-1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977-1991

POLITICAL EXPERIENCE

CHADEMA Principal Secretary 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 To date
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch (Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
Quote
 
 
+3 #26 2010-08-13 17:45
Mimi nafikiri kwa mtazamo wangu kuwa huo ni UHURU wa kikatiba ambao kila mtu anayo fursa ya kuchukua maamuzi ambayo kwa utashi wake anaona unafaa kwa muda husika pasipo kuvunja katiba ya Nchi. Kuhama kwa Ntagazwa na wengine wengi wanaotarajia kufanya hivyo ni kukomaa kisiasa na pia ni njia pekee ya kuufanya upinzani kukua, kwa wale wanaofuatilia Biblia, ilibidi Mungu aruhusu Stefano apigwe mawe hadi kufa ndipo KANISA la kwanza lilipo sambaa ulimwenguni mwote kutoka pale walipokuwa mwanzo wamejifungia Yesusalemu baada ya YESU kunyakuliwa. Huu ni wakati wa Mageuzi ya kweli, ni nyakati za watu wengi walionyanyaswa na kunyonywa kupewa nafasi na Mungu kufaidika na rasilimali ambazo Nyerere alizihifadhi kwa miaka mingi ya uongozi wake. Bado tunahitaji viongozi waadilifu kama akina Ntagazwa, Shibuda, Selelii, Nape na wengineo ambao watatupa experience pale CHADEMA itakapotwaa Nchi hii na kuwakilisha wanyonge. Tumechoshwa na Wanyonyaji, ambao wanabana kila sehemu, hata biashara za vinyozi wanafanya wao, Dry Cleaners, Shule, kila kitu, mlalahoi atavuna nini?? na hiyo mitaji wamepata wapi huku tunajua mishahara yao ni midogo? au ndio wanafwata mafungu ya mabilioni ya hela ambayo huwa yanatengwa kwenye halmashauri???
Quote
 
 
+1 #25 2010-08-13 17:27
Quoting Deus:
Quoting LENGAI:
Mtanzania mwenye akili na machungu ya nchi yake hawezi bakia ndani ya CCM. Chama kinaongozwa na wasanii na wakora tu.Unadanganya Wananchi eti uchumi umekuwa wakati dola moja inakimbilia 1,600/=.Hawa CCM wendawazimu tu.Utaendeshaje nchi bila viwanda.Utaendeshaje nchi kwa kutegemea wahisani.Fufueni "STAMICO" mchimbe madini wenyewe tuone kama nchi itakuwa na shida ya fedha.Reli mumeua mizigo yote mizito inapitia barabarani sijui hizi barabara zitadumu vipi?.Kibaya zaidi reli zinakatwa na vyuma kuuzwa madukani Serekali inaangalia tu.Huu ni usanii hakuna uongozi.



Uchumu haungaliwi kwenye exchange rate tu ndugu yangu. jielimishe kabla ya kutoa maoni yako.


Mbona wewe hujajielimisha na ukaandika uchumu badala ya uchumi?, usiangalie exchange rate! hiyo 1,600/= aliyoandika hapo juu anaangalia suala zima la inflation na kuporomoka kwa thamani ya fedha yetu, ambayo inachangiwa na kuendekeza kununua bidhaa toka nje, supermarkets na kuacha kununua bidhaa zetu. Kama nyanya mnanunua Mlimani City na zimetoka South Africa mnategemea uchumi utakua?
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner