MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Uchambuzi & Maoni Bwagamoyo:Tanzania pepo ya wabunge, wateule wachache , wateuaji
BOOKMARK THIS PAGE
Bwagamoyo:Tanzania pepo ya wabunge, wateule wachache , wateuaji  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 20:22


Na. L. W. Nzela
HAPANA shaka tena kuwa ukitaka kuwa na usalama wa maisha yako, mali zako, na nafasi yako jitahidi uwe mwanasiasa tena uwe mwanasiasa wa ngazi ya juu. Usifikirie kuwa mwenyekiti wa mtaa au kijiji – hivi havilipi.  Fikiria kuanzia ngazi ya Ubunge. Ukitaka kuionja pepo – yaani Tanzania – jitahidi ugombee ubunge au fanya kila jitihada upate kuteuliwa kushika nafasi moja kubwa. Nchi yangu imegeuzwa kuwa pepo ya wanasiasa.
Nimechukua muda kidogo kujifunza juu ya mafao ya viongozi na wanasiasa wanapostaafu. Yaani, haki zao mbalimbali walizo nazo za mafao ya uzeeni na kulinganisha hizo haki zao na zile ambazo zinaongozwa watumishi wengine wa umma. Kumekuwa na sheria tatu ambazo zimesimamia kwa muda mrefu wa historia yetu kama taifa ambazo ni Sheria ya Viongozi Wastaafu wa Kisiasa ya 1981, Sheria ya Mafao ya Viongozi Mahsusi wa Nchi ya 1986 na Sheria ya Wastaafu wa Utumishi wa Kisiasa ya 1999.
Sheria hiyo ya mwisho ndiyo inasimamia mafao ya viongozi wetu mbalimbali wa kisiasa kuanzia Rais hadi Mkuu wa Wilaya.
Ukisoma sheria zote hizo utajikuta mara moja unapatwa na hasira hasa unapoisoma Sheria ya 1999 ambayo ndiyo inasimamia mafao ya viongozi wetu unaowaona kila siku wanatembea na magari yenye bendera, wenye kupigiwa saluti au wakati mwingine kuzungukazunguka katika viti vyao vile vyekundu vikubwa bungeni; wakiwa macho au wamelala.
Ni vizuri kukumbushia kuwa watumishi hawa wanaopewa mafao haya mara nyingine hawalingani kwa muda waliolitumikia taifa katika nafasi hizo na watumishi wa kawaida wa umma ambao wengi wao wanapofika muda wa kustaafu wanakuwa wameli tumikia taifa kwa miaka kati ya 25 na 40.
Mafao ya Rais Mstaafu
Mtu aliyewahi kushika nafasi ya urais akimaliza muda wake,  baadhi ya mafao yake ni haya yafuatayo:
•    Mafao ya mwaka atakayolipwa kwa mwezi yakiwasawa na asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyepo madarakani.
•    Mkono wa shukrani wa kiasi kinacholingana na asilimia50 ya mishahara yake yote alipokuwa madarakani (kama alikaa miaka kumi basi atalipwa kiasi cha mishahara yake ya miaka mitano!).
•    Posho ya miezi 24 ikilingana na mshahara wa rais aliyeko madarakani. Hizo ni fedha tu!
Pamoja na fedha, Tanzania inampatia mtu aliyekuwa rais vingine kama nyumba inayohudumiwa na serikali ambapo atapewa kiasi cha asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani kama matunzo pamoja na wasaidizi tisa! Makamu wa Rais mstaafu naye anapewa kwa kiasi kikubwa aina hiyohiyo ya mafao japo kwa kulinganisha na Makamu wa Rais aliyeko madarakani

Mafao ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu
Mtu aliye wahi kuwa Waziri Mkuu atapokea pensheni ya kila mwezi sawa na asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani. Pia atapewa mkono wa shukrani sawa na asilimia hamsini ya mshahara wake katika muda wote aliowahi kuwa madarakani. Naye pia atapewa fedha za kuagana sawa na mshahara wa miezi 24 (miaka miwili) ya Waziri Mkuu aliyepo madarakani. Waziri Mkuu mstaafu naye atapewa baadhi ya vitu vingine ikiwemo posho ya kujikimu ambayo itakuwa sawa na asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani. Vilevile atapewa wasaidizi sita wa kumhudumia!
Kwa hawa wote hatujazungumzia vitu kama ulinzi, magari ambavyo vinakuja pamoja na vitu kama bima ambavyo anapatiwa kwa matibabu ndani ya nchi (ikumbukwe bima anayopewa hailipi nje ya nchini kwa matibabu ya hapahapa nchini). Spika naye anapatiwa mafao ya aina kama hiyo japo hayakaribii yale ya Rais, Makamu au Waziri Mkuu Mstaafu.
Mbunge mstaafu
Sasa wabunge nao wanapofikia mwisho wa kazi yao, anapewa mafao mbalimbali. Anapewa mafao hayo vilevile hata kama atagombea tena na kurudi Bungeni kwani ule muda wa miaka mitano iliyopita unahesabiwa ni mwisho wa kazi yake. Anapoingia tena anaanza upya. Anapewa asilimia 40 ya mshahara wake kwa miaka yote ambayo ametumikia kama fedha ya jumla. Mbunge huyo mstaafu naye atapewa posho ya kumaliza kazi ikiwa sawa na asilimia 20  ya mishahara yake yote aliyopokea kwa miezi 24.
Sasa kitu cha kuudhi kuna vitu viwili vya harakaharaka. Kwanza, mapato hayo yote ambayo ni mamilioni ya shilingi kwa mujibu wa sheria hii havilipiwi kodi!
Kwa hiyo ndugu zetu hawa wanajua wanapomaliza miaka yao ya utumishi wanakusanya taratibu bila kodi. Jambo la pili la kuudhi ni kuwa haijalishi hawa watu walifanya kazi gani, au walishika nafasi zao vipi. Mwadilifu na fisadi wote wanapata sawa, aliyeuza nchi na aliyepigania wote wanapewa sawasawa; yaani aliyestaafu vizuri au aliyejiuzulu kwa kuzira au kukerwa wote wanapewa mafao sawa! Sheria za 1981 na 1986 zilikuwa na vipengele tofauti kwani zilizuia wazi kabisa mafao kwa viongozi wabovu!
Ukichukulia pamoja na ujiko mwingine wote unaokuja na ofisi zao ni lazima ukubali kuwa “uanasiasa ni dili”. Na sasa unapoona watu hawa ambao tayari wametengenezewa mfumo tofauti kabisa wa pensheni ukilinganisha na watumishi wengine wa umma wanajiongezea posho karibu asilimia 200 huku  madaktari (watumishi wa kawaida wa umma) ni lazima uone kuwa Tanzania ni pepo kwa wachache wetu. Ndiomaanautaonakuwawabungewamekaakiposhoposhozaidikiasikwambajapowapowanaopingaposhozavikaowatuhaohaowanakubaliposhonyingine.Mimi naamini hata hizi posho za vikao zikibadilishwa jina – Posho za uongozi, au posho za kulitumikia taifa- zaweza kabisa kukubaliwa.
Cha kuudhi ni kuwa wapo watu wanashangaa madaktari kugoma! Hivi, katika mazingira haya walimu wakigoma tushtuke? Hivi, leo hii tukisia wauguzi nao wamegoma tutashangaa? Hivi, ukisikia daktari anaacha kutibu watu nakukimbilia kwenye siasa utashangaa?
Hivi tukipunguza haya mafao ya hawa ndugu zetu kweli tutakuwa na watu wanagombania kwenda Ikulu au huko Bungeni? Kwa vile wanaoandika sheria ni wao   hivi tunafikiria kuwa watakuja kupunguza mafao yao wenyewe na posho zao bila wananchi kukasirishwa? Vyama vya wafanyakazi vinapokaa kwenye mazungumzo ya miaka nenda rudi kuboresha mafao ya wafanyakazi halafu wanasiasa wetu kwa kauli moja tu wanajipa mafao bora na vyama hivyo vinapepesa macho tu, tuna matumaini?
Historia huandikwa na wale wenye kuleta mabadiliko siyo wanaoombea mabadiliko yaletwe! Kwa ni hawa historia huwasahau kwa haraka kama umande upoteavyo jua linapochomoza. Pepo hii ya watawala wetu Watanzania wengine wataionja vipi?
Niandikie: This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner