MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Biashara Mkurugenzi TBS ashindwa kutimiza ahadi
BOOKMARK THIS PAGE
Mkurugenzi TBS ashindwa kutimiza ahadi  Send to a friend
Sunday, 29 January 2012 10:34

Ibrahim Yamola
MKURUGENZI  Mkuu wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Charles Ekelege, ameshindwa kutekeleza ahadi yake kukutana na waandishi wa habari ili kutoa vielelezo vya kumsafisha dhidi ya tuhuma za kuwa na ofisi hewa za ukaguzi wa bidhaa zinazoingizwa nchini nje ya nchi.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliliminika katika ofisi kuu za TBS, jijini Dar es Salaam baada ya mkurugenzi huyo kutoa ahadi juzi baada ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), kumbana kwa kile walichoeleza kuwa ni kubaini udanganyifu kwenye mpango wa TBS kukagua bidhaa.

Saa 3.30 asubuhi jana waandishi wa habari walifurika ofisini kwa Ekelege lakini, walijikuta wakiambulia patupu.Baada ya kusubiri kwa takribani saa 1.30 bila ya Ekelege kutokea walimtafuta kwa simu yake ya kiganjani ambayo hata hivyo iliita bila ya kupokelewa, ndipo wanahabari hao wakaamua kwenda  kuonana na sekretari wake ili kujua kama mkurugenzi huyo atafika ofisini kama alivyoahidi.

“Kwa kuwa yeye mwenyewe aliwaambia atakuja hivyo subirieni tu atakuja msiwe na wasiwasi, kaeni nje pale mumsubiri,” alisema Katibu Muhtasi wake ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Baada ya wanahabari kusubiri kwa mda mrefu walirudi kwa katibu muhtasi na kumtaka ampigie simu Ekelege, naye alikubali.

“Nimeongea nae(Ekelege), amesema mumusubiri, yupo njiani anakuja,” alisema katibu huyo muhtasi akiwajibu wanahabari.Baada ya dakika 30 katibu huyo aliwaendea wanahabari hao akiwa na kauli mpya akisema: “Mkurugenzi amesema amepata dharura. Hataweza kufika. Hivyo, amewataka muondoke, mkaendelee na shughuli zingine.”

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo Ekelege aliwaahidi waandishi wa habari juzi kwenye ofisi za Bunge jijini akisema: “Kwa leo siwezi kusema lolote kwa kuwa sina data (vielelezo), kesho (jana) njoo ofisini kwangu nitawaeleza kila kitu, ila kwa sasa siwezi kusema lolote,” alisema Ekelege  

Mkurugenzi huyo alijikuta katika wakati mgumu juzi baada ya Makamu Mwenyekiti POAC, Deo Filikunjombe kueleza kuwa waligundua madudu baada ya kutembelea vituo vya ukaguzi wa magari nchini Singapore na mjini Hong Kong, China. “Tulikwenda Hong Kong na Singapore na tumegundua kwamba TBS ni wababaishaji, huwezi kuamini anachokifanya Mkurugenzi (Ekelege) huko nje.”  
 
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa kamati, Ekelege aliwapeleka katika ofisi hewa  ambayo baadaye waligundua kuwa haikuwa ya ukaguzi wa magari.“Tumekwenda Hong Kong na akatupeleka katika ofisi feki na tulipombana akasema kuwa aliomba kwa muda kuitumia ofisi hiyo,” alisema Filikunjombe.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner