MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Michezo Angetile alazwa
BOOKMARK THIS PAGE
Angetile alazwa  Send to a friend
Sunday, 05 February 2012 09:48

Vicky Kimaro
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah amelazwa hospital ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua ghafla jana ugonjwa unaodhaniwa kuwa ni Kiharusi.

Kabla ya kupelekewa Muhimbili, Osiah alipelekwa hospital ya Agakhan na kupewa matibabu ya awali na kisha taratibu za kumhamishia zikafanyika.

Taarifa za kuumwa na kulazwa kwake zilithibitishwa na mke pamoja na Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.
"Ni kweli anaumwa na hapa tuko Agakhan tunajiandaa kupeleka muhimbili kwa matibabu zaidi," alisema mke wa Osiah.

Alipoulizwa kuhusu ugonjwa unaomsumbua Osiah, alisema: "Mimi sijui anaumwa nini." Majibu kama hayo pia alitoa Wambura ambaye alikwenda hospitali kumjulia hali.

Aidha, ndugu wa karibu wa Osiah aliyejitambulisha kuwa ni dada yake, alisema ndugu yake huenda amepatwa na ugonjwa wa Kiharusi ingawa hali yake si mbaya sana.

"Hali yake ilibadilika ghafla jana asubuhi na mke wake kuamua kumkimbiza hospitali," alisema ndugu huyo.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner