|
Mtoto akutwa amekufa kwenye banda la video |
Send to a friend |
|
Thursday, 02 September 2010 22:19 |
|
Joel Malebeja
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti jijini Dar es Salaam akiwemo mtoto wa miaka mitano ambaye mwili wake ulikutwa ndani ya banda la video.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema mwili wa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Said,ulikutwa ndani ya banda la kuonyesha video eneo la Vingunguti Kiembe mbuzi. Shilogile alisema mwili wa mtoto huyo ambao ulikuwa hauna jeraha lolote, ulikutwa asubuhi na mmiliki wa banda hilo ambaye hakujulikana jina lake.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Amana kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Katika tukio la pili, maiti ya mwaume mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Beno(45) imekutwa ikiwa inaelea kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi Kigamboni.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 11 jioni katika eneo la Kigamboni Kisiwani , ambapo maiti hiyo ilikutwa na wakazi wa eneo hilo ikiwa haina jeraha lolote.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke ,David Misime alisema kuwa mwili wa marehemu umehifdahiwa katika hospitali ya Vijibweni kwa uchunguzi zaidi.
Katika hatua nyingine, mkazi wa Tandika, Ahmed Rashidi (41) alikutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia shuka alilolitandika juu ya dari.
Misime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 3 asubuhi katika eneo la Tandika Tambuka Reli.
Misime alisema sababu za kujinyonga marehemu bado hazijafahamika isipokuwa kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, enzi ya uhai wake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa Moyo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katka hospitali ya Temeke kwa uchunguzi zaidi
|