MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Kalembo amsimamisha kazi mkurugenzi wa hamlashauri Tanga
BOOKMARK THIS PAGE
Kalembo amsimamisha kazi mkurugenzi wa hamlashauri Tanga  Send to a friend
Monday, 31 May 2010 19:37

Burhani Yakub,Tanga

SAKATA la ujenzi na ukarabati wa barabara ya Raskazone-Bombo, limeingia katika sura mpya baada ya Mkuu  wa Mkoa wa Tanga Meja Jenerali Mstaafu, Said Kalembo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo, Majuto Mbuguyu.

Kalembo amemsimamisha kazi Mbuguyu kwa kukiuka agizo la la Bodi ya Barabara mkoa lililomtaka kusimamisha kazi ya ukarabati wa barabara ya eneo la Mkonge mpaka Raskazoni kwa kiwango cha lami.

Kazi hiyo ya ukarabati wa Barabara yenye urefu wa kilometa mbili na nusu ilitarajiwa kugharimu  zaidi ya Sh575milioni hadi kukamilika.

Taarifa za mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo unamuelekeza Mkandarasi huyo kukwangua tabaka la juu na kisha kushindilia kabla ya
kuweka lami jambo ambalo hata hivyo limefanyika kinyume kwa kuchimbua mawe yote na kuweka kokoto.

"Tofauti na mkataba unavyosema na hata maagizo ya Bodi ya Barabara, mkandarasi ameendelea kuchimba barabara na kutoa mawe, hii ni dharau
kubwa",alisema Kalembo.

Kalembo pia aliwaweka mahabusu kwenye Kituo cha Polisi Chumbageni
Tanga, mkandarasi wa kampuni inayojenga barabara hiyo  Ediya Mwalusya, Mavumira Bori,Dereva wa Trekta Ayub Yakub pamoja na Injinia wa Barabara wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Arafat Kaniki waliokutwa wakisimamia kazi  katika eneo la Barabara hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa aliyekuwa ameongozana na Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Paul Chikira na Mkuu wa wilaya ya Tanga Dk Ibrahimu Msengi aliamua kufanya ziara ya ghafla kwenye eneo hilo baada ya kubaini kuwa agizo lililotolewa na Bodi ya Barabara mapema mwezi Mei mwaka huu limekiukwa.

“Hivi inakuaje agizo litolewe na Bodi ya Barabara ya mkoa ambayo
Mwenyekiti wake ni Mimi mwenyewe Mkuu wa mkoa likiukwe, yaani mpaka leo mnaendelea kuchimba hivi mnadhani sisi wote hatujasoma eeeh...?, RAS andika barua DED namsimamisha kazi kuanzia leo.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa mkoa, Ofisi yake iliandika barua
ya kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kusimamisha kazi hiyo mara moja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Majuto Mbuguyu alisema kuwa alitoa taarifa za mdomo kwa mkandarasi huyo na kwamba hata yeye haelewi sababu za mkandarasi kutotii maagizo ya bodi na kuendelea na kazi.

“Mimi nilimwambia kwa mdomo tu tena niliongea na yule mkurugenzi na walisimama, lakini, nashangaa kwa nini wameendelea kuchimba Barabara, hata mimi Mheshimiwa sielewi?”,alisema Mbuguyu.

Hivi karibuni katika kikao cha Bodi ya Barabara, Kalembo
alimsimamisha kazi na kumfukuza kwenye kikao Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Rickson Lema kwa madai ya kushindwa kutoa maelezo ya
kitaalamu kuhusiana na ujenzi wa Barabara hiyo.

Mawe yaliyokuwa yakiendelea kutolewa katika Barabara hiyo yameanza kuibwa na watu wasiojulikana.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2010-06-01 09:38
“Hivi inakuaje agizo litolewe na Bodi ya Barabara ya mkoa ambayo
Mwenyekiti wake ni Mimi mwenyewe Mkuu wa mkoa likiukwe, yaani mpaka leo mnaendelea kuchimba hivi mnadhani sisi wote hatujasoma eeeh...?, RAS andika barua DED namsimamisha kazi kuanzia leo.

kwa hiyo kalembo amechukua mamlaka ya pinda sasa yeye ni waziri mkuu duh hapa patamu...

haya ndio matatizo ya kuwa na katiba mbovu iliyopitwa na wakati inayoruhusu kila kiongozi kuwa na mamlaka na kuingilia majukumu ya mtu mwingine... mkoa mmja vyeo kibao; mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mwenyekiti/meya wa halmashauri, diwani, katibu kata, mwenyekiti wa kijiji, afisa mtendaji, Mkurugenzi wa Halmashauri/Jiji,... hapo bado hawajaorozeshwa wakuu wa kitaifa kama rais, waziri mkuu,...

sasa hatuelewi iwapo mkuu wa mkoa akituhumiwa kutenda kosa nae mkurugenzi ana mamlaka ya kumsimamisha?

ole sendeka vs mkuu wa mkoa manyara = katiba bomu
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner