MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Watafiti wa kimataifa watua Samunge
BOOKMARK THIS PAGE
Watafiti wa kimataifa watua Samunge  Send to a friend
Wednesday, 22 February 2012 21:03

Mussa Juma, Arusha
WATAFITI wa kimataifa wa masuala ya tiba na wanahabari kutoka Japan wamefika Samunge kuendelea kutafiti dawa inayotolewana Mchungaji Ambilikile Masapila.

Mmoja wa wasaidizi wa Mchungaji Masapila, Paulo Dudui, alisema Wajapani hao wamefika hivi karibuni na watafiti wengine tokanchi za ulay ikiwepo Ujeremani na Uingereza .

“Wanakuja watafiti wanachukua dawa wanasema wamepata taarifa za dawa hizo wakiwa nchi kwao,” alisema Dudui.
Akizungumzia tiba hiyo, Dudui alisema bado inatolewa ingawa ni watu wachache wanaofika.
“Watu wanakuja na babu bado anasema kuna miujiza mingine itakuja na anaendelea na ujenzi wa kituo kipya cha tiba,” alisema Dudui.

Kampuni ya Simu ya Vodacom haitafunga huduma zake Kijiji cha Samunge , wilayani Ngorongoro, ambako maelfu ya watu walikuwa wakifika kupata kikombe cha tiba kwa Mchungaji Masapila licha ya sasa watu kupungua na wanaofika wengi ni watafiti.

Kampuni kadhaa ya simu zilifikisha huduma zake Samunge kuanzia Mei mwaka jana kutokana na kufurika kwa watu kupata kikombe cha tiba, lakini sasa baadhi ya kampuni zimesitisha huduma eneo hilo.
Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando, alisema wakazi wa Samunge wataendelea kupata huduma zote za kampuni hiyo.

“Ni kweli kuwa hivi sasa kuna wateja wachache Samunge na ni gharama kuendesha mtambo kule, lakini Vodacom hatutafunga mawasiliano kwani kuna wateja wetu wengi eneo hilo,” alisema Kamando.

Alisema wateja hao na wengine wa Mkoa wa Arusha na maeneo mengine, wamekuwa wakinufaika na huduma za kampuni hiyo, ikiwapo ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao.

Awali, Meneja wa Vodacom Arusha, Jerome Munishi, alisema kampuni hiyo mkoani hapa ina mawakala 600 ambao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #6 2012-02-24 02:31
mi nataka kupata ukweli wa kisayansi je ni kweli watu wamepona? basi wajitokeze wapimwe ili tupate ukweli
Quote
 
 
0 #5 2012-02-24 00:40
nikiskia swala la vodacom najiskia vibaya mno maana huduma zenu ni mbovu kupita kiasi,hela ilileta shida kwenye Mpesa tangu tarehe za mwanzoni mwezi2 sh 300000 mpaka leo mmeshindwa kunifanikishia kila siku naambiwa subiri masaa 24 sasa hiyo ni huduma gani?
Quote
 
 
0 #4 2012-02-23 16:35
HAWANA HAJA YA KWENDA SAMUNGE KWANI WAMECHELEWA WAWAFANYIE UTAFITI WALIOKUNYWA DAWA IWAPO INA MADHARA TUMESUBIRI MAJIBU KUTOKA WHO BILA MAFANIKIO IKIZINGA[NENO BAYA] UGUNDUZI WA MTU MWEUSI HAUTAMBULIWI NA WAZUNGU MBONA NABII TB JOSHUA WA NIGERIA HATANGAZWI NA WAZUNGU
Quote
 
 
0 #3 2012-02-23 16:08
BABU MSANII
Quote
 
 
0 #2 2012-02-23 14:05
huyo mzee mjanja sana sasahv anajenga kituo kikubwa cha afya kikimaliza kujengwa ndio atasema kuna miujiza mingine anayo ili awakamue vizuri , ndio mana amesema kuna kuujiza mwingine unakuja karibu , anasubiri tu hiyo klinik yake iwe tayari ndio atangaze .
Quote
 
 
+3 #1 2012-02-23 11:46
Mbona mwandishi wa makala hii huelewiki? Mumeandika kwamba Vodacom watafunga mitambo yao Samunge huku munasema tena Mkoa wa Arusha yaani Samunge muna wateja wengi sana ambao wamekuwa wakinufaika na huduma za vodacom, hii typing mbona haieleweki? Munatuchanganya wasomaji wenu.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner