
| Tambaza ya Sekondari kukarabatiwa | Send to a friend |
| Sunday, 29 January 2012 10:22 |
|
SERIKALI imetoa Sh100 milioni k ukarabati Sekondari ya Tambaza kutokana na majengo mengi ya shule hiyo kuchakaa.Ukarabati huo ambao tayari umeanza utahusisha vyoo vya wanafunzi, maabara ya fizikia na kemia, madarasa 28 na mfumo wa umeme. Akizungumza Dar es Salaam jana, kwenye mahafali ya kidato cha sita, Mkuu wa shule hiyo, Hussein Zubeir, alisema shule hiyo ni kati ya shule kongwe nchini iliyofunguliwa mwaka 1957 na sasa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo uchakavu wa majengo. Zubeir alitaja changamoto nyingine zinazowakabili kuwa, ni upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ukosefu wa uzio wa uhakika na usafiri kwa wanafunzi.Nyingine ni upungufu wa walimu kwa baadhi ya masomo, uchakavu wa jengo la utawala na nyumba za walimu na viwanja vya michezo. “Tunaomba tupatiwe walimu hasa wa masomo ya sayansi na hisabati, ili kuukabili uhaba wa walimu,” alisema Zubeir.Pia, mkuu huyo wa shule aliitaka Serikali kuendelea kuboresha mishahara na maslahi ya walimu, ili kukabiliana na uhaba wa walimu kutokana na wengi kuhama shule au kwenda kwenye shughuli zinazolipa zaidi. Akisoma risala ya wahitimu, Caroline Yesse, alisema kukosekana kwa vitabu vya kutosha kunarudisha nyuma jitihada za wanafunzi kujisomea.Katika mahafali hayo zaidi ya wanafunzi 500 walihitimu kidato cha sita. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani















Comments