MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Michezo Wachezaji, viongozi CDA wasimamishwa
BOOKMARK THIS PAGE
Wachezaji, viongozi CDA wasimamishwa  Send to a friend
Sunday, 05 February 2012 09:46

Masoud Masasi, Dodoma
CHAMA cha Soka Mkoa wa Dodoma, Dorefa, kupitia Kamati ya Mashindano ya Ligi Taifa ngazi ya mkoa imewafungia mechi tatu kila mmoja wachezaji na viongozi wawili wa timu ya CDA kutokana na kufanya utomvu wa nidhamu wa kumpiga mwamuzi  wakati wa mchezo wao dhidi ya Magereza Mpwapwa.

Timu hiyo ambayo inahaha kupanda daraja, ilifanya kitendo kisicho cha kiungwana hivi karibuni baada ya kumvamia mwamuzi Kimu Rajab mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kuanza kumshambulia kwa kile kilichoelezwa aliwapendelea wapinzani wao.

Katibu wa Dorefa, Aboubakar Ibrahim alisema kuwa kamati ya mashindano iliyokaa juzi  ambayo ilipitia taarifa ya msimamizi wa mchezo na mwamuzi huyo imeamua kuwafungia  mechi tatu wachezaji na viongozi wao.

Ibrahim aliwataja wachezaji hao kuwa ni Aron Michael na Tamimu Abdul amao pia wametozwa faini ya Sh50,000 kila mmoja huku kwa upande wa makocha hao Mrisho Songa na Juma Ikava wakitozwa Sh60,000 kila mmoja.
“Hili litakuwa fundisho kwa timu nyingine kuzingatia nidhamu kwa kuwa safari hii tunataka kutoa timu yenye nidhamu na hatotokuwa na mzaha kwa hili,” alisema katibu huyo.

Alisema kwa upande wa waamuzi kamati hiyo imetoa onyo kali kwa Shukuru Said, Omari Juma na Linyasi Saidi kutokana na kutokuwa makini uwanjani  na kutakiwa kuongeza umakini  wanapokuwa kwenye mechi.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Sunday, 05 February 2012 09:53
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner