MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Michezo Mshindi Fun Run Moshi kuzoa laki 2
BOOKMARK THIS PAGE
Mshindi Fun Run Moshi kuzoa laki 2  Send to a friend
Sunday, 05 February 2012 09:47

Sosthenes Nyoni
MSHINDI wa mbio za kujifurahisha zinazodhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Fun Run atazawadiwa Sh200,000 wakati mshindi wa pili atazoa Sh160 huku wa tatu akiondoka na Sh120,000.

Meneja matukio wa Vodacom, Rukia Mtingwa aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi ikilinganisha na mwaka jana ili kuleta msisimko zaidi na ushindani.

Mbio za Fun Run ni miongoni mwa mbio zinazoshindaniwa katika mbio za kila mwaka za Kilimanjaro Marathon ambazo mwaka huu zitafanyika Februari 26 kwenye mji wa moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema kuwa zawadi hizo ambazo ni kwa wanaume na wanawake, washindi wa nne hadi na wa tano watazawadiwa Sh100,000 na Sh80,000.

Mtingwa alisema kuwa mbali na fedha hizo, kutakuwa na zawadi kwa wakimbiaji wazee kwa mwanamke na mwanamke ambao kila mmoja atapata Sh100,000.

Mbali na mbio hizo, Vodacom imekuwa ikidhamini mashindano mbalimbali ikiwemo mbio za mashua, majahazi, Ligi Kuu Bara, mashindano ya baiskeli na mikokoteni.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner