MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Mauaji Songea
BOOKMARK THIS PAGE
Mauaji Songea  Send to a friend
Wednesday, 22 February 2012 21:16

POLISI WAUA RAIA WANNE WAJERUHI 41
Waandishi Wetu
MJI wa Songea na viunga vyake jana ulikumbwa na machafuko makubwa yaliyofanya polisi waue watu wanne baada ya wananchi kuandamana wakipinga mauaji yanayodaiwa kuambatana na imani za kishirikina tangu Novemba mwaka jana.

Katika machafuko hayo watu wengine 41 walijeruhiwa, wawili wakiwa katika hali mbaya huku shughuli za kiuchumi na kijamii zikisimama kwa muda.

Hata hivyo, idadi hiyo ya vifo na majeruhi inatofautiana kati ya ile iliyotolewa na jeshi la polisi, uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Wakati polisi ikisema waliokufa ni wawili na majeruhi ni 10, uongozi wa hospitali ya mkoa umesema umepokea maiti nne na majeruhi 41 na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inasema waliokufa ni wawili na majeruhi ni 20.

Tukio hilo la kwanza kutokea katika historia ya Mji wa Songea, lilitokana na hatua ya wananchi kuamua kuandamana kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuelezea kilio chao baada ya kuwepo kwa mauaji ya mara kwa mara ya raia tangu Novemba mwaka jana ambao baada ya kuuawa wamekuwa wakinyofolewa sehemu zao za siri.
Hadi jana, imeripotiwa kwamba watu tisa wameshapoteza maisha katika mazingira hayo kwa nyakati tofauti. Habari zilizopatikana mjini Songea zinasema kwamba mauaji hayo yanayohusishwa na imani za kishirikina yakidaiwa kufanywa na wachimba madini wa migodi iliyoko nchi jirani.
Maandamano na vurugu

Maandamano hayo yaliibuka baada ya jana asubuhi mtu mmoja wa kiume kukutwa amekufa kwa kukatwa mapanga eneo la Makarawe huku pia sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.

Baada ya kuuona mwili huo wa marehemu, umati wa watu ulianza kukusanyika na kuamua kuandamana wakisema kwa amani ili kuwasilisha kilio chao kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Maandamano hayo yalivuta umati watu na mamia ya wananchi walijiunga na kuanza kutembea kwa miguu huku wengine wakiwa katika pikipiki maarufu kwa jina la 'Yeboyebo,' kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa zilizo jirani na Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Ruvuma.

Kadri wananchi hao walivyokuwa wakiendelea kuandamana, habari zilitapakaa mitaa mbalimbali na kuwafanya wananchi wengi zaidi kuungana nao, hali iliyowalazimu polisi nao kujipanga kuwazuia kwa kutumia mabomu ya mchozi.

Hata hivyo, wananchi walizidi kuongezeka wakipinga hatua hiyo ya polisi kuwazuia kufikisha ujumbe wao kwa Mkuu wa Mkoa. Katika hatua hiyo, ndipo vurugu zilipoanza kwani wakati polisi watumia mabomu ya kutoa machozi, baadhi ya waandamanaji walianza kuvurumisha mawe hali iliyowafanya watu kukimbia huku na huko.

Vurugu zilishika kasi hali iliyowafanya polisi kuanza kutumia risasi za moto katika kile ilichodai baadaye kwamba ni katika kujilinda na ndipo vifo hivyo vilipotokea na idadi hiyo kubwa ya majeruhi. Hata hivyo, haikuelezwa mara moja kama miongoni mwa majeruhi hao alikuwamo askari polisi.

Baada ya mauaji hayo, vurugu zilizidi kusambaa katika mitaa mbalimbali ya Mji wa Songea huku wananchi wakianza kurusha mawe kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi. Lakini wengine waliendelea kupigia kelele madai yao ya msingi huku wakilishutumu jeshi hilo kwa kushindwa kudhibiti mauaji hayo kwa muda mrefu.
Vurugu hizo zilisababisha ofisi za Serikali na taasisi binafsi mkoani Ruvuma kufungwa kwa muda yakiwemo maduka, masoko na huduma za kifedha katika mabenki kusimama kwa muda.

Huduma za usafiri katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani nazo zilisimama, huku madereva wa mabasi na abiria wakikimbia kujificha kuepuka mabomu ya machozi na risasi za moto zilizokuwa zikipigwa hewani.

Pia huduma za matibabu katika Hospitali ya Mkoa zilisimama kwa muda baada ya walinzi wa hospitali hiyo kufunga lango kuu, kutokana na wananchi wengi kukimbilia huko wakikimbia mabomu.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zimeeleza kuwa maandamano hayo yalichochewa na taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa juzi kwamba mauaji hayo yanahusiana na masuala ya kipenzi. Ilielezwa kwamba wananchi walikuja juu wakipinga madai hayo ambayo pia yaliripotiwa jana na gazeti hili.

Utetezi wa Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda alisema polisi ililazimika kutumia nguvu ya ziada baada ya wananchi kukaidi amri ya kuwataka watawanyike.
Alidai waliopoteza maisha kutokana na vurugu hizo ni wawili na majeruhi 10 akisema watu hao walifariki dunia kwa kupigwa risasi za moto baada ya kukaidi amri ya polisi kutawanyika.

“Tulilazimika kutumia risasi za moto baada ya hawa vijana kukataa kutii amri ya polisi,” alisisitiza Kamanda Kamhanda.
Kamanda Kamhanda alisema watu 56 wamekamatwa kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na tukio hilo.
Kamanda Kamhanda alisema ingawa bado uchunguzi unaendelea, taarifa za awali zinaonyesha kuwa chanzo cha vurugu hizo ni imani za kishirikina na siasa. Hata hivyo, hakufafanua ushirikina wala siasa zilivyochochea maandamano hayo.
RC atoa amri ya kutombea usiku

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu alisema vurugu hizo zilizodumu kwa saa sita zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na kuhatarisha usalama katika mji huo.

Kutokana na hali hiyo, alitoa amri ya kutotembea usiku akisema msako wa kuwasaka watuhumiwa wa maandamano hayo bado unaendelea.

“Kama watakuwa hawana shughuli za muhimu wabakie tu majumbani mwao ili kuepuka usumbufu. Polisi itaendelea kuwasaka watuhumiwa usiku ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria,” alisema.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa kauli hiyo baada ya kuongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichoitishwa ghafla kutokana na machafuko hayo makubwa.
 
Hospitalini
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Benedicto Ngaiza alisema kati ya watu nne waliokufa na miili yao kupokewa, miwili ilikuwa na majeraha ya risasi na majeruhi wawili  kati ya hao 41, walipelekwa chumba cha upasuaji kwa kuwa walikuwa na majeraha ya risasi pia.
“Hii miili ilikuja kwa awamu, mara ya kwanza ulikuja mmoja na mara ya pili ikaja mitatu. Yote ililetwa kwa magari ya polisi,” alisema Dk Ngaiza na kuongeza:
“Katika hii mitatu iliyokuja kwa pamoja miwili ilikuwa na majeraha ya risasi na mmoja alikuwa ni kijana aliyegonga mti na pikipiki akikimbia vurugu hizo. Kati ya majeruhi hao wawili wamepelekwa chumba cha upasuaji shida yao pia ni majeraha ya risasi.”

Kisa cha maandamano
Tangu Novemba mwaka jana, kumekuwa na matukio ya mauaji katika Mji wa Songea kwa nyakati tofauti hadi sasa ambayo yamekuwa yakitokea katika mazingira ya kutatanisha huku miili ya marehemu ikiwa imejeruhiwa kwa kukatwa mapanga, shoka au marungu na kunyofolewa sehemu za siri.

Hali imekuwa mbaya zaidi mwishoni mwa wiki ambako kwa siku tatu mfululizo mauaji hayo yalitokea hali iliyochochea hasira za wananchi hadi kufikia uamuzi wa kuandamana.

Watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo wanashikiliwa na polisi. Watuhumiwa ni Johari Kassim (16), Onesmo Hinju (14), Samason Haule (22) na Mussa Fuala (20) wote wakazi wa Mtaa wa Lizaboni mjini Songea.

Kilio chasikika

Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imewataka watendaji na wenyeviti wa mitaa na mabalozi kuanzisha ulinzi wa doria za usiku katika maeneo yao kuanzia sasa na kwamba ambaye tukio la mauaji hayo ya kishirikina yatatokea katika mtaa wake atakamatwa na kuchukuliwa hatua.

Katika kikao cha kamati hiyo kilichowashirikisha pia viongozi hao, imeamuliwa pia kwamba watendaji hao wa ngazi ya msingi ya Serikali za Mtaa watalazimika pia kuwatambua wageni wote watakaofika katika maeneo yao ni pamoja na kuwataka waonyeshe vitambulisho vyao na wale watakaokuwa na shaka nao watoe taarifa zao katika vyombo vya sheria.
 
Habari hii imeandaliwa na Joyce Joliga, Kwirinus Mapumba Songea na Fredy Azzah, Dar

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Friday, 24 February 2012 00:21
 

Comments 

 
0 #65 2012-02-25 10:02
TANZANIA INAJULIKANA KWA MATAIFA MENGINE KUWA NI NCHI YA AMAN LAKIN KWANINI WATU WAFANYE MAANDAMANO YA AMAN WAUAWE AU HAO ASKARI WANAOWAUA WANATETEA UPANDE MMOJA?Kama sivyo kwanini wananchi waishi kama ndege ee mheshimiwa raisi tunaomba uingilie kati.
Quote
 
 
0 #64 2012-02-24 04:56
laiti wananchi tungezijua sheria zetu kingenuka.nilishuhudia kwa macho yangu polis wakiwapiga mabom na risasi wananchi.risas hzo kwanin wasitumie kwa wauaji.ni bora nchi iuzwe kila mtu apewe chake kuliko kuwa na siri kali yenye u[NENO BAYA] ndan.
Quote
 
 
0 #63 2012-02-24 01:16
#43dismas umesema kweli kabisa! Polisi na FFU huwa wanajivuna kuonyesha misuli yao kwa kuwakong'ota watu kwa kutumia hata silaha za moto
Mauaji yanatokea HAKUNA YEYOTE TOKA SERIKALINI ANAYEFUATILIA/KWANINI MAUAJI HAYA YAMETOKEA.
yaani watu wanauawa hovyo, kwao ni sawa tu mradi sio ndugu au watoto wao.UTU NA ELIMU NI VITU MUHIMU SANA(SIJUI HUKO VYUONI WALI!KOSOMEA KAZI ZAO WALIFUNDISHWA NINI?Lakni kila kitu kina mwisho!Kauli yeyote kutoka Mkuu wa polisi TZ? Rais?waziri wa mambo ya ndani?waziri mkuu wote kimya!
Mbunge wa Songea,RC,DC?Kimyaa!Ole wenu!
Quote
 
 
0 #62 2012-02-23 23:55
Quoting ASM:
WACHANGIJI WENGI UPEO WA KUFIKIRI NI MDOGO AU WAANDISHI WANA UPEO MDOGO WA KURIPOTI MAMBO KWA MAANA NYINGINE NI WACHOCHEZI HIVI NI LINI WAANDISHI WA HABARI WATAANDIKA MAKALA ZA MASLAHI YA TAIFA HAINGII AKILINI MKUU WA MKOA MUMLAZIMISHE KATIKA ZAMA HIZI ASHULIKE NA USHIRIKINA MBONA KUCHUNWA NGOZI MBEYA,KUUAWA WATU WENYE
VIPARA KIGOMA ,KUUAWA BIBI VIZEE WENYE MAHO ME[NENO BAYA] NA ALBINO SHINYANGA NI VYA ZAMANI HAKUNA ALIYEANDAMANA UPO UKWELI KUNA UCHOCHEZI WA SIASA NASHAURI MZEE MAKWAIA WA MAKWAIA ANZISHA SHULE YA UANDISHI WA HABARI MAPEMA KUNA UWEZEKANA WA KUFA NA ELIMU YAKO AMBAYO NI ADIMU TUMECHOKA NA MAKANJANJA NASHANGAA HAWAKUITI STUDIO

we sijui umefikiri kabla ya kuandika
Quote
 
 
0 #61 2012-02-23 23:03
polisi wa tanzania ni mali ya nani, iwapo kila mara wanaua raia wanaopaswa kuwalinda, hivi raia wa nchi hii wamekuwa sawa na panya, hawana haki ya kuishi, kazi ya polisi ni kulinda ama kuua na kama unaua unayemlinda wewe unawajibika kwa nani? jamani polisi wa Tza jifunzeni kazi ya polisi nini popote duniani katika nchi za kidemokrasia. msiue mnaopaswa kuwalinda ama hilo jeshi livunjwe na kuundwa upya kwa misingi ya sheria na haki jamii kidemokrasia na si polisi wa kutumwa tu na kuua na kuharibu usalama badala ya kuuhifadhi. kazi yenu kikatiba ni kulinda raia na usalama wao na si kuwaua kamwe!
Quote
 
 
0 #60 2012-02-23 20:43
Huyu mkuu wamkoa ni m[NENO BAYA] sana watu wanaandamana kwa nia ya kutaka polisi iwasake wale wanaowauwa raia wema yeye badala ya kusema jeshi la pilisi liwasake hao wauaji anataja kuwasaka walioandamana hii ni hatari sana na yote inaonyesha jinsi upeo wake ulivyo mdogo kama kokwa ya ndimu,
Quote
 
 
0 #59 2012-02-23 19:50
mungu atawaukumu kwa makosa ya kuuwa raia wasio na atia na ifahmike kwamba kila lenye mwanzo na lina mwisho.mkae mkijua mwisho wenu umekaribia na tutawashitaki kila aliyefanya maovu
Quote
 
 
0 #58 2012-02-23 18:55
Kwa kweli hakukuwa na sababu ya polisi kuingilia maandamano ya amani kama haya ambayo watu walitaka kutoa hisia zao kwa mkuu wa mkoa. Serikali yetu haidhamini maisha ya watu wake na ipo siku laana hizi zitawarudia.
Quote
 
 
0 #57 2012-02-23 18:34
Mimi sioni msada wa watanzania tena katika aldhi hii ya Tanzania nibora wanisaidie kunifanyia mpango nipate uraia angarau wa Somalia kwani kule kunahata msada wa msaraba mwe[NENO BAYA], we ona hata wanaharakati badala ya kishitaki serikali ya tanzania kwenye mahakama kama Theheg wanaishia eti wafikishwe mahakamani; nani awafikishe mahakamani??? Mfano nilafiki yangu

Frederick Fussi
Mwanaharati wa haki za binadamu
Dar es Salaam.

Na malizia "E Mungu tunaomba Walio Mwaga Damu za wenzetu damu hizo ziwe juu yao na uzao wote amina".
Quote
 
 
0 #56 2012-02-23 18:08
Jaman polis wa tz mnataka kuwa kama polis wa kenya?
Quote
 
 
0 #55 2012-02-23 18:02
Polisi, Polisi!!! Hivi jamani polisi wa Tanzania wanahusika na usalama wa akina nani?
Quote
 
 
+1 #54 2012-02-23 17:36
Jeshi la polisi linahitaji kufumuliwa na sheria za usalama kudurusiwa. Hakuna weledi hata kidogo.
Quote
 
 
-6 #53 2012-02-23 17:35
Mimi naona nguvu zimeenda sawa sababu hata hao askari vile vile ni wanaadamu ndio maana hata katika idadi ya majeruhu kuna askari,na kingine sisi wananchi muda mwingine tujaribu kutii amri itapotolea ili kuepusha mambo mengine kutokea.
Quote
 
 
+1 #52 2012-02-23 17:13
jifunzeni kutika mataifa yenye demokrasia,anga lia wallstreet protester nani kapigwa risasi?
Quote
 
 
+3 #51 2012-02-23 17:02
Nadhani sasa wataznzania tumefika pabaya fikra za mkuu wa polisi anapopindisha ukweli eti vurugu ni za kisiasa wakati ukweli unajulikana.Kwa hiyo anataka kuuwambia uma wa watanzania kuwa walioandamana ni wafuasi wa vyama vya upinzani na yeye kama kawaida kapokea amri ya chma tawala kuwa uwa hao nae kauwa.Kama sio atwambie siasa inaingiaje hapo.DAMU HII ITAMWAGIKA LAKINI RAHO ZENU ZITAONJA HUKUMU KULINGANA NA MALIPO YENU.AMEEN
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner