MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Michezo Kocha: Messi kukosa penalti siyo 'ishu'
BOOKMARK THIS PAGE
Kocha: Messi kukosa penalti siyo 'ishu'  Send to a friend
Sunday, 05 February 2012 09:45

BARCELONA, Hispania
KOCHA wa Barcelona, Pep Guardiola amesema kuwa hakuna mchezaji kama Lionel Messi pamoja na kukosa penalti katika mechi ya timu yake dhidi ya Valencia katikati ya wiki.

Mchezaji huyo alishindwa kufunga penalti katika mchezo uliomalizika kwa Barca kutoka sare ya 1-1 na Mestalla ikiwa ni mechi ya kwanza ya Copa del Rey nusu fainali.

"Lionel yuko vizuri wakati wote, ni mchezaji mwenye sifa zote," Guardiola aliwaambia waandishi wa habari. " Ana kila aina ya uwezo, na amefanya mengi na hilo halina ubishi.

"Bila kuwa katika kiwango chake, bado ni mzuri kwa wachezaji wengine. Wakati mwingine huvaa majukumu ya mwingine uwanjani. Linapokuja suala la penalti, hutokea mambo kama hayo. Natumai ataendeleza rekodi yake nzuri.

"Kilichotokea, ukweli ni kwamba kimetuharibia. Tuko kwa ajili ya kumsaidia, na tunafahamu kuwa anahitaji kusaidiwa. Kila mmoja anafurahi kuona Messi yuko uwanjani."

Guardiola alikanusha kusema kuwa timu yake iko kwenye mgomo kwa kile kilichoelezwa kuwa timu yake ilicheza mechi tatu bila ushindi.

"Ni ngumu kufahamu timu inakabiliwa na matatizo gani," aliongeza, "Nitafurahi tu karibuni. Katika mechi dhidi ya Valencia hatukuwachezesha Xavi, [Andres] Iniesta, [David] Villa au  [Daniel] Alves, ambao ni roho ya timu.

"Tulikuwa tunajaribu wengine. Karibu mambo yatakuwa mazuri." Barca iko nyuma kwa pointi saba na Real Madrid.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Sunday, 05 February 2012 10:13
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner