MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Uchambuzi & Maoni Tuache siasa suala la waathirika wa mafuriko
BOOKMARK THIS PAGE
Tuache siasa suala la waathirika wa mafuriko  Send to a friend
Saturday, 14 January 2012 19:29

    

   KAYA zipatazo 300 za watu walioathirika na mafuriko yaliyotokea mwishoni mwa mwezi uliopita jijini Dar es Salaam, jana zilitarajiwa kuhamishiwa katika makazi mapya zilizopewa na Serikali katika eneo la Mabwepande, wilayani Kinondoni nje kidogo ya jiji hilo. Mafuriko hayo yalichukua maisha ya watu zaidi ya 40. Serikali mkoani Dar es Salaam ilifanya kazi ya ziada kwa kuwahamishia maelfu ya waliokosa makazi katika kambi mbalimbali jijini na kuhakikisha wanapewa ulinzi na huduma zote muhimu.
   Tunaipongeza Serikali Kuu na uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusimamia vyema zoezi hilo kwa umakini mkubwa na kuweza kuratibu misaada iliyotolewa na watu na taasisi mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko hayo. Kazi kubwa inayoikabili Serikali hivi sasa ni kuhakikisha inawapatia waathirika wote wa mafuriko hayo huduma muhimu angalao kwa miezi mitatu ijayo ili wapate fursa ya kujitegemea na kuanza maisha mapya.
   Jukumu hilo linaloikabili Serikali ni zito mno kwa vigezo vyovyote vile, kwani ni jukumu lililojaa changamoto za kila aina. Tayari watu wasiohusika wamejitokeza kuhakikiwa kama waathirika. Hivyohivyo, imegundulika kuwa, baadhi ya watu wasiohusika wamejitokeza kupewa viwanja huko Mabwepande wakati siyo wamiliki wa nyumba zilizoathiriwa na mafuriko hayo.
  
    Serikali imesema idadi hiyo ya kaya 300  zilizotarajiwa kuhamishiwa Mabwepande jana ni ya awamu ya kwanza kati ya kaya 659 zilizohakikiwa za waathirika waliokuwa kwenye kambi mbalimbali jijini. Tunayo matumaini makubwa kwamba Serikali itaweza kuhitimisha zoezi hilo kwa ufanisi iwapo itaepuka kutoa ahadi za uongo, zisizotekelezeka na za kufurahisha baraza.
   Ndiyo maana tumefadhaishwa na habari zilizochapishwa na gazeti dada la Mwananchi Jumamosi kwamba Rais Jakaya Kikwete alipotembelea kambi ya Mabwepande juzi na kupokelewa na mabango yaliyobebwa na waliokuwa wapangaji wa nyumba zilizoathiriwa na mafuriko,  ghafla kwa mshangao wa serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, aliagiza kwamba nao watafutiwe viwanja kama ilivyo kwa wamiliki wa nyumba zilizokumbwa na mafuriko.
   Ni kweli kwamba wapangaji waliokuwa katika nyumba hizo wanastahili msaada wa Serikali kwa sababu hawatazamiwi kwa sasa kuwa na fedha za kulipa kodi ya pango, hasa kwa kutilia maanani kwamba fedha na mali zao zilikwapuliwa na mafuriko hayo. Pia wamiliki wa nyumba walimokuwa wakiishi nao hawawezi kuwarudishia fedha za pango kwa sababu nao walipoteza kila kitu katika maafa hayo.
   Hata hivyo, sisi tunadhani Serikali ilitoa tahadhali na muda wa kutosha kwa wamiliki na wapangaji wa nyumba hizo kuhama mabondeni. Watu hao waliidhalilisha Serikali kwa kukaidi amri hiyo, tena kwa kauli za kejeli. Iweje sasa Serikali itoe motisha (incentive) kwa kuwapatia viwanja watu wasiotambua mamlaka yake? Serikali itambue kwamba ina kikomo au mpaka inaoweza kutoa msaada kwa watu hao. Zaidi ya hapo ni siasa tu.
  

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner