
| Tucta: JK wawajibishe mawaziri wazembe | Send to a friend |
| Monday, 02 January 2012 22:06 |
|
SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua viongozi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kusababisha kuwepo kwa migogoro ya wafanyakazi nchini.Kauli ya Tucta imekuja siku moja tangu Rais Kikwete adai kwamba anashangazwa na watendaji wanaosababisha kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya stahiki ya watumishi wa umma wakiwemo walimu wakati wamekuwa akitoa maagizo ya mara kwa mara juu ya kulipa stahiki zao mapema. Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, malimbikizo hayo yanatokana na mawaziri wenye dhamana za Utumishi wa Umma na ile ya Kazi na Ajira kushindwa kutii maagizo ya rais, hivyo kusababisha kuwepo kwa malimbikizo hayo. Alisema, mawaziri hao walipaswa kuwahimiza watendaji wao ili kuhakikisha stahiki hizo zinalipwa mapema, lakini mpaka sasa wameshindwa kutimiza wajibu.Mgaya alisema mawaziri hao wanapaswa kuwajibishwa kwa kuchukuliwa hatua na mamlaka ya uteuzi ambayo ni rais. “Tatizo sio Rais, tatizo liko kwa mawaziri wake, wao ndio wenye jukumu la kuwasimamia watendaji wakuu wa wizara zao ili kuhakikisha kuwa stahiki za watumishi wa Umma wakiwemo walimu zinalipwa kwa wakati ili kuondoa migogoro, lakini mpaka sasa hakuna kinachofanyika zaidi ya maneno,wanapaswa kuwajibishwa,”alisema Mgaya. Aliongeza malimbikizo ya malipo ya madeni ya walimu na watumishi wengine ni miongoni mwa vichocheo vya migogoro kazini na kwamba uzembe wa watendaji wakuu unapaswa kukemewa kwa nguvu zote. “Wafanyakazi ni tabaka kubwa nchini na wanachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi, hivyo wanapaswa kutathiminiwa na kuondoa migogoro,”aliongeza Mgaya. Hata hivyo Mgaya alisema pamoja na kauli ya Rais Kikwete, Tucta kwa kushirikiana na Chama Cha Walimu(CWT) watahakikisha mgomo wa walimu ulioitishwa wakati shule zitakapofunguliwa unafakiwa ili kilio chao kiweze kufika kwa Rais na kutambua kuwa watendaji wake wanashindwa kuwajibika. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani















Comments
Anao Mawaziri/Makatibu Wakuu na Wakurugenzi ambao yeye mwenyewe hajui wanachokifanya au kuamua kwa manufaa ya Taifa,hivyo yeye ndio Tatizo katika Ufuatiliaji. Pamoja na kutumia fedha za Uma kwa Semina na vikao vya Uelekezi lakini bado yeye kama mkuu anashindwa kuwa na Uamuzi hata kama nchi i[NENO BAYA]sa waalimu na wataalamu.
Mwanakijiji wa Isanzu-Isene-Iramba.