MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Ripoti mgonjwa wa sindano tata MNH yatua kwa waziri
BOOKMARK THIS PAGE
Ripoti mgonjwa wa sindano tata MNH yatua kwa waziri  Send to a friend
Wednesday, 22 February 2012 21:18

James Magai
RIPOTI ya uchunguzi wa sakata la kudungwa sindano tata mtoto Imran Mwerangi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imekamilika na tayari imepelekwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi.
Imrani alidungwa sindano hiyo miezi sita iliyopita na kumfanya alazwe katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), baada ya kupata mtindio wa ubongo na mwili kupooza.

Taarifa zilizopatikana jana zilisema kuwa jopo madaktari limegundua ‘madudu’ katika suala hilo hatua ambayo uongozi wa MNH umeona uombe kwanza ushauri wa wizara kabla ya kuanza kulishughulikia.

Alhamisi iliyopita, uongozi wa MNH ulikutana na mama wa mtoto huyo, Amina Mwerangi na kumtaarifu kuwa umeunda jopo la madaktari bingwa kuchunguza suala hilo na kuahidi kutoa taarifa Jumatatu juma hili.
Hata hivyo, juzi uongozi wa hospitali hiyo ulishindwa kuwakabidhi wazazi wa mtoto huyo taarifa hiyo ambayo wamekuwa wakiisubiri kwa hamu ili kujua hatima ya mtoto wao.

Jana, habari zilieleza kuwa tayari jopo la madaktari lililoundwa kuchunguza suala hilo limeshakamilisha kazi yake na liliikabidhi ripoti yake kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dk Merina Njelekela.

Baba wa mtoto
Baba wa mtoto huyo Iddy Mwerangi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dodoma, alisema waliitwa jana asubuhi ofisini kwa Dk Njelekela na kuelezwa kuwa ripoti hiyo imekamilika.
“Alisema ripoti imekamilika lakini wameiandikia barua wizara kuomba maelekezo ya hatua za kuchukua,” alisema Mwerangi akimnukuu Dk Njelekela.

Mwerangi alisema licha ya Dk Njelekela kukiri kuipokea taarifa hiyo, hakuikabidhi kwa familia kama alivyoahidi wala familia hiyo haikuelezwa kilichomo zaidi ya kuambiwa kunahitajika kwanza ushauri wa wizara.
Alisema uongozi wa MNH umekiri kuwa tatizo la awali la mtoto huyo yaani mtindio wa ubongo na kuvimba tezi za pua, bado halijashughulikiwa na kwamba linahitaji ufumbuzi wa haraka huku tatizo jipya alilolipata hospitalini hapo likiwa ni la kudumu hali itakayomfanya awe tegemezi.

Alisema pamoja na hayo, wamekubaliana kuwa mtoto huyo ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa hospitali mpaka wizara itakapotoa maelekezo.

Baba huyo wa mtoto alisema, Profesa Victor Mwafyongo na Dk Mulungu wataendelea kumwangalia kwa karibu mtoto huyo na kuwasiliana kwa karibu na wazazi.

Hata hivyo, alisema familia yake haikuridhishwa na uongozi wa Muhimbili kushindwa kuchukua hatua za haraka baada ya taarifa hiyo kukamilika ili kupata ufumbuzi wa haraka wa matatizo yanayomkabili mtoto huyo.
Mwerangi alisema baada ya kupata taarifa hizo, walikaa na kuzitafakari na sasa wanatafuta ushauri kwa baadhi ya wataalamu wa tiba ambao nao wameeleza kutoridhishwa na mlolongo wa utaratibu huo ambao unachelewesha kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya mtoto.

Alisema kwa mujibu wa wataalamu hao, baada y ripoti hiyo kukamilika, hospitali ilikuwa na uwezo wa kufanya uamuzi na kuitaarifu tu wizara na si kuomba na kusubiri maelekezo yake.

“Mtoto yuko kwenye critical condition, (hali mbaya) hivyo inaweza kufikia mahali kwamba sasa amepata rufaa kupelekwa kwa mfano, India kwa matibabu zaidi tukaambiwa kuwa tumeshamchelewesha kwa hiyo hata kwa matibabu ambayo yangeweza kufanyika basi yakashindikana,” alisema.

Alisema wanajipanga leo kumwandikia barua Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda kumwomba aingilie kati na kutoa tamko ili hatua za haraka za matibabu ziweze kuchukuliwa, kwa kuwa amekaa ICU muda kwa mrefu na hakuna lolote lililofanyika.

Dk Njelekela pamoja na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaeshi hawakupatika jana kuzungumzia ripoti hiyo baada ya simu zao za mkononi kuita bila kupokewa.

Yaliyomsibu mtoto
Mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa nyama zilizokuwa puani lakini alidungwa sindano tata iliyomuathiri zaidi afya yake.

Baada ya kudungwa sindano tata, familia iliitaka hospitali hiyo kutoa maelezo ya kuridhisha baada ya baadhi ya madaktari na wahudumu wa hospitali hiyo kutaka kumrejesha nyumbani akiwa katika hali hiyo isiyo na matumaini.
Katika barua hiyo ya Januari 10, mwaka huu, Mwerangi licha ya malalamiko hayo, aliomba maelezo ya kuridhisha kuhusu tatizo hilo na ufumbuzi wake.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #7 2012-02-24 09:22
Natumaini serikali inayaona haya makosa ya madaktari wetu sasa cha msingi sio malumbano tena ni kufanya haraka huyo mtoto ampatiwe haraka matibabu nje ya nchi kwa gharama zozote ili kuokoa maisha yake.Pia hao waliofanya madudu yao wachukuliwe hatua za kisheria haraka ili iwe mfano kwa wengine.
Quote
 
 
0 #6 2012-02-23 18:11
Quoting ABDULAHAMAN JUMA:
Napenda kutumia jukwa hili kuwajulisha juu ya walimu 28 wa Wilya ya Newala ambao halmashauri ya wilaya iliwapa ruhusa ya kwenda kusoma, cha kushangaza mwezi huu wa febr 2012 hawajapata mishahara yao, inasemekana wakati wa ukaguzi wa watumishi document za walimu hawa hazikuonekana kwenye mafaili yao yalioko halmashauri, ndiomaana wakaguzi walichukua jukumu la kuwakatia mishahara yao. ombi langu kwa mhalili wa gazeti hili kuweka bayana jambo hili ili wale ambao wanaathirika na swala hili waelewe nini kinaendelea, kwani mishahara hiyo ndiyo inayotumika kuendeshea maisha ya watumishi hawa, ikumbukwe makosa ni yawatumishi wa afisaelimu au mkurugenzi kutokutunza kumbukumbu, sasa kwanini waathirika wawe watumishi? na je, halmashauri imewasaidiaje watumishi hao kwa muda huu wote. ni matumainiyangu ombi langu mtalifanyia kazi. WALIMU HAWA HAWAKUTOROKA VIYUONI BALI WALIPEWA RUHUSA NA MKURUGENZI KWANINI WANATESWA KIASI HIKI.


Sasa hii inahusiana vipi na hii story ya huyu mtoto??????
Quote
 
 
-1 #5 2012-02-23 17:31
Napenda kutumia jukwa hili kuwajulisha juu ya walimu 28 wa Wilya ya Newala ambao halmashauri ya wilaya iliwapa ruhusa ya kwenda kusoma, cha kushangaza mwezi huu wa febr 2012 hawajapata mishahara yao, inasemekana wakati wa ukaguzi wa watumishi document za walimu hawa hazikuonekana kwenye mafaili yao yalioko halmashauri, ndiomaana wakaguzi walichukua jukumu la kuwakatia mishahara yao. ombi langu kwa mhalili wa gazeti hili kuweka bayana jambo hili ili wale ambao wanaathirika na swala hili waelewe nini kinaendelea, kwani mishahara hiyo ndiyo inayotumika kuendeshea maisha ya watumishi hawa, ikumbukwe makosa ni yawatumishi wa afisaelimu au mkurugenzi kutokutunza kumbukumbu, sasa kwanini waathirika wawe watumishi? na je, halmashauri imewasaidiaje watumishi hao kwa muda huu wote. ni matumainiyangu ombi langu mtalifanyia kazi. WALIMU HAWA HAWAKUTOROKA VIYUONI BALI WALIPEWA RUHUSA NA MKURUGENZI KWANINI WANATESWA KIASI HIKI.
Quote
 
 
0 #4 2012-02-23 13:46
Jamani Serikali mpelekeni mtoto huyu asiye na hatia India haraka kuokoa maisha yake,hapa kwetu hatuwezi.baba na mama wa mtoto Mungu wetu awapiganie mko ktk kipindi kigumu sote ni wazazi tunajua uchungu wa mtoto.
Quote
 
 
+1 #3 2012-02-23 10:05
Mamtu mengine bana tabu tu! Ukiyakuta yanaomba kuongezewa posho na mishahala, yanakomaaaa! Lakini hakuna ufanisi katika utendaji wao wa kazi, utasikia tumpeleke india, sasa nyinyi mlisomea nini kama kila kitu india! Eti madaktari bingwa! Mtoke tuajiri wahindi basi! Mnaboa sana nyie madaktari uchwara! siasa mpaka kwenye magonjwa!
Quote
 
 
0 #2 2012-02-23 08:42
eeeee bwana mungu okoa maisha ya huyu kijana kwani bila matarajio hakutegemea kukumbana na mateso alonayo leo. wahusika wanajua walikosea wapi ila hatutoi lawama yawezekana mungu anajua kwa nini wamefanya hayo waliyoyafanya. mungu akusaidie kwani wewe ni kiumbe chake. amin
Quote
 
 
+1 #1 2012-02-23 03:47
Wazazi wapewe report hiyo mapema iwezekanavyo ili wachukue hatua zozote za haraka wakishirikiana na Serikali ambayo ndiyo iliyohusika na uzembe huo wote ili kwa pamoja wajue ni jinsi gani wanaweza kufanya katika mchakato mzima wa matibabu ya mtoto huyo...
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner