MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Polisi Tz, Interpol wakamata magari 50 ya wizi
BOOKMARK THIS PAGE
Polisi Tz, Interpol wakamata magari 50 ya wizi  Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 22:23

Boniface Meena

JESHI la Polisi Nchini kwa kushirikiana na Makao Makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Polisi (Interpol), limekamata magari 51 yaliyoibwa kutoka nje ya Tanzania na baadaye kuingizwa nchini.

Magari hayo yalikamatwa katika operesheni maalumu iliyofanyika kati ya Agosti 27 na 28 mwaka huu, kwa ajili ya kuwasaka, kuwatambua na kuwakamata wahalifu mbalimbali nchini.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini,Peter Kivuyo, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa operesheni hiyo ilifanyika kulingana vipaumbele vya Mashirikiano ya Majeshi ya Interpol,  Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya Kusini mwa Afrika na Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki.

Alisema mbali na magari hayo, katika kipindi hicho cha siku mbili, polisi pia walikamata wahamiaji haramu 42, silaha haramu 13, risasi 506 na kilogramu 40,001 za dawa za kulevya.

Alisema magari 22 miongoni mwa hayo yaliibwa Japan,  12 Afrika Kusini na mengine matatu yaliibwa Uingereza.

Alisema gari moja limeibwa nchini Kenya.

Alitaja nchi zingine ambako magari yaliibwa na idadi ya magari hayo ikiwa katika mabano kuwa ni Tanzania (1), Malaysia (8), Slovenia (1), Ujerumaji (1), Msumbiji (1). Alisema magari 10 yameonekana na kasoro kadhaa ikiwamo nyaraka na chesisi tofauti.

 Kivuyo alisema jeshi hilo pia limekamata  wahamiaji haramu 42 wanaoishi nchini kinyume na sheria.

Alisema polisi litaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisheria dhidi ya wale wote wanaojihusisha na matendo ya uhalifu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
  • Kupiga Kura

  • Jumapili


Ajali ya Meli ZnZ inatufundisha nini?