
| Majaji tuzo za waandishi waapishwa | Send to a friend |
| Sunday, 05 February 2012 10:05 |
|
JOPO la majaji tisa, watakaosimamia tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania (EJAT), kwa mwaka 2011 wameapishwa jijini Dar es Salaam jana. Akizungumza baada ya kuwaapisha majaji hao, Mwenyekiti wa Bodi ya Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Thomas Mihayo alisema kuwa ili kupata mwandishi bora atakayeibuka mshindi, wamelazimika kuwaapisha majaji hao ili kuondoa minong’ono ya hapa na pale. “Leo (jana), nimewaapisha kwa nia ya kusimamia usawa na haki katika zoezi la kumpata mwandishi bora atakaye pata stahiki ya kuchukua tuzo hiyo,”alisema Jaji Mihayo. Katibu Mtendaji wa (MCT) Kajubi Mukajanga alisema, kuwa baada ya majaji hao wa EJAT kuapishwa, walikutana katika kikao cha pamoja ili kujadiliana njia watakazo zitumia katika kumpata mshindi. “Zoezi la kupitia kazi ambazo zimewasilishwa hapa MCT na waandishi mbalimbali wa habari zinaanza leo (jana) mara tu baada ya kuapishwa na kukubaliana njia watakazi zitumia ili kuhalakisha kumalizika kwa zoezi hilo litakalo dumu kwa kipindi cha wiki moja,” alisema Mukajanga. Akifafanua alisema tuzo hizo za EJAT zinazo shirikisha kazi kutoka katika vyombo vya habari za Televisheni,Radio pamoja na Magazeti ambazo ni za tatu kufanyika tangu kuazishwa kwake mwaka 2009 na mshindi wa jumla kwa mwaka huo alikuwa ni Jerry Muro aliyekabidhiwa kitita cha dola za kimarekani 4,000. Alisema tangu kuaznishwa kwa tuzo hizo na EJAT imekuwa ikikua kila mwaka kutokana na washiriki wengi kujitokeza kushiriki hivyo kuwafanya kuongeza vipengele mbambalimbali kutoka tisa mwaka 2009 hadi vipengele 19 kwa mwaka huu. “Mwaka 2009 tulikuwa na vipengele tisa na kazi zilizo wasilishwa zilikuwa 403,Mwaka 2010 tulikuwa na vipengele 16 na kazi zilipokewa 437 lakini kwa mwaka huu tuliongeza vipengele na kufikia 19 ambapo zimeweza kuongeza hamasa kwa wemgi kushiriki kwani tumepokea jumla ya kazi 772 zitakazo shindanishwa ili kumpata mshindi,” alisema Mukajanga. Aliwataja majaji watakao shiriki katika zoezi hilo kuni ni Wanceslaus Mushi atakaye kuwa Mwenyekiti,Attilio Tangalile Katibu wa jopo hilo la majaji,wengine ni Yusuf Chunda,Mwanzo Millinga,Edda Sanga,Pundenciana Temba,Anaclet Rwegayura na Pili Mtambalike. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














