MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Kinondoni yaongoza wizi wa magari nchini
BOOKMARK THIS PAGE
Kinondoni yaongoza wizi wa magari nchini  Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 22:24

Boniface Meena

WILAYA ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imetajwa kuwa ndiyo inayongoza kwa wizi wa magari baada ya Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na makao makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Polisi (Interpol) kukamata magari 12 kati ya 51 yaliyoibwa nje ya nchi na kuingizwa nchini.

Hilo ni doa jingine kwa wilaya hiyo ambayo imekuwa ikiripotiwa kwa ufisadi unaofanyika kwenye uuzwaji wa viwanja na pia kashfa ya biashara ya dawa za kulevya ambayo inaonekana kuwa sugu kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu taarifa za taaisisi hizo mbili, wilaya hiyo inafuatiwa na visiwa vya Zanzibar ambako yamekamwatwa magari nane, wakati Wilaya ya Ilala inafuatia kuwa kukutwa na magari matano na Mbeya magari matatu.

Magari hayo pamoja na mengine yanafika idadi ya magari 51 yaliyoibwa nje ya nchi na kuingizwa nchini kwa mujibu wa jeshi la polisi.

Magari hayo yalikamatwa katika operesheni maalumu iliyofanywa kati ya Agosti 27 na 28 mwaka huu kwa ajili ya kuwasaka, kuwatambua na kuwakamata wahalifu mbalimbali nchini.

Naibu mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCP), Peter Kivuyo aliwaambia waandishi wa habari jana operesheni hiyo ilifanyika kulingana vipaumbele vya Interpol, Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya Kusini mwa Afrika na Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki.

Kivuyo alisema mbali na magari hayo, katika kipindi hicho cha siku mbili, polisi walikamata wahamiaji haramu 42, silaha haramu 13, risasi 506 na kilo 40,001 za dawa za kulevya.
Alifafanua kuwa kati ya magari hayo, magari 22 yaliibwa nchini Japan, magari 12 nchini Afrika Kusini, magari matatu Uingereza na gari moja limeibwa nchini Kenya.

Alitaja nchi nyingine ambako magari hayo yametoka kuwa ni Tanzania (1), Malaysia (8), Slovenia (1), Ujerumani (1), Msumbiji (1). Alisema magari 10 yameonekana na kasoro kadhaa ikiwamo nyaraka na chesisi tofauti.

DCP Kivuyo pia alisema jeshi hilo pia limekamata jumla ya wahamiaji haramu 42 wanaoishi nchini kinyume na sheria ambapo raia wa Somalia walikamatwa 14, Burundi 24, Congo mmoja, Kenya wawili, na Zambia mmoja.

Jeshi hilo limefanikiwa kukamata jumla ya silaha haramu ambazo ni risasi 506 na kwamba bunduki aina ya SMG zilizokamatwa ni saba, bastola moja, gobore moja, G3  moja, Riffle moja, Short Gun moja na bomu la mkono moja.

Kwa upande wa dawa za kulevya, jeshi hilo limekamata jumla ya kilo 243 za dawa aina ya heroin, kilo 39, 958 za bangi, kilo 43 za mirungi na watuhumiwa waliokamatwa ni 38.
“Operesheni hii inaitwa “OPERESHENI MODJADJI” iliendeshwa kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizokusanywa kutoka kwa wananchi na wadau wengine na polisi ilizingatia misingi ya sheria na utawala bora,” alisema.

Alisema polisi litaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisheria dhidi ya wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na wale wote wanaofadhili au kuchochea uhalifu na amewasihi wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo ili amani iweze kudumu katika jamii.

Kwa upande wa silaha haramu mikoa inayoongoza ni Shinyanga, Manyara na Kigoma na kwa upande wa wahamiaji haramu mikoa inayoongoza ni Kigoma, Mbeya na Mwanza.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
  • Kupiga Kura

  • Jumapili


Ajali ya Meli ZnZ inatufundisha nini?