MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Madaktari sasa watangaza mgomo rasmi
BOOKMARK THIS PAGE
Madaktari sasa watangaza mgomo rasmi  Send to a friend
Monday, 23 January 2012 19:59

Geofrey Nyang’oro
MADAKTARI wametangaza rasmi kuanza mgomo katika hospitali zote za rufaa na vituo mbalimbali vya afya nchini kote hadi hapo madai yao yatakaposhughulikiwa na Serikali.

Pia wamepitisha azimio la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuifumua na kuiunda upya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya kutokana na kile wanachodai kuwa ni kudhalilisha taaluma yao.

Dk Uliomboka pia aliwataja Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa kwamba wanapaswa kuwajibishwa na Rais.

Akitangaza mgomo huo, Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Jumuiya ya Madaktari hao, Dk Stephene Ulimboka alisema hatua hiyo inalenga kupata ufumbuzi wa madai waliyotoa kwa muda mrefu na kuongeza kwamba, leo wanatarajia kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Dk Ulimboka alitaja baadhi ya madai yao kuwa ni kuwawekea mazingira bora ya kazi madaktari kwa kupeleka vifaa vya kazi hospitalini na kwenye vituo vya afya, kuboresha malipo ya posho na kuwapatia sitahili zote wanataalamu hao.

Hata hivyo, tafauti na ilivyokuwa awali, kikao cha jana ambacho kilikuwa cha majumuisho, kilitumika pia kupokea ripoti ya mikutano iliyokuwa ikiongozwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kupokea majukumu ya kuongoza harakati hizo.

“Kuanzia leo tunatangaza kuwa madaktari wote wanaoguswa na hili kote nchini kuacha kufanya kazi hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yetu, tunataka Serikali iboreshe mazingira ya kutolea huduma za afya, ili kumwezesha daktari kumpatia huduma mgonjwa katika kiwango  kinachostahili,” alisema Dk Ulimboka.

Alitaja madai  mengine matatu ambayo kamati anayoiongoza inasimamia kuhakikisha yanatekelezwa kuwa ni pamoja na madaktari kurejeshewa nyumba za kuishi kama inavyoelekezwa kwenye ‘Standard order’ ya Serikali, ambayo inasema daktari atapatiwa nyumba ya kuishi na Serikali na kama sivyo atapatiwa asimilia 30 ya mshahara.

Alisema kipengele hicho kiliondolewa kinyemela bila wao kushirikisha wala kuelezwa sababu za kuondolewa kwake, jambo linalowaongezea ugumu wa maisha na kuwafanya wadharaulike.
Madai mengine yalihusu nyongeza za mishahara, ambayo alisema kumekuwa na ugumu wa kutekeleza suala hilo kila mara hadi wanapofanya mgomo.

“Mwaka 2005 wakati tunaanza kazi, mshahara wa daktari ulikuwa unafikia Sh124, 000, lakini baada ya mgomo ndipo ukapandishwa hadi kufikia karibu ya laki 700,000 sisi tunataka suala hili lirekebishwe na nyongeza yake isisubiri shinikizo,” alisema.

Madai mengine ni malipo kwa madaktari pindi wanapofanya kazi katika mazingira hatarishi na kupendekeza walipwe asimilia 30 ya mshahara wao, posho wakati wa kazi ya ziada ambayo kwa sasa wanalipwa asimilia 10 ya mshahara wao. Kuhusu mshahara, alisema yapo mapendekezo ambayo alisema wataitaarifu Serikali watakapokutana na viongozi wake.Madaktari hao leo wanatarajia kuendelea na mkutano wao katika ukumbi wa Don Bosco.

Rais  wa MAT, Dk Namala Mkopi alisema alikabidhi majukumu kwa kamati iliyoundwa na wanachama baada ya kuonekana kuwa hadi sasa Serikali imekuwa ikiwazungusha.

“Wanachama wamesema hapo mlipofikia tunashukuru mmejitahidi vya kutosha na sasa tunaomba mtukabidhi majukumu ili shughuli hii iweze kusimamiwa na kamati ya madaktari,” alisema Dk Mkopi.

Hatua hiyo imelenga kuongeza wigo wa washiriki ambao watawahusisha madaktari wasio wanachama wa MAT na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo ya afya.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #26 2012-01-26 12:06
duh wakigoma wote jaman tutakufa
Quote
 
 
0 #25 2012-01-24 23:49
Jamani gomeni lakii pia tufikirie wagongonjwa ambao hawana makosa. Gomeni kiustaarabu ili wagonjwa na nyie madaktari mfaidike. Kugoma kiiustaarabu ni kupunguza masaa ya huduma na sio kusimamisha huduma. Ni maana kwamaba asilimia 25 wanagoma na 75% wanakwenda kazini. waliogoma jana leo wanaenda kazini na walioenda kazini jana leo wanagoma na kuendelea ili angalau wale mahutiti watibiwe na wasio mahututi wasubiri mpaka mgomo ukiisha. Tukumbuke sio madaktari tu wenye madai je manesi, watu wa maabara, xray nk.
Quote
 
 
0 #24 2012-01-24 17:36
hivi mnafikiria na wafanyakazi wengine? au kila mtu huvutia kwake? kwa staili madaktari na wabunge lao moja
Quote
 
 
0 #23 2012-01-24 17:23
serikali iwe sikivu madai ya madaktari ni ya msingi.watu hawa wamejitoa kuna wengine wanaambukizwa magonjwa kama vile HIV katika kazi zao.maslahi wanayodai kama nyumba na night allowance ni za kawaida tu..hivi ni pesa gani inalingana na kuokoa maisha ya mtu
Quote
 
 
+1 #22 2012-01-24 17:06
NYIE MNAJISUMBUA, NCHI HII NI YETU WANASIASA,WENYE VITI WA BODI, HIYO 10000 INAWATOSHA. KUPATA KWETU 200000 NA 500000 ZA POSHO INAKUWA NONGWA? MBONA MADAKTARI WALIO KWENYE TAASISI KAMA ZA UKIMWI HAWAGOMI? TUMEWAACHIA WAJICHOTEE,MSIT UNYIME USINGIZI
Quote
 
 
0 #21 2012-01-24 16:53
Ukiwa baba wa familia na ukawa unaahidi watoto wako kuwanunulia kitu na usifanye, matokeo yake watakudharau. Ndivyo serikali ya Tanzania inavyowafanyia madaktari pamoja na walimu ambao ndio mhimili mkubwa wa taifa. Kibaya zaidi wabunge walipitisha posho zao mara moja bila mjadala wowote ndiyo maana wengi tumechukizwa na kitendo hicho.
Quote
 
 
0 #20 2012-01-24 16:27
Madaktari kazeni uzi. Serikali inakimbilia kuilipa DOWANS huku madaktari wetu hawana hata mahali pa kulala. Bila kuikomalia serikali hampati kitu.
Quote
 
 
0 #19 2012-01-24 15:30
Hivi nchi hii haina serikali?
Kwa kweli ni jambo la kuhuzunisha sana kama kweli madaktari wameamua kuitisha mgomo tena.

Serikali mbona inalinyazia hili! maana mtu anapo lalamika kuna kitu pale, maana hata kiumbe chochote kilicho hai kikisikia njaa au kiu huwa dawa ipo ina maana ni chakula au maji.

Tatizo linakuja hapa hawa madaktari wakigoma anayeteseka ni mwanachi wa hali ya chini maana viongozi na matajiri watapata huduma kwanye hospitali za watu binafsi ambazo zimekuwa zikitoza gharama kubwa mno! utadhani ni hotel za kitalii sasa huyu mwananchi wa hali ya chini jamani atakimbilia wapi? ili hali kwa sasa kuna wagonjwa mahututi kila hospitali ambao wanahitaji huduma ya hawa madaktari.

Serikali isijikaushe kana kwamba hawaoni hilo wakati wako vigogo wamekula pesa nyingi za wanachi na wala hawajachukuliwa hatua yeyote ile! sasa utamdanganya daktari nini hapo, walipwe chao muone kama watagoma!

Ninyi viongozi mkiugua mnakimbilia India kutibiwa kwa kodi za wananchi hamumuogopi hata mungu shilingi ngapi imetumika mwaka 2011 kwa vingozi walioenda kutibiwa India, mnatutia kichefuchefu.

Sasa wanagoma fanyeni yale mnayoyafanya kwa kutumia nguvu ya dola sasa mkawapige mabomu hao madaktari maana hawajaandama, ila wamegoma iansikitisha sana!!
Quote
 
 
+2 #18 2012-01-24 14:31
madaktari mna haki kaza buti.hawa wanasiasa wanatuchezea sana.mungu yupo pamoja nanyi
Quote
 
 
+2 #17 2012-01-24 14:02
mi nakuambia sisi tunavumilia kuwa watanzania hatujivunii kuwa watanzania,kwan i moja ya umasikini ni kupoteza matumaini na seri kali hii ya mafisadi inazidi kutuongezea machungu hao ni madaktari tu kuna idara kibao zilizosahaulika ,tuamke sasa
Quote
 
 
+1 #16 2012-01-24 13:22
Serikali sikilizeni matakwa ya Madaktari,wanao hathirika ni Watanzania wasio na uwezo wala hatia,Madai ya Madaktari ni ya Msingi,tunawaun ga mkono kwenye mgomo wenu.
Quote
 
 
+1 #15 2012-01-24 13:22
madaktari kaza buti, mwendo mdundo!! serikali ya CCM haijali watu wake, inajijali yeynyewe ( group la watu. kwa hili nawapa support, leo madr kesho walimu, then wanajeshi hadi kieleweke. kudadadeki!!!!
Quote
 
 
0 #14 2012-01-24 12:30
Quoting Masikini Upepo:
Mnathamini pesa kuliko roho za watanzania masikini ambao ni wagonjwa, hawa madaktari hawana UZALENDO,na kama Serikali inadaiwa pesa na hao madaktari basi serikali ndio wakulaumia iwapo wagonjwa wa[NENO BAYA]sa huduama.


Acha unafiki wewe. Uzalendo maana yake nini? Haya yote ni matokeo ya watu kama ninyi kuingiza madarakani chama cha watu wenye ubinafsi na ulafi, matokeo yake wananchi wasio na hatia wanaumia. Kama serikali haina hela kwa nini haikuwaambia wabunge wasithubutu kutoa madai ya kuongezewa posho, tena mara tatu? Fedha za kuwalipa wabunge wanazo, za kulipa wengine hawana, huu ndiyo unauita uzalendo? Hiki chama hakitatoka madarakani mpaka mchapo nchi hii utembee na Tanzania iwe huru kweli. kudadeki!
Quote
 
 
+1 #13 2012-01-24 12:02
ni kweli kabisa katika hili linatubidi wote tuliopo ktk secta ya afya tuungane tuwe kitu kimoja,naunga mkono hoja.
Quote
 
 
0 #12 2012-01-24 11:47
Mnathamini pesa kuliko roho za watanzania masikini ambao ni wagonjwa, hawa madaktari hawana UZALENDO,na kama Serikali inadaiwa pesa na hao madaktari basi serikali ndio wakulaumia iwapo wagonjwa wa[NENO BAYA]sa huduama.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner