
| Mgomo wa Tucta kujulikana Juni 5 | Send to a friend |
| Monday, 31 May 2010 19:41 |
|
SHIRIKISHO la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta), linatarajia kutoa tamko la kugoma au kuacha Juni 5, baada ya kukaa kwenye kikao cha majadiliano Juni 4 mwaka huu. Hatua hiyo imekuja mara baada ya serikali kushindwa kutoa tamko la makubaliano yao ya kikao cha utatu kilichofanyika Mei 8 mwaka huu, ambapo kwa mujibu wa sheria, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, anapaswa kutoa taarifa ya kikao hicho ndani ya siku 21. Akizungumza na Mwananchi kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya alisema kuwa, kutokana na serikali kushindwa kutoa taarifa yoyote ndani ya siku hizo, baraza linaloratibu mgomo litatoa tamko lake. Alisema wafanyakazi wamekuwa kimya kutokana na kusubiri tamko la serikali kuhusiana na kikao chao hicho, ambapo mpaka sasa waziri ameshindwa kutoa taarifa yoyote kutokana na hali hiyo watakaa kikao hicho kwa ajili ya kujadili hatua zitakazofuatwa na wafanyakazi hao. “Tunatarajia kufanya kikao cha mwisho siku ya Ijumaa, ambacho kitatoa mwelekeo wa wafanyakazi kufanya mgomo au la, kwa sababu tulikuwa tunasubiri tamko la makubaliano kutoka serikalini, lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika badala yake waziri amekaa kimya,"alisema Mgaya. Aliongeza kutokana na hali hiyo baraza hilo limesikitishwa na hatua hiyo, kwa sasa wanaendelea na mikutano ya ndani kwa ajili ya kupanga utaratibu watakaotumia wakati wa kutoa tamko hilo. Alisema malalamiko ya wafanyakazi juu ya nyongeza ya mishahara ni ya muda mferu, lakini mpaka sasa serikali imeshindwa kuchukua hatua zozote juu ya suala hilo, jambo ambalo linawafanya waamini kuwa wafanyakazi wanadharauliwa. “Wafanyakazi ndio wanaokuza uchumi wana chi, lakini wanarudishwa nyuma na baadhi ya viongozi kwa kuwadharau na kutosikiliza matatizo yao, jambo ambalo linawafanya waingie kwenye mgogoro mkubwa namna hii na serikali,”anaongeza. Kwa mujibu wa Mgaya, mbali na tamko hilo pia,siku hiyo hiyo shirikisho hilo litatoa taarifa za kutaka kumshitaki waziri huyo kutokana na kutangaza mishahara yenye mapungufu katika baadhi ya vipengele. Awali, Tucta ilitoa mapendekezo ya nyongeza ya mishahara baada ya kufanya tathimini na kubaini kuwa, kutokana na hali ngumu ya maisha, wafanyakazi wanalipwa kiasi kidogo. Tucta ilitoa mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara kutoka Sh 84,000 hadi 315,000 kwa mwezi, jambo ambalo serikali imedai kuwa haina uwezo wa kuwalipa. Mbali na mapendekezo hayo, Tucta imeitaka serikali kupunguza makato ya kodi ya mifuko ya hifadhi ya jamii na kodi. Kutokana na hali hiyo Tucta ilitangaza mgomo huo ambapo awali ulitakiwa kuanza Mei 5 mwaka huu, baada ya serikali kuwaomba warudi kwenye meza ya majadiliano. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani















Comments