MwanzoContactsEmail
Home Habari Matukio ya kusisimua RC ahimiza matumizi ya nishati mbadala wa kuni
BOOKMARK THIS PAGE
RC ahimiza matumizi ya nishati mbadala wa kuni  Send to a friend
Thursday, 03 June 2010 08:33

Israel Mgusi, Singida

UHARIBIFU wa mazingira hasa unaotokana na ukataji miti hovyo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida na sehemu nyingine nchini, unaweza kukoma kama jamii itajikita katika matumizi ya nishati mbadala wa kuni na mikaa.

Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Pascal Kone, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa mitambo inayozalisha gesi kwa kutumia kinyesi kibichi cha wanyama hasa ng'ombe.

Uzinduzi huo ulifanyika   sambamba na maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, yaliofanyika katika Kijiji cha Muhalala, wilayani Manyoni.

Kone alisema nishati mbadala ndilo jibu pekee kwa uhai na usalama wa mazingira nchini.


Mkuu huyo wa mkoa ambaye hata hivyo aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni,Ali Rufunga, alisema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa iliyokubuhu kwa uharibifu wa mazingira unaotokana na uvunaji wa mkaa na kuni.

Alisema kama hali hiyo ikiendelea, kuna hatari ya kuzalisha matatizo mengi yatokanayo na uharibufu unaofanyika sasa ikiwa ni pamoja na jangwa.

Alisema kwa kuwa mitambo iliyozinduliwa inazalisha gesi inayoweza kutumika katika kupikia, kuzalisha mwanga (taa) na mbolea, ni vema wananchi wakatumia fursa hiyo kuokoa mazingira badala ya kuendelea kuharibu.


Mitambo hiyo ya kuzalisha nishati ya gesi kwa kutumia kinyesi cha wanyama(biogas) katika Kanda ya kati inaratibiwa na kusambazwa na Shirila la Migesado.

Meneja mradi wa shirika hilo, Hebert Kitange, alisema suala la uhifadhi wa mazingira ni la kila mtu na kwa kulitambua hilo, shirika lake limeamua kupeleka mradi wa gesi inayoweza kupatikana kiurahisi zaidi ili kumwezesha kila mwananchi, kunufaika.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner