MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Biashara Tarangile watakiwa kuanzisha hifadhi za jamii
BOOKMARK THIS PAGE
Tarangile watakiwa kuanzisha hifadhi za jamii  Send to a friend
Sunday, 05 February 2012 10:03

Mussa Juma,Babati
 WANANCHI wa vijiji  45 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire vimetakiwa kuanzisha Hifadhi za Jamii za Wanyamapori(WMA), ili waweze kunufaika mapato yatokanayo na sekta ya utalii.
 
Mhifadhi  Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Beatrice Kessy alisema hayo mbele ya wanahabari, akieleza kuwa kwa sasa vijiji hivyo havinufaiki ipasavyo na wanyamapori waliopo katika maeneo yao hasa wakati wa masika.
 
Kessy alisema kuwa kuanzishwa kwa WMA katika vijiji hivyo vya Wilaya za Simanjiro, Monduli, Babati, Kondoa na Kiteto  kutasaidia pia kupunguza ujangili wa wanyamapari
 
Alisema kuwa hifadhi hiyo tayari imeanza kuwasaidia  baadhi ya viongozi wa mila na vijiji kutembelea maeneo ambayo WMA zimeanzishwa na kuwa na manufaa makubwa.
 
"Tunawapeleka  WMA wa Burunge na Longido ili kujionea wenzao ambao wamenufaika kwani wanapokea fedha za watalii wanaowatembelea, fedha za kuwekwa mahema na fedha na ujenzi wa mahoteli katika maeneo yao,"alisema Kessey
 
Awali Mhifadhi Mkuu wa Tarangire,Erastus Lufungulo alisema kuwa umuhimu wa kuwa na WMA katika vijiji hivyo ni mkubwa kwani karibu vyote vipo katika maeneo ya mapito ya wanyama na ukanda wa wanyama.
 
"Hili ni eneo la kilomita 30,000 za mraba, lote wanyama wanazunguka na wakati wa kiangazi ndipo wanyama  wengi hurudi ndani ya hifadhi ambapo kuna Mto Tarangire usiokauka maji,"alisema Lufungulo.
 
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ina ukubwa wa kilometa 2850 za mraba ambapo inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner