MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Michezo Walcott ang'ara Arsenal ikishinda 2-1
BOOKMARK THIS PAGE
Walcott ang'ara Arsenal ikishinda 2-1  Send to a friend
Saturday, 28 August 2010 19:56

LONDON , Uingereza
THEO Walcott ameendelea kung'ara msimu huu baada ya kuifungia Arsenal bao la kuongoza katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa mapema jana kwenye Uwanja wa Ewood Park.

Bao hilo la dakika ya 20, hata hivyo lilifutwa na Mame Diouf, raia wa Senegal ambaye anaichezea Blackburn Rovers kwa mkopo akitokea Manchester United, dakika saba baadaye  kutokana na pasi  ya 'kaka' yake El- Hadji Diouf.

Andrei Arshavin alikamilisha ushindi kwa timu yake baada ya kupachika bao la dakika ya 51 mbele ya watazamaji  25,059.

Katika mchezo huo ambao timu zote zilishambuliana kwa kiasi kikubwa, mwamuzi Chris Foy alimwonyesha kadi ya njano Gael Givet pekee.

Katika hatua nyingine, Arsenal imepangiwa kucheza na Tottenham Hotspur raundi ya tatu ya Kombe la Ligi (Carling Cup) mwezi ujao.

Katika ratiba iliyotolewa jana, klabu hizo za London Kaskazini zimekutanishwa huku klabu nyingine za ligi hiyo, Aston Villa itacheza na Blackburn, timu hizo zilikutana hatua ya nusu fainali msimu uliopita.

Chelsea ambayo imeanza msimu wa ligi kwa kishindo itaikaribisha Newcastle iliyoanda daraja na Manchester City imepangiwa kucheza  dhidi ya West Bromwich Albion.

Mabingwa watetezi, Manchester United  wamepangwa dhidi ya timu ndogo ya Scunthorpe na Liverpool ikipata mtelemko kwa Northampton ya daraja la nne kwenye mechi ambazo zitaanza Septemba 20.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
  • Kupiga Kura

  • Jumapili


Ajali ya Meli ZnZ inatufundisha nini?