
| Capello apinga Terry kuvuliwa unahodha England | Send to a friend |
| Sunday, 05 February 2012 09:46 |
|
KOCHA wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello na Chama cha Soka England, FA wameingia kwenye mzozo kuhusiana na nahodha wa timu hiyo, John Terry kuvuliwa unahodha kwenye timu hiyo ya England. Capello alikuwa akipigana kuhakikisha beki huyo wa Chelsea anaendelea na unahodha wa timu hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo licha ya FA kufanya uamuzi wa kumpoka unahodha. Pamoja na hayo, vyombo vya habari navyo vimemgeukia Capello kumhadharisha aangalie mkataba wake wa kufundisha England kama una nafasi ya kupingana na masuala yanayoamriwa na FA. Mwenyekiti wa FA, David Bernstein alimwambia Terry juu ya uamuzi wa Bodi ya FA ya kumvua unahodha. Terry baadaye alisema kwamba kwa sasa anafikiria kustaafu soka ya kimataifa. Beki huyo alipatikana na hatia ya kufanya vitendo vya kashfa ya ubaguzi wa rangi Oktoba mwaka jana kwa mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand. Nahodha huyo wa Chelsea alikanusha kuwepo kwa hali hiyo lakini FA ilimtia hatiani. FA ilisema kuwa Terry hatakuwa nahodha wa timu ya taifa hadi suala lake litakapopatiwa ufumbuzi. Capello alikubali kwa kuwa hakuwa na mamlaka ya kuingilia kati hilo, lakini kwa sasa anaonekana kukerwa na maamuzi ya FA. Mapema kabla ya suala la ubaguzi kuibuka, FA ilimsimamisha Terry unahodha lakini Capello alikwenda kinyume na alimteua Terry kinyemela kuwa nahodha mapema Machi mwaka jana ikiwa ni baada ya miezi 13. Capello alifanya hivyo kama vile haoni kwani alikuwa akiamini kuwa Terry ni mchezaji kiongozi uwanjani. Alimtetea hadi dakika ya mwisho licha ya Rio Ferdinand kupewa mikoba yake uwanjani. Uamuzi wa kumrudisha terry ulizua mkorogano kwenye timu hiyo. Kocha huyo alisema kuwa anataka Terry kuiongoza England kusaka tiketi ya Euro 2012 katika mechi dhidi ya Poland na Ukraine. Capello alichanganyikiwa zaidi baada ya kaka wa beki wa Manchester United, Rio Ferdinand - Anton Ferdinand kumshinikiza kumvua unahodha Terry, licha ya kuwa alikuwa anataka amuone kikosini. Ferdinand naye baadaye alisema kuwa awali alipewa unahodha, lakini hakufurahishwa na jinsi kocha huyo alivyomvua unahodha wake na kumpa tena Terry. |
| Last Updated on Sunday, 05 February 2012 10:11 |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














