MwanzoContactsEmail
Home Habari Top News Story Muswada wa madini waitoa jasho serikali
BOOKMARK THIS PAGE
Muswada wa madini waitoa jasho serikali  Send to a friend
Wednesday, 21 April 2010 23:20

Habel Chidawali na Frederick Katulanda, Dodoma

MUSWADA wa Sheria mpya ya madini unaendelea kuitoa jasho serikali baada ya jana kukwama kuwasilishwa bungeni kwa siku ya pili bila maelezo.Juzi Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliwaeleza wabunge kuwa muswada huo ambao tayari umeleta mvutano mkubwa katika jamii ungewasilishwa jana baada ya kushindikana Jumatatu iliyopita lakini, tofauti na ahadi hiyo, haukuwamo kwenye ratiba ya shughuli za Bunge.

“Niwaombe wabunge kuwa kesho (jana) tutajadili muswada wa sheria ya madini, niwaombe mkajiandae,” alisema Spika Sitta wakati wa matangazo ya mwisho kabla ya kuahirisha Bunge juzi.

Lakini jana orodha ya shughuli za Bunge hazikuonyesha muswada huo na Spika baadaye aliwatangazia wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini mkutano baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Mbali na mkutano huo wa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, pia Spika Sitta alitangaza mkutano wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baadaye jioni jana.

“Leo muswada wa sheria ya madini hautawasilishwa kwa sababu hali bado ngumu sana, unaendelea kujadiliwa ili kuhakikisha ukiwasilisha haukumbani na upinzani na unapita kwa sababu hiki ni kipindi cha kuelekea uchaguzi,” alieleza mmoja wa wabunge ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini.

Wabunge wengine waliozungumza na gazeti hili jana walisema kitendo cha serikali kushindwa kuwasilisha muswada huo ni dalili ya waziri mwenye dhamana kusoma alama za nyakati na kuugopa kukwama kuupitisha.

"Waziri angelazimisha kuleta Muswada huo ni wazi kuwa angekutana na kiyama kama alichokutana nacho Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambaye wabunge walimgomea katika miswada yake miwili," mbunge mmoja ambaye hakutaka atajwe gazetini alisema.

Wadau walianza kushikwa wasiwasi kuhusu muswada huo pale gazeti hili liliporipoti taarifa za ndani kwamba Rais Jakaya Kikwete ametoa maelekezo maalum kutaka muswada huo ujadiliwe kwa hati ya dharura.

Mbali na wadau mbalimbali kupinga muswada huo waziwazi, Waziri na Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige waliupinga muswada huo hadharani wakati wa semina ya Kamati ya Madini iliyofanyika mjini hapa wiki iliyopita.

Kitendo cha muswada huo  kupingwa na viongozi wa dini na hata mawaziri kimeonekana kuistua serikali kiasi cha kusitisha kuwasilisha haraka hivyo kuamua kuutayarisha upya ili kukidhi mahitaji ya wengi.

“Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, Shelukindo anawatangazia wajumbe wote wa kamati hiyo kuelekea katika kikao cha kamati katika Ukumbi wa Pius Msekwa kuanzia majira ya saa 5 asubuhi,” alisema spika Sitta na kuongeza;

“Nyaraka za sera za madini ziko tayari zimewekwa katika masanduku yenu, naomba mzichukue na kuzisoma kwa makini waheshimiwa wabunge.”

Jana ilikuwa siku ya pili kwa Kamati ya Nishati na Madini kukutana baada ya juzi kutwa nzima wajumbe wake kuendeleza majadiliano hayo hadi usiku jambo linaloonyesha kuwa bado ngoma ni nzito.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini William Shelukindo jana alijifungia na kamati yake na kila alipopigiwa simu ya mkononi iliita bila mafanikio muda wote.

Hata hivyo, Shelukindo aliwahi kukaririwa akisema kamati hiyo haitaweza na wala haithubutu kupitisha vitu ambavyo vinaopnekana wazi kuwa na utata na ambavyo havitakuwa na tija kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Bunge unaoendelea mjini hapa, sheria hiyo ilipaswa kuwasilishwa bungeni tangu siku ya Jumatatu ambapo ungejadiliwa kwa siku mbili hadi jana, lakini haikuweza kuwasilishwa.

Mwishoni mwa wiki Wizara ya Nishati na Madini iliitisha semina katika Ukumbi wa Pius Msekwa ambapo wabunge pamoja na wadau wa madini walionyesha nia ya wazi kuwa walitaka kuukwamisha muswada huo.

Katika semina hiyo, mawaziri wawili walionyesha wazi kuwa walikuwa wanapingana na serikali kuwa hawangekuwa tayari kuunga mkono muswada huo kwa kuwa ulikuwa ukiwakandamiza wananchi.

Jana Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wasira aliliambia Mwananchi kuwa kupinga kwake muswada hakuwa akiikomoa serikali kama alivyoripotiwa katika katika vyombo vya habari bali ilikuwa ni makusudi mazima ya kumsaidia waziri mwenzake.

“Mimi sikuwa napinga muswada hata kidogo kama watu wanavyosema, lakini nilikuwa na kila sababu kwa kuwa nilikuwa namsaidia Waziri mwenzangu pamoja na Watanzania wote ambao wanaguswa katika sekta hiyo,” alisema Wasira.

Kuhusu baadhi ya watu kumtaka ajiuzulu wadhifa huo kutokana na mabishano hayo Wasira alisema “Sina cha kusema” hata alipotakiwa kuendelea kuzungumza zaidi aliondoka na kumuacha mwandishi.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanaonekana kuwatetea mawaziri hao wakisema kuwa ilikuwa ni haki yao na kwamba hawatakiwi kuhukumiwa kwani mabishano yao yalikuwa kwenye semina na sio ndani ya kikao halali.

Kabla ya hapo walishakaa wabunge tena ambapo waliweza kulumbana bila ya mafanikio kwani taarifa za ndani ya kikoa hicho zilidai kuwa kulikuwa na malumbano makali jambo lililothibitishwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

“Ni kweli tulikuwa na malumbano makali sana, lakini ni ya kawaida tu wala sio jambo la kutisha maana kitu kinachogusa masilahi ya nchi hatuwezi kukipitisha hivi hivi tu,” alisema Ziito wakati akizungumza Mwananchi katika viwanja vya Bunge juzi.

 Hata hivyo, habari zilizolifikia Mwananchi kutoka kwa mmoja wa wabunge ambaye ni mdau wa kutoka katika maeneo yanayozalisha madini alisema kuwa muswada huo unatarajia kuwasilishwa siku ya Ijumaa jambo linaloonyesha kuwa wabunge watakuwa wamenyimwa nafasi ya kuchangia.

Siku ya Ijumaa ilikuwa na ratiba za wabunge kupkiea Taarifa za kamati ya Miundombinu kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Utendaji wa kazi usioridhisha wa kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) pamoja na Uendeshaji usioriudhisha wa Shirika la Reli Tanzania uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India

 
Mambo mengine yaliyotarajia kuwasilihwa siku hiyo yaliwasilishwa jana ambayo ni pamoja na taarifa za Hesabu za serikali za Mitaa,Serikali Kuu pamoja na Hesabu za Mashirika ya Umma ambazo zote ziliwasilishwa jana.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 22 April 2010 23:27
 

Comments 

 
0 #21 2011-04-13 12:34
Mwananchi hongela kwa nakala zako lakini kumbuka kuhimiza watanzania kufanya kazi na sio malumbano ya kisiasa. inchi yetu ipo nyuma japo ni kwa sababu ya watu wachache. lakini kila mwananchi wa tanzania awajibike kikamilifu kujenga nchi.
Quote
 
 
0 #20 2010-09-12 07:15
yangu ni kutoa hongera kwa nakala zenu za kiswahili kwani hata kama tuko mbali tunajihisi tuko karibu.
Quote
 
 
0 #19 2010-04-24 14:03
Kamati imetenda kazi iliyotumwA,nawa pa heko,Sita(Mzee wa speed),Simbacha mwene,John Cheyo na Zito kwa kazi nzuri, na wengine ambao walichangia angalau wanachi wa sehemu za madini nao waonekane kama wenye mali badala ya kugeuka ombaomba.
Quote
 
 
+1 #18 2010-04-22 19:50
Wabunge kama kweli mgendua ghiliba za Ngeleja kwa moyo wa dhati basi baneni serikali ili PM PINDA akajinyonge atuambie habari ZA MEREMETA, TANGOLD na wengineo ambao tunadanganywa kuwa eti siri ya jeshii, hivi hili jeshi mshahara wanapata wapi kama si kwa wananchi na wapo kwa masilahi ya wananchi iweje watu tuliowapa dhamana wafanye mambo si ndivyo halafu tuwaone kama watu wa mataifa vile, hao si waganda wala wakenya huko hatuna HAKI YA KUJUA MASUALA yao lakini ya kikosi cha Mwamunyange hapana.

Ni uongo tu wa kuwatisha watanzania na kuficha uchafu, kwa uongo. Ni mamlaka tu ndiyo inayozuia hayo kuwafikia watz lakini sababu za kujua na kuhoji na kuwashitaki pia wenye kutenda makosa.
Wito kwa wabunge baneni serikali ikifikia hatua ya Rais basi kuvunja bunge kwa sababu ya kutaka kujua ukweli tutawaunga mkono!
Quote
 
 
+2 #17 2010-04-22 18:50
Ninazo kila sababu ya kulipongeza gazeti la mwananchi kwa kupewa sura mpya nzuri inayovutia. Binafsi napenda kuwashukuru sana wote waliohusika katka mchakato wa kubadirisha sura ya gazeti la mwananchi. Tunazidi kusonga mbele wala haturudi nyuma.
Quote
 
 
0 #16 2010-04-22 16:33
Kuna kila haja ya watanzania kulipongeza bunge letu kwa kazi nzuri wanayoifanya.Binafsi napata kigugumizi wapi tunaelekea kwa sababu serikali yetu ina wataalamu waliobbobea kuliko hata Bunge letu,kwa nini wanatuandalia mikataba ya ajabu?Ninaomba kuwepo sheria ambayo itawabana wanopeleka nchi pabaya (wanaoacha miiko ya utumishi kwa maslahi yao binafsi au kikundi)kujiuzu lu (sio utashi wa kisiasa) na inapobainika wahukumiwe kifungo cha maisha
Quote
 
 
+1 #15 2010-04-22 15:19
Ewe mwananchi wa Tanzania CCM inatupeleka kwenye dimbwi la umasikini. 2010 imefika piga chini hicho chama hakina dira ya maendeleo.

Kataa CCM ndio kauli mpya ya 2010.
Quote
 
 
0 #14 2010-04-22 15:03
When you see them finding the tricky techniques to enable bill accepted, don't surprise, that is as good as protecting their interest:You want to be knocked stand at their site.No more patriotism;it is now survival for the fittest.
Quote
 
 
+1 #13 2010-04-22 12:26
Mimi kwa kweli sijafurahi mswaada huu kwenda bungeni haraka haraka hivi. ilibidi wananchi ama wadau washirikishwe kabla
Quote
 
 
0 #12 2010-04-22 11:49
Sioni sababu ya ya bunge letu ambalo ni muhimili mkubwa kabisa katika serikali kufanya siasa kwa masuala nyeti kama kama haya; hivi sababu nin nini mswada muhimu hivi wa rasilimali za taifa letu upewe siku moja. Yalipasa bunge kuwa makini kuepuka miscelenous amendments na kupewa muda wa kutosha kuujadili na kuondoa siasa ndani ya mambo muhimu hivi.
Quote
 
 
+1 #11 2010-04-22 11:27
Hongereni kwa kubadili sura ya Gazeti hili.
Quote
 
 
-3 #10 2010-04-22 10:00
Ihave no comment as i trust the concerned committee i hope everything will not left untouched
Quote
 
 
-3 #9 2010-04-22 09:54
MIMI KINACHONICHANGA ZA NI HAWA WABUNGE WETU WA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUWEMO KATIKA MSWADA WA MADINI UNAWAHUSU NINI WAO WAKATI MADINI HAYAMO KTK MUUNGANO,WAO IKIJADILIWA MAMBO HAYA INATAKIKANA WATIKE NA KUIPA HESHIMA SEREKALI YA TANGANYIKA KUJADILI MAMBO YAO.
Quote
 
 
+1 #8 2010-04-22 09:53
Kuwahimiza wananchi wenzangu kuwanyima kura wagombea wenye sifa za kinyama kama tulionao kwa sasa si uchochezi,ni fahari kwa kila mwananchi na hasa Mzalendo wa kweli,ndivyo walivyofanya waasisi wetu. Ubaguzi katika mgawanyo sahihi wa pato la Taifa hauna tofauti na ule ubaguzi wa enzi za kina Voster wa Afrika Kusini,aina ya viongozi tulionao hawatufai,tuwat upe nje maana malengo yao si kutukomboa wananchi wanyonge wa taifa hili,ni maadui wa ustawi wetu,TUWAKATAE kwa nguvu zetu zote. Ikibi kuugomea uchaguzi ili watu wengi zaidi wajiandikishe ili kuunganisha nguvu zaidi kuwatoa wahuni hawa. Truly we are fed up with you. Hatuwataki tena jamani hamtufai,si wafalme ninyi,madaraka ni dhamana ya kufanya uliyoagizwa na wapiga kura wako,mmefanya nini?
Quote
 
 
0 #7 2010-04-22 09:39
Hili ni jambo muhimu kwa sisi Wananchi kulifikiria kwa kina na kuchukua maamuzi sahihi na kwa kasi ya ajabu itakayowatoa nje akina Mhe.Rais na kabineti yake yote. Kwa kutazama aina ya mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya na viongozi wa taasisi nyeti za nchi,hapo utajua ni aina gani ya rais tuliye naye! Ubora wa baba yeyeote nyuma yake kuna watu makini kumuunga mkono. Nini ubora wa Rais Kikwete? Angalia aliowateua,utaj ua,kama walivyo ndivyo na yeye alivyo. Watanzania Mungu wangu tukoje? Tumerogwa? Hatuna jinsi? Sisi ndio tunaweka hao madarakani,je nasi akili zetu kama zao? Yaani ubinafsi,wizi,u badhirifu,kutow ajali katu raia,rushwa ambayo ni kama mavi mapya,tutaje mangapi maana nafasi haitoshi. Nitaandika tena labda mnikatalie,nina uchungu usiopimika wa nchi yangu na watu wake masikini.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner