
| Ghana, Tunisia kusaka tiketi leo | Send to a friend |
| Sunday, 05 February 2012 09:48 |
|
BATA, Equatorial Guinea Mshindi wa mechi hiyo atakumbana na mshindi wa robo fainali nyingine kati ya Zambia na Sudan watakaopambana Jumatano ijayo mjini Bata, Equatorial Guinea. Ghana (Black Stars) ilifikia hatua hiyo baada ya kuifunga Botswana bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo, na kisha kuifunga Mali mabao 2-0, kabla ya kwenda sare ya 1-1 na Guinea katika mechi ya mwisho ya Kundi D. Kocha wa Ghana, Goran Stevanovic, aliyetoa ahadi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo hapo Februari 12, amesema kikosi chake kitacheza vizuri. Kiungo anayecheza soka la kulipwa, Ukraine Derek Boateng, yeye alisema wazi kuwa mechi ya leo ni mtihani mkubwa kwao. "Tunisia wana timu nzuri. Wana nidhamu kubwa uwanjani kama ilivyo kwa Guinea," alisema Boateng, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Guinea. "Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu, lakini ni matarajio yetu tutafanya kila linalowezekana kushinda na kwenda nusu fainali." Nahodha wa zamani wa Ghana, Sammy Kuffour alisema kikosi chao ni lazima kiwe makini kumkaba mshambuliaji hatari wa Tunisia, Youssef Msakni aliyefunga bao nzuri dhidi ya Morocco. "Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa uwanjani, lazima macho yawe kwake muda wote wa mchezo," alisema Kuffour. "Labda kocha atampanga mtu maalum wa kumchunga kama alivyofanya wakati tukicheza na Mali Seydou Keita kupewa ulinzi mkubwa." Nahodha John Mensah amepata nafuu baada ya kuumia misuli. Tunisia inaonekana kuwa mshindani wa kweli wa Ghana baada ya kupita Kundi C ambalo lilimaliza mechi, huku wenyeji Gabon wakishika nafasi ya kwanza. Timu zingine ni Morocco na Niger. Tunisia (Carthage Eagles) waliotwaa ubingwa wakati walipoandaa fainali za mwaka 2004 ikiwa ni mara ya tatu, waliwafunga Ghana bao 1-0 ilipocheza nayo mara ya mwisho mwaka 2006 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani














