MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Biashara Wataka halmashauri kuvunja mkataba
BOOKMARK THIS PAGE
Wataka halmashauri kuvunja mkataba  Send to a friend
Sunday, 29 January 2012 10:23

Dinna Maningo,Tarime
WAJUMBE wa Baraza la Mamlaka ya Mji mdogo wa Tarime, mkoani Mara, wameomba halmashauri kustisha zabuni kwa washindi wanaoshindwa kutimiza mapato.

Wakizungumza kwenye kikao cha baraza la wajumbe wa mamlaka ya mji mdogo wa Tarime, wajumbe hao walisema kuna mzabuni aliyeshinda ujenzi wa Kituo cha Mabasi, vibanda na choo amekuwa halipi mapato.
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo, Mwita Mantago, alisema mzabuni huyo anatakiwa kulipa mapato kila baada ya miezi mitatu ya Sh5.7 milioni kila mwezi, amelipa malipo ya mwezi mmoja pekee na anaonekana kikwazo na ukwamishaji wa mapato kwa mamlaka.

Mantago aliomba mzabuni huyo kupandishiwa kodi kwa madai kuwa, hata ushuru wa stendi anaolipa ni kidogo hauendani na mapato halisi ya makusanyo.

“Mkurugenzi wa halmashauri tunakuomba umuondoe huyo mzabuni, wapewe wengine kwanini alipie ushuru wa stendi pekee wakati anamiliki choo, hoteli na maduka!” alisisitiza na Matango na kuongeza:
“Isitoshe ana zaidi ya miaka minne hajalipa ushuru wa choo, wakati kila mtu anapotaka kwenda chooni analipia Sh200, ana muda wa miaka mitatu hajawahi kulipia ushuru wa vibanda.”

Hata hivyo, mkurugenzi wa Halimashauri ya Tarime, Fidelis Lumato, alimtetea mzabuni huyo kwamba amekuwa akilipa ushuru wa stendi kwa kiwango kinachotakiwa.

“Tunatakiwa ni kumpongeza huyu mzabuni kwa sababu anatulipa vizuri, amelipa ushuru wa stendi kwa asilimia 56 amekuwa akivuka kiwango cha mapato alichotakiwa na halmashauri,” alisema Lumato.
Alisema hivi sasa wamejipanga vizuri katika taratibu za kusaini mikataba ya itakayowashirikisha waombaji, wanasheria na mkurugenzi wa mamlaka ya mji mdogo.

Naye Mkuu wa wilaya hiyo, John Henjewele, alitaka baada ya kusainiwa kwa mikataba itolewe nakala kisha ipelekwe katika mamlaka ya mji siyo kush8ikiliwa na halmashauri pekee.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner