
| Wahadzabe wapewa elimu ya kupiga kura | Send to a friend |
| Saturday, 28 August 2010 19:50 |
|
SERIKALI wilayani Mbulu mkoani Manyara, imeanza kutoa elimu ya ya uraia kwa jamii ya Wahadzabe wanaoishi katika bonde la Yaeda ili wajitokeze kwa wingi kwenye kampeni na kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao. Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Anatory Choya akizungumza na mwananchi mjini hapa, alisema jamii ya wahadzabe, moja ya jamii zinazoishi maisha ya asili hapa nchini, imewekewa utaratibu mzuri wa kushiriki kwenye uchaguzi. "Tayari elimu imeanza kutolewa na kuna baadhi yao walishiriki hata katika kura za maoni, hivyo tumejipanga kuhakikisha wanashiriki katika uchaguzi kama walivyo raia wengine," alisema Choya. Alisema sambamba na kushiriki katika uchaguzi huo, pia elimu bado inatolewa ili jamii hiyo iweze kukabiliana na changamoto mbali mbali za kiuchumi ikiwepo kupata elimu, chakula na makazi bora. "Tatizo lililopo ni kwamba kuna baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo hayataki jamii hii ibadilike kwani yananufaika kutokana na hali ya jamii hii"alisema Choya. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Links za wateja na washirika wetu
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani












