
| Songea yapima viwanja 10,000 | Send to a friend |
| Sunday, 05 February 2012 10:03 |
|
ZAIDI ya viwanja 10,000 vya makazi katika Kata ya Mshangano Manispaa ya Songea vimepimwa hadi sasa na Kampuni ya Ardhi Plan limited ya jijini Dar es Salaam kupitia mradi wa upimaji viwanja ulioibuliwa na wananchi wenyewe. Akizungumza na gazeti hili jana Mwenyekiti wa Mtaa wa Mshangano, Paulo Mangwe alisema mradi huo umekubalika na Wananchi wanaotaka viwanja vyao vipimwe ili kuondokana na makazi holela huku mradi ukitarajia kukamilika Februari mwaka huu. Mangwe alisema kuwa hadi sasa tayari michoro 23 inafanyiwa kazi na kwamba hakuna matatizo yaliyojitokeaza kwa kuwa wananchi wanatoa ushirikiano wakionyesha kuridhishwa na kazi inayoendelea. “Hadi sasa kazi ya upimaji wa viwanja inaendelea vizuri na tayari viwanja 10,000 vimeshapimwa na wananchi wengi wamepata ajira kupitia mradi huo. Tunatarajia ajira zitaongezeka kwa wananchi ,” alisema Mangwe Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa kazi hiyo inafanikiwa kutokana na Kamati ya Upimaji kushinda maeneo ya kazi kusaidia kuwapa wananchi maelekezo wanapopata shida ya kuelewa. Alitoa ushauri kwa kata nyingine na halmashauri nyingine kutumia kampuni kupima viwanja ili kupunguza migogoro ya wanananchi kuuziwa kiwanja kimoja mara mbili. Alisema upimaji huo wa viwanja utasaidia wananchi kupata makazi bora, kwa kuwa thamani ya ardhi yao inapanda kutoka mashamba hadi viwanja, hivyo kuweza kupata Benki za Ardhi. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














