
| Kombe la Taifa kikapu Nov. | Send to a friend |
| Saturday, 28 August 2010 19:58 |
|
MASHINDANO ya mpira wa kikapu kuwania Kombe la Taifa yamepangwa kufanyika baadaye Novemba mwaka huu yatajumuisha mikoa yote ya Tanzania. Katibu msaidizi wa Chama cha mpira wa kikapu Tanzania, Michael Maluwe alisema kwa sasa wako katika mchakato wa kutafuta wadhamini wa kusaidi kufanikisha mashindano hayo mapema Novemba. Maluwe aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa mpaka sasa hawajapanga tarehe kamili ya kuanza mashindano hayo na wako katika mazungumzo na wadhamini. Alisema mashindano hayo tayajumuisha mikoa yote ya Tanzania na lengo kubwa ni kupata wachezaji waliofanya vyema na kuunda timu ya taifa na wengine kuwakilisha mikoa yao katika mashindano mbalimbali ya ndani na je ya nchi. "Bado tupo katika mchakato wa kupata wadhamini ingawa tayari tumepanga yatafayika Novemba ila tarehe bado hatujapanga kwa sasa...cha msingi tunaiomba mikoa ianza maandalizi yao mapema ya kuandaa mashindano," alisema Maluwe. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Links za wateja na washirika wetu
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani












