MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Wavulana wapeta matokeo kidato cha nne
BOOKMARK THIS PAGE
Wavulana wapeta matokeo kidato cha nne  Send to a friend
Wednesday, 08 February 2012 21:57

Fredy Azzah
BARAZA la Mtihani la Taifa(Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa asilimia 53.59 ya wanafunzi 426,314 waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Hata hivyo, wakati asilimia hiyo ambayo ni sawa na wanafunzi 180,216 wakifurahia matokeo hayo, wenzao 3,301 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu ikiwamo mfanano usio wa kawaida wa majibu. Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako alisema wasichana waliofaulu ni 90,885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni 134,241 sawa na asilimia 57.51.

“Mwaka  2010 watahiniwa waliofaulu walikuwa 223,085 sawa na asilimia 50.74, hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.63,” alifafanua  Dk  Ndalichako. Wanafunzi 10 bora Dk Ndalichako aliwataja wanafunzi 10 bora kitaifa kuwa ni Moses Andrew Swai kutoka shule ya Feza Boys,  Rosalyn  Tandau kutoka Marian Girls, Mboni Mumba kutoka St Francis Girls na  Sepiso Mwamelo kutoka St Francis Girls. Wengine na shule zao kwenye mabano ni  Uwella Rubuga (Marian Girls), Hellen Mpanduji (St Mary’s Mazinde Juu), Daniel Wallace Maugo (St Joseph Millennium), Benjamin Tilubuzya, (Thomas More Machrina), Simon Mbangalukela (St. Joseph Millennium) na Nimrod Rutatora (Feza Boys).

Wasichana 10 bora
 Kwa upande wa wasichana kumi bora, Dk Ndalichako aliwataja na shule walizotoka kwenye mabano kuwa ni Rosalyn (Marian Girls), Mboni  (St Francis Girls),  Sepiso Mwamelo (St Francis Girls),  Uwella Rubuga (Marian Girls) na Hellen Mpanduji (St Mary’s Mazinde Juu). Wengine ni Lisa Chille (St Francis Girls Mbeya), Elizabeth Ng’imba (St Francis Girls Mbeya), Doris Noah (Kandoto Sayansi Girls),  Herieth Machunda  (St Francis Girls Mbeya) na Daisy Mugenyi (Kifungilo Girls Tanga).

Wavulana 10 bora  
Wavulana kumi waliofanya vizuri zaidi katika mtihani humo ni Moses Andrew Swai (Feza Boys), Daniel Maugo (St Joseph Millennium), Benjamini Tilubuzya, (Thomas More Machrina), Simon Mbangalukela (St. Joseph Millenium) na Nimrod Rutatora (Feza Boys). Wengine ni Simon Mnyele (Feza Boys), Paschal Madukwa (Nyegezi Seminary), Henry Stanlay (St Joseph Millenium), Fransisco Kibasa (Mzumbe) na Tumain Charles (Iliboru).

Shule 10 bora 

Matokeo hayo yanaonyesha shule kumi bora zenye zaidi ya watahiniwa 40 kuwa ni St. Francis Girls ya Mbeya, Feza Boys, St Joseph Millenium,  Marian Girls,  Don Bosco Seminary, Kasima Seminary,  St. Mary’s Mazinde Juu,  Canossa, Mzumbe na Kihaba.

Matokeo hayo yanaonyesha pia  shule 10 bora zenye watahiniwa chini ya 40 kuwa ni Thomas  More Machrina, Feza Girls, Dungunyi Seminary,  Maua Seminary,  Rubya Seminary, St Joseph Kilocha Seminary, Sengerema Seminary,  Lumumba,  Queen of Apostles- Ushirombo na Bihawana Junior Seminary. 

Shule 10 za mwisho 

Shule kumi za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 40 ni Bwebwera, Pande Daraja, Mufindi, Zirai, Kasokala, Tongoni, Mofu, Mziwa, Maneromango na Kibuta. Na shule kumi za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40 ni Ndongosi, St Luke, Igingwa, Kining’inila, Ndaoya,  Kilangali, Kikulyungu, Usunga, Mto bubu day na  Miguruwe. Waliofutiwa matokeo Dk Ndalichako alifafanua zaidi kuwa watahiniwa 3,301  waliobainika kufanya udanganyifu wamefutiwa matokeo na hawataruhusiwa kufanya mtihani wowote wa Necta kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.  

Dk Ndalichako alisema  kati yao watahiniwa waliofanya mtihani huo walikuwa 426,314, sawa na asilimia 94.67 ya watahiniwa wote waliosajiliwa. “Mwaka 2010 watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 458,114  hivyo, idadi ya watahiniwa imepungua kwa watahiniwa 7,790 sawa na asilimia 1.70,” alisema Dk Ndalichako. Alisema  mwaka jana, watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 349,39 na watahiniwa huku wa kujitegemea wakiwa ni 100,934.  Akifafanua zaidi juu ya matokeo hayo, Mtendaji Mkuu huyo wa Necta alisema watahiniwa 450,324 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambao  wasichana ni 201,799, sawa na asilimia 44.81 na wavulana 248,525, sawa na asilimia 55.19. Alisema  jumla ya watahiniwa wa shule 180,216 sawa na asilimia 53.59 ya waliofanya mtihani wa kidato cha nne wamefaulu, kati yao wasichana wakiwa 69,913 na wavulana 110,303.

Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, waliofaulu ni 44,910  wasichana wakiwa 20,972 na wavulana 23,938.

Waliofutiwa mitihani 

Dk Ndalichako alisema  Necta imefuta matokeo ya watahiniwa 3,03 waliobainika kufanya udanganyifu kati yao,  watahiniwa wa shule ni 3,301 na wawili wakiwa wa maarifa (QT). Akifafanua zaidi juu ya udanganyifu huo alisema , 182 walikamatwa na wasimamizi wakiwa na makaratasi (notes) sita walikamatwa na simu, watatu walikuwa wakifanyiwa mtihani na watu wengine, wanne walisajiliwa kufanya mtihani kwa majina ya watu wengine.

 Dk Ndalichako aliongeza kwamba,  pia   watahiniwa 2,896 karatasi zao za majibu zilikuwa na mfanano usio wa kawaida, 155 karatasi zao za majibu  zilikuwa na miandiko zaidi ya mmoja, 14 kubadilishana karatasi katika chumba cha mtihani, 18 kukamatwa na karatasi za majibu zaidi ya moja, 25 wakiwa  na mfanano usio wa kawaida wa majibu ,  kuwa na vikaratasi  ama kubadilishana vikaratasi. “Mtu mmoja unakuta mitihani  yake ya majibu ina miandiko zaidi ya 10, na jeshi la polisi ndilo lililothibitisha kuwa miandiko ya wanafunzi hawa ilikuwa inatofautiana. Alisema pia kuwa, baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa nane walioandika matusi ya nguoni kwenye karatasi zao za majibu.  “Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu kinaonyesha utovu wa nidhamu, hivyo pamoja na kuwafutia matokeo ufuatiliaji zaidi unaendelea ili kuona hatua za kuwachukulia,” alisema Dk Ndalichako.

Pia alitoa onyo kali kwa vituo vilivyohusika na udanganyifu huo, huku akisema kwa vilivyobaika vitaandikiwa barua ya kutaka vijieleze kwa nini visifutiwe matokeo. Dk Ndalichako akielezea zaidi juu ya hali hiyo, alisema baadhi ya watahiniwa waliandika nyimbo za  kizazi kipya  (Bongo fleva) kwenye karatasi zao za majibu huku wengine wakichora michoro isiyo eleweka na wachezaji wa mpira. “Mwingine aliandika bongo fleva,  ngoja niwasomee ‘wasahihishaji msinisamehe..., acha utani na girl wangu, najukuja home nakukuta.. nikifeli mtihani naendelea na fani ya muziki,” Dk Ndalichako alisoma moja ya karatasi za majibu za watahiniwa hao huku akiruka baadhi ya maeneo akisema ameandika matusi yasiyoweza kusomeka.

Ubora wa ufaulu kwa jinsi  

Dk Ndalichako  alisema  ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha kuwa, jumla ya watahiniwa 33,577 sawa na asilimia 9.98 wamefaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu.  

“Wasichana waliofaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu ni 10,313 sawa na asilimia 7.13 na wavulana ni 23,267, sawa na asilimia 12.13,” alisema Dk Ndalichako. Aliongeza kwamba,  waliopata daraja la nne ni 146,639 sawa na asilimia 43.60 ambao wavulana ni  87,039 sawa na asilimia 45.40 na wasichana 59,600, sawa na asilimia 41.22. Dk Ndalichoka aliongeza kwamba,  waliofeli ni 0156,089  sawa na asilimia 46.41, kati yao wavulana wakiwa 81,418 sawa na asilimia 42.47 na wasichana wakiwa 74,667, sawa na asilimia 51.64. mwisho


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 09 February 2012 09:16
 

Comments 

 
0 #17 2012-02-10 10:49
Yatupasa tujiulize hizo shule za sekondari hazina mahabara, hazina library, kweli mtoto kushinda itakuwa ni ngumu. Aliyenacho ataongezewa zaidi kwani atakuwa na uwezo wa kumsomesha mtoto shule nzuri. Ambaye amenyimwa ndio hivyo siku zote atakuwa ni kilio tu.
Quote
 
 
0 #16 2012-02-10 00:13
inasikitisha sana bora hizo shule za Kata wazifute tu.wamezijenga kwa ajili ya kufanyia kampeni zao kpnd cha Uchaguzi.Watoto hao waliofeli wataenda wapi maskini?maana hata waliolist paper feli mby mno.uwiiiii hii ndo Tz!!!!!tutapata je kupona?tutalima wapi?Kilimo kwanza aridhi inaporwa?Mhhhhh sijui
Quote
 
 
0 #15 2012-02-09 18:44
Hawa watoto hatuwapi elimu bali tunawapeleka vituo vya kuwakuza tu, hebu tupate mchanganuo wa waliofaulu na waliopata mimba na kuolewa mashuleni tutajua kazi ya shule hizi. Taifa limepoteza dira
Quote
 
 
+1 #14 2012-02-09 18:18
pengine sababu ya kufeli kwa wanafunzi ni walimu hawashibi
Quote
 
 
0 #13 2012-02-09 15:16
Mbona baraza mnaeleza tu kwa ujumla na sehemu muhimu mnataja faster? au hamtaki tujue? 2mewastukia! kwa kifupi walofaulu sio asilimia 53.59 kwa sababu mwenye Div IV nae kafeli ila waliofaulu ni asilimia 9.98 tu kama mlivyo sema kwasababu hawa ndo wana daraja la kwanza mpaka la tatu ambapo madaraja haya ndo yanamuwezesha mwanafunzi kuendelea mbele ki masomo. so it is hopless kabisa na mnatakiwa kuwajibika.
Quote
 
 
+4 #12 2012-02-09 12:11
WALIMU WAMEBUNI MFUMO WA KUFUNDISHIA UNAITWA F.U.K.U (YAANI FUNDISHA KADIRI ULIPWAVYO)
Quote
 
 
+5 #11 2012-02-09 11:40
Kwa wasioelewa! unapoambiwa 52% wamefaulu ujue wamepata kuanzia daraja la 1 hadi la 4. kwa hiyo 48% wamepata zero.
Aibu kubwa sana.
Quote
 
 
+4 #10 2012-02-09 11:15
Kati ya "waliofaulu" zaidi ya asilimia 70 wamepata Div IV. Hivi siku hizi mwanafunzi aliyepata hizo marks anaenda high school? Taifa limekwisha. Naomba baraza litupe takwimu za wangapi wamepata Div I, II, III na IV kulinganisha na mwaka jana tujue tuanelekea wapi. Lakini Kama mtoto wa mheshimiwa anasoma private school unategemea nani ajali shule za serikali kwa mlalahoi
Quote
 
 
+2 #9 2012-02-09 10:30
Hizi ni dalili za taifa kuteketea, kwani katika taifa lolote Elimu ndo roho ya taifa, kama elimu yetu ndo ina sura hii na serikali haichukui hatua zozote basi nchi finished!
Quote
 
 
0 #8 2012-02-09 10:26
Tunaomba takwimu sahihi za waliofaulu na waliofeli mbona takwimu zinachanganya?
Quote
 
 
0 #7 2012-02-09 10:06
Sii haki kwa watahiniwa wa shule za sekondari za Kata ambazo hazina huduma muhimu kutahiniwa kwa kiwango kile kile na kwa kipimo kile kile na wanafunzi wanaosoma shule zenye waalimu wazuri, Maabara, Maktaba na huduma zinazowawezesha kujifunza na kufaulu.
Quote
 
 
0 #6 2012-02-09 09:58
Hawa watoto walioandika [NENO BAYA] wafunguliwe mashitaka ili kulinusuru Taifa kwa u[NENO BAYA] wa watoto waliomaliza kidato cha nne.
Quote
 
 
0 #5 2012-02-09 08:57
46.41% wamepata sifuri kabisa ni hatari sana
Quote
 
 
+1 #4 2012-02-09 07:55
SAFI SANA WALIMU SISI TUENDELEZE MGOMO KWA NJIA HII HII,TUJIWEKEE MALENGO MPAKA 2014 95%ZIRO NA 5% WAMEFAULU ILISERIKALI TUWEZE KUKAA NAYO MEZA MOJA KWANI HAIONI UMUHIMU WA WAALIMU
Quote
 
 
+2 #3 2012-02-09 07:49
serikali inajisifu kuanzisha shule za kata ni za nini? mi naona ni kiwanda cha kutengeneza div 0.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner